UMUHIMU WA KIJANA KUJIAJIRI NA KUWA MJASIRIAMALI KATIKA KIPINDI HIKI

Makala hii imeandikwa na Charles Nazi.
Hali ya uchumi duniani imekuwa ngumu si hapa kwetu Tanzania tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea. Uwezo wa serikali nyingi duniani hasa wa kutoa huduma kwa watu wake unazidi kupungua kutokana na serikali nyingi kuelemewa na madeni. Matatizo yaliyosababisha hali hii ni pamoja na; kushuka kwa thamani ya pesa, kupanda kwa deni la taifa, ongezeko la watu, kupanda kwa bei ya mafuta, makampuni kufilisika na wafanyakazi kupunguzwa kazini na kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali kwa jamii. Hali hii inazidi kuwagusa watu wengi zaidi duniani pengo la masikini na matajiri linazidi kuwa kubwa na tabaka la kati linaanza kutoweka. Vijana wanaomaliza masomo vyuo vikuu wanazidi kuongezeka huku ajira zikizidi kupungua na kupatikana kwake kukizidi kuwa kugumu.

Je suluhisho la hali hii ni nini? Ni kujiajiri na kuwa mjasiriamali.
Hali hii ikiendelea kama ilivyo kutakuwa na matabaka mawili tu duniani yaani matajiri na masikini. Je unawezaje kuepuka kuingia katika tabaka la umasikini na kuingia katika tabaka la matajiri? Suluhisho ni kuwa mjasiriamali kwa kujifunza na kutekeleza kwa vitendo mbinu za ujasiriamali. Kuna kipindi mnamo mwaka 2010 nilipata bahati ya kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wanaosoma vyuo vikuu kule mbeya niliulizwa swali na mwanafunzi mmoja kwamba ‘ Jee sisi wasomi tunaomaliza vyuo vikuu tutafanya nini ili kujikwamua kiuchumi? Tukitafuta kazi hazipatikani na tukitaka kufanya biashara tunakosa mtaji. Mimi niliwajibu kuwa watumie maarifa niliyowafundisha kuangalia fursa zilizopo ili kuanzisha biashara. Suala hili liliendelea kunisumbua akilini hadi nilipoamua kuanzisha kampuni yangu ya ushauri ijulikanayo kwa jina la CPM Business Consultants ndipo niliamua kuanzisha mpango wa kutoa fursa ya vijana wasomi wa ngazi ya Diploma na Shahada ya chuo kikuu, kujiajiri kupitia mpango wa kuwafundisha kuwa Washauri wa biashara.

Wasifu wa CPM Business Consultants
CPM Business Consultants ni Kampuni anayojishughulisha na kutoa ushauri wa biahshara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia inatoa ushauri kwa wa uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO, makampuni, Mashirika ya umma na Taasisi za serikali. Kampuni hii imeajiri washauri wa biashara waliobobea katika fani ya biashara na uchumi waliohitimu shahada za Masters (MBA) kutoka vyuo vikuu humu nchini na nje ya nchi. Pia washauri wanao uzoefu wa miaka mingi kwa kufanya kazi katika taasisi za serikali mashirika na makampuni ya ndani ya nchi na ya kimataifa. Makao makuu ya Ofisi yetu yako Sinza kwa Remi, Dar es salaam.

Kampuni yetu imeanzisha utaratibu wa kupanua shughuli zake kuwa na matawi mikoani ambayo yatajitegemea kwa kuwa na ofisi, kulipia leseni na kupata mafunzo ya kujengewa uwezo. Wamiliki wa matawi wasomi watatakiwa kulipa sh. 300,000 kwa ajili ya mafunzo ya ushauri wa biashara. Pia watalipia leseni ya tawi na gharama zote za uendeshaji. Matawi yatafundishwa namna ya kutafuta kazi za ushauri na wateja wa ushauri. Ili waweze kupata mapato na kuendesha ofisi zao watatakiwa kutafuta kazi za ushauri.
Kwa upande wa CPM Business Consultants itatoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa matawi, itatoa Registration certificate,kwa ajili ya kurahisisha kupata leseni na kufungua tawi. Itatoa mfumo wa uendeshaji wa ofisi,masomo kama semina za ujasiriamali,kujiandaa kustaafu na mfumo wa kuandaa mchanganuo. Pia itatoa ushirikiano kwenye kutoa wawezeshaji wa mafunzo na ushauri kwenye tawi kwa malipo endapo itapatikana kazi kubwa ambayo tawi halitakuwa na uwezo nayo. Kabla ya kufungua tawi CPM Business Consultants na kiongozi wa tawi watasaini mkataba wa ushirikiano (Memorandum of understanding).
Kwa kupata fursa hii vijana wataweza kuanzisha biashara ya Ushauri wa biashara kwa urahisi. Huduma hii inahitajika sana mikoani na kuna soko kubwa. Huduma ambazo watazitoa baada ya kupata mafunzo ni kutoa ushauri wa biashara, kuendesha semina za ujasiriamali, kuendesha semina za namna ya kujiandaa kustaafu, kuandaa mchanganuo kwa ajili ya kuombea mikopo, Kuuza vitabu vya ujasiriamali na kutoa ushauri kwa makampuni kwa kushirikiana na CPM Business Consultants. Faida ya kuwa mshauri wa biashara ni kwamba biashara hii ina malipo mazuri sana hasa ukipata maelekezo mazuri namna ya kuifanya kwa ufanisi unaweza kupata mapato ambayo mtu anaweza kulipwa kwa mwezi ndani ya siku moja tu. Biashara hii unaweza kuianza kwa mtaji mdogo kulinganisha na biashara zingine ambazo zinahitaji uwe na mtaji mkubwa wa kunnua bidhaa au malighafi mashine nk. Ni matumaini yangu kwamba vijana wasomi mtachangamkia fursa hii. Sifa za mwombaji wa kujiunga na fursa hii ni kuwa na stashahada(diploma) toka chuo chochote au shahada(degree) ya kwanza au ya pili ya chuo kikuu. Pia kuwa na moyo wa ujasiri wa kuweza kuthubutu kuanzisha biashara yako na CPM Business Consultants watakusaidia kufika kwenye ndoto yako.

Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0755394701

http://cpmbusinessconsult.wordpress.com/

kitabu kava tangazo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: