Habari za leo msomaji wa AMKA MTANZANIA, nafurahi kwa wewe kuendelea kujifunza na kubadili maisha yako kwa yale unayojifunza kupitia AMKA MTANZANIA. Watu wengi wamekuwa wakinishirikisha ni jinsi gani mambo wanayoyasoma yamebadili mitazamo yao na wanaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yao. Hata kama wewe hujaniandikia bado ninaamini kuna kitu fulani cha kipekee ambacho unakipata na unaona mabadiliko hata kama ni kidogo sana. Nina uhakika huo kwa sababu mambo haya ambayo nimekuwa nikikushirikisha hapa nimeyatumia kwenye maisha yangu na yananiletea mabadiliko makubwa sana.

Leo nataka tujadili kidogo umuhimu wa wewe kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na kama huna uwezo huo ndio muhimu zaidi kwako.

Kwanza kabisa KISIMA CHA MAARIFA ni mtandao pacha wa AMKA MTANZANIA ambao umejikita zaidi kwenye MAFANIKIO MAKUBWA.

Kupitia KISIMA CHA MAARIFA unajifunza mambo yote yanayohusiana na mafanikio kwenye kazi, biashara, na hata maisha kwa ujumla. Na hapo utajifunza kujenga tabia za mafanikio, kuacha tabia zinazokuzuia kufikia mafanikio na hata kukuwezesha kufikia mafanikio ya kiwango cha kimataifa(WORLD CLASS). Mambo yote haya unajifunza kila siku na hivyo kama ukizingatia na kuyatumia unakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio.

Kujiunga na KISIMA kuna gharama kidogo unazohitaji kuchangia ili kuweza kupata mambo yote haya mazuri. Gharama hizi zimegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo;

1. BRONZE MEMBER. Uanachama huu unapata nafasi ya kusoma na kujifunza kuhusu ujasiriamali na biashara na pia kujenga tabia za mafanikio. Gharama yake ni shilingi elfu kumi kwa mwaka.

2. SILVER MEMBER. Uanachama huu unapata nafasi ya kusoma vyote anavyopata BRONZE na unapata pia nafasi ya kusoma uchambuzi wa vitabu vya mafanikio. Gharama yake ni shilingi elfu thelathini kwa mwaka.

3. GOLD MEMBER. Uanachama huu unasoma vyote wanavyosoma SILVER NA BRONZE na pia unapata nafasi ya kujifunza kuhusu mafanikio ya kiwango cha kimataifa(WORLD CLASS), Unapata nafasi ya kujua fursa mbalimbali za kiuchumi na kibiashara na pia unapata baadhi ya AUDIO BOOKS na VIDEO zinazohusiana na mafanikio. Gharama ya uanachama huu ni shilingi elfu hamsini kwa mwaka.

Kwa nini ni muhimu sana wewe kujiunga na uanachama wa GOLD.

Kwanza kabisa sahau kuhusu uanachama mwingine na nataka nikuambie kwa nini ni muhimu sana kwako kuwa GOLD MEMBER wa KISIMA. Najua jibu lako la kwanza ni SINA FEDHA, ELFU HAMSINI NI KUBWA SANA.

Sasa hii ndio sababu kubwa kwa nini ujiunge na uanachama huu. Kama hujanielewa vizuri namaanisha hivi; sababu kubwa ya wewe kujiunga na kisima kwa uanachama wa GOLD ni kwa sababu huna hiyo fedha ya kujiunga.

Hebu tujaribu kuwa wawazi kidogo, kama kweli unafanya kazi au biashara na kwa mwaka mzima unashindwa kuwekeza shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kujifunza na kujiendeleza, hiyo kazi inakupeleka wapi? Kama umefanya kazi au biashara kwa miaka miwili, mitano au hata kumi na bado huwezi kuwa na shilingi elfu hamsini ya kujifunza zaidi hutoweza kuongeza kipato chako na kila siku utaendelea kulalamika.

Kinachokuzuia mapaka sasa unashindwa kuongeza kipato chako ni kwa sababu hujapata elimu sahihi ya kukusaidia kufanya hivyo. Unafanya kazi au biashara yako kwa mazoea na ndio maana hupati mafanikio makubwa. Unaishi maisha ya kukimbiza fedha kila siku kwa sababu umekosa mbinu nzuri za kukufanya ufikie mafanikio makubwa.

Hii ndio sababu kubwa inayotakiwa kukusukuma sasa hivi leo hii ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa sababu jinsi unavyozidi kuchelewa ndio unavyozidi kupoteza nafasi ya wewe kufikia mafanikio makubwa.

Fanya chochote utakachofanya, iwe ni kukopa, kuuza kitu ambacho hutumii sana au hata kuomba mchango ili upate fedha ya kujiunga kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kama umefanya yote kabisa na umeshindwa kupata fedha ya kujiunga tafadhali nitumie email kwenye amakirita@gmail.com na tujadiliane vizuri jinsi unavyoweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Napenda sana wewe ujifunze na kufikia mafanikio makubwa, hivyo kama kweli una kiu ya kufanya hivyo tuwasiliane na nina uhakika tutapata njia nzuri ya wewe kuweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hilo neno ikishafunguka jaza fomu kwa kuweka username na password na utengeneze akaunti yako. Baada ya hapo unatuma fedha kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 na unatuma username au email uliyojiunga nayo kwa meseji kisha unapewa ruhusa ya kusoma na kujifunza.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

TUKO PAMOJA NA TUKUTANE KILELENI.

KWA-NINI-SIO-TAJIRI