Makala hii imeandikwa na  Mwakatika Geofrey

Kuboresha utendaji wako katika kazi ni mojawapo ya faida inayotokana na mtu kuwa na mawazo chanya akilini mwake. Unapokuwa na mtizamo/mawazo chanya akilini mwako unaweza kufanya mambo mengi mazuri yenye manufaa kwa ajili ya maisha yako hata kufikia hatua ya kuboresha utendaji wako wa kazi unapokuwa kazini . Mambo kama haya huwa hayatokei kwa watu wengi sana. Lazima ufahamu kuwa mafanikio yako katika kazi kwa kiasi kikubwa yanategemea mtizamo wako na jinsi gani unatumia muda wako unapokuwa kazini au katika shughuli yoyote ile yenye manufaa au faida kwenye maisha yako. MAKALA HII INALENGA KUKUSAIDIA WEWE BINAFSI JINSI UNAVYOWEZA KUBORESHAUTENDAJI WAKO WA KAZI UNAPOKUWA KAZINI AU KATIKA SHUGHULI YOYOTE ILE.

NJIA 4 RAHISI SANA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA ILI KUBORESHA UTENDAJI WAKO UNAPOKUWA KAZINI

1.JIFUNZE JINSI YA KUSIMAMIA VIPAUMBELE VYAKO.

Ili kuboresha utendaji wako katika kazi ni lazima uwe na uwezo wa kuweka vipaumbele. Lazima uweke tofauti au utenganishe kati ya vitu ambvyo ni muhimu na vyenye manufaa kwenye kazi yako na kwa ajili yako wewe mwenyewe na vitu vile ambavyo havina faida yoyote ile katika kazi yako na ndani ya maisha yako unapokabiliana na majukumu mengi ya kila siku. Pia ni lazima uwe na hisia za haraka sana pamoja na tabia ya kuhakikisha kila kazi inafanyika kwa haraka sana.

2.JARIBU KUWA MTU MWENYE MAWAZO/MTAZAMO CHANYA.

Njia nyingine inayoweza kuboresha utendaji wako unapokuwa kazini ni wewe binafsi kuendeleza tabia ya kuwa na mitazamo chanya kuhusu wewe mwenyewe pamoja na kazi yako. Kadri unavyozidi kuwa na mitazamo chanya unapokuwa katika kazi ndivyo unavyofungua milango yenye fusa nyingi zaidi kuja kwako na kuanza kuboresha maisha yako.

3.BORESHA UJUZI WAKO.

Boresha utendaji wako katika kazi kwa kuendelea kuboresha ujuzi wako kuhusiana na kazi unayoifanya na hakikisha kuwa mwajiri wako anajua kuhusiana na mipango yako. Unaweza kutafuta kozi za ziada ambazo unaweza kuchukua ili kuboresha utendaji wako unapokuwa kazini . Vilevile unaweza kujadili kozi hizo pamoja na bosi wako. Unaweza kumuuliza bosi wako ni vitabu gani ambavyo unahitaji kuvisoma au kuvisikiliza (audio books). Na kama akipendekeza kitu au jambo lolote lile chukua ushauri wake mara moja, kisha unaweza kurudi tena kwake na kuomba ushauri zaidi. Lazima utashangazwa sana jinsi njia hii inavyoweza kukuweka karibu na mtu ambaye anaweza kukusaidia katika kila hatua ya kazi yako.

4.KUWA NA UTU UNAPOKUWA KAZINI.

Lazima ufahamu kuwa asilimia 85 ya mafanikio yako katika kazi yatakuja kutokana na utu wako na uwezo wako wa kuwasiliana vizuri na wengine unapokuwa kazini au sehemu yoyote ile. Kwa hiyo ni muhimu sana wewe kuwa na heshima pamoja na nidhamu nzuri sana unapokuwa kazini pamoja na wafanyakazi wenzio. Tabia hii ya kuwa na utu si tu itaboresha utendaji wako katika kazi bali pia itawafanya watu wengine wawe wanataka kukusaidia kutokana na tabia yako ya usikivu,heshima kwao unapokuwa kazini.

Fanya mambo haya manne na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye kazi yako.

TUPO PAMOJA

Unaweza kusoma makala nzuri zaidi za Mwakatika Geofrey kwa kutembelea blog yake geofreymwakatika.blogspot.com bonyeza hiyo link kufungua.

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

kitabu-kava-tangazo432