Tengeneza Blog Yako Leo na Upate Faida Hizi Tano

  Tunaishi kwenye kipindi ambacho teknolojia imekua kwa kiwango kikubwa sana kushinda kipindi chochote kilichowahi kutokea. Na katika kukua huku kwa teknolojia mtandao wa internet imekua kwa kiwango kikubwa sana na watu wengi sana wamenufaika na mtandao.

  Mtandao wa internet umetumika sana kwenye biashara na mawasiliano. Katika makampuni kumi bora duniani makampuni zaidi ya matano yanafanya biashara inayohusisha internet.  Internet imekuza biashara nyingi sana kwa sasa. Internet imetengeneza mabilionea wengi sana na mmoja wao ni mmiliki wa Facebook(soma habari yake hapa).

             blog

  Wewe unatumia internet mara nyingi na inawezekana kila siku. Swali ni je unafaidika vipi na matumizi hayo ya internet? Unaweza kuwa unanufaika kwa kujifunza na kuhamasika kupitia vitu mbalimbali unavyosoma kwa njia ya mtandao(kama unavyosoma hapa AMKA MTANZANIA ). Kuna njia nyingine ambayo unaweza kuitumia kufaidika na internet kwa kiwango kikubwa sana na ukakuza biashara yako ama ujuzi wako. Kwa shughuli yoyote unayofanya, iwe umeajiriwa, umejiajiri ama unafanya biashara kama mpaka sasa hujaanza kutumia manufaa ya internet kuikuza unakosea sana. Iwe unatoa bidhaa ama huduma, internet ni sehemu muhimu sana ya kukuza biashara ama ujuzi wako.

  Njia unayoweza kuitumia wewe kufaidika na internet ni kuwa na BLOG. Tofauti na inavyoonekana kwamba kutumia mitandao hii inabidi uwe na ujuzi wa ziada, kuwa na blog haihitaji ujuzi mkubwa wa ziada zaidi ya ulionao sasa. Kama umeweza kusoma hapa ina maana una email ama una akaunti facebook. Kama umeweza kufungua email ama facebook basi unaweza kuendesha blog tena kwa kiwango kikubwa sana.

 

  Ni faida zipi utazipata kwa kuwa na BLOG?

  Kuna faida nyingi sana za kuwa na blog kama ilivyo kwa faida za kutumia internet. Hapa nitakueleza faida tano za muhimu ambazo utazipata kama utaamua kuwa na blog yako.

1. Kukuza biashara yako ama utaalamu wako. Kwa biashara ama kazi yoyote unayofanya ni muhimu sana kuwa karibu na watu unaowahudumia. Na kwa kuwa watu wanapokuwa na tatizo huwa wanatafuta suluhisho kwa kupitia mtandao, ni rahisi kukutana na wewe na ukakuza biashara yako ama huduma unayotoa.

2. Kuwa mtaalamu na unabobea kwenye ujuzi wako. Kama unafanya biashara unaweza kuwa unaandika kuhusu biashara yako. Kama unafanya kazi unaweza kutumia blog kueleza mambo yanayohusiana na kazi yako. Kwa njia hiyo itakufanya utake kujua mengi zaidi na hivyo kuzidi kuwa mtaalamu zaidi.

3. Kutoa elimu au kuwahamasisha watu wengine. Unaweza kuniuliza kwa kutoa elimu wewe unanufaika nini? Kuna faida kubwa sana kama utaamua kuwaelimisha watu kwa jambo fulani ambalo unalijua. Utatengeneza mahusiano mazuri na watu na baadae unaweza kutengeneza biashara kwa kupitia mafundisho yako.

4. Kuibua vipaji vyako vingine. Huenda wewe ni mwandishi mzuri ila hujijui. Huenda wewe ni mshauri mzuri ila hujawahi kujua hilo. Huenda wewe ni msanii mzuri na unaweza kutunga hadithi nzuri, mashairi mazuri ila hujawahi kupata nafasi ya kujua hilo. Ukiwa na blog na ukachagua kitu unachopenda kuandika jinsi muda unavyozidi kwenda utaanza kuwa bora kwenye uandishi na kwenye kile unachoandika. Baadae unaweza kujikuta umekuwa mtaalamu mkubwa kwenye hicho unachoandika na ukafaidika kwa kiasi kikubwa sana.

5. Kutengeneza PESA. Najua hiki ndicho wengi wanachofikiria linapokuja swala la kuwa na blog. Ni kweli kwa kuwa na blog unaweza kutengeneza fedha nyingi sana tena zisizo na kikomo, ila sio kitu ambacho kitatokea mara moja. Huwezi kufungua blog leo halafu mwezi ujao ukaanza kutengeneza mamilioni kupitia blog hiyo, ni lazima uwekeze muda na utaalamu wa kile unachoandika ili baadae upate nafasi ya kutengeneza mamilioni kupitia blog yako. Kwa kufikiria unaweza kupata fedha za haraka kwa kuwa na blog utajikuta unashawishika kuweka picha za uchi ili watu wengi watembelee. Kwa kufanya hivyo utaharibu haiba yako na bado hutopata fedha unazotegemea kupata. Ni nani anayeweza kumlipa mtu anayesambaza picha za uchi?

  Kwa kuwa na blog unaweza kupata faida nyingi sana, ila sio kitu ambacho kitatokea mapema. Ni lazima uwekeze muda na utaalamu wa kitu unachoandika au kufundisha. Pia uvumilivu ni muhimu ili kufikia lengo ulilojiwekea kupitia blog.

  Kama unataka kutengeneza blog yako na hujui ni wapi pa kuanzia basi ondoa shaka maana umeshapata jibu lako hapa. Wasiliana na mimi kupitia 0717396253 au andika email kwenda amakirita@gmail.com Kama tayari una blog na unahitaji kuikuza zaidi pia wasiliana na mimi kwa ushauri zaidi.

 

  Kwa maelezo zaidi juu ya kupata huduma ya kuanzisha na kuboresha blog yako bonyeza maandishi haya

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: