Hizi Ndizo Nguvu Tatu Za Kukupa Maisha Unayoyatamani.

Wengi wetu huwa tunapenda kuishi kwenye maisha ambayo tunaridhika nayo na ambayo tumeyachagua. Ugumu unakuja pale ambapo wengi wetu huwa hatuelewi namna ya kuyafikia au kuyapata maisha hayo tunayoyatamani, hasa tunapolinganisha na hali halisi inayotuzunguka.

Hata hivyo, zana au vifaa kwa ajili ya kazi hiyo ya kuyatengeneza maisha hayo tunayoyataka tunavyo, ni suala la kuanza kuvitumia tu. Hivi ni vifaa muhimu kwako kuvijua na kuvitumia, kwani vitakupa nguvu ya kufikia maisha unayoyatamani uwe nayo katika maisha yako.
Inawezekana umekuwa ukipanga malengo na mipango yako kwa uzuri kabisa, lakini umekuwa ukishindwa kuyafikia kama vile unavyotaka kutokana na wewe kushindwa kutumia vizuri zana au vifaa hivi ambavyo unavyo. Unaweza ukawa unajiuliza vifaa hivyo ni vipi? 
Vifaa hivyo ni mawazo yetu, maneno yetu na hisia zetu. Inaonekana kushangaza kidogo. Hata hivyo, ukweli ndiyo huo. Suala la kuvitumia vifaa hivyo linahitaji zoezi la kutosha linalohusu kuvifanyia kazi kwa vitendo, kwa nguvu zetu zote, na kwa hekima zetu zote.
Ili kufanikisha jambo hili, kila mmoja wetu anapaswa kuwa makini na mwangalifu kwa kila kifaa anachopaswa kukitumia, tunapaswa tukumbuke kwamba , ndani ya kila wazo tunalofikiria kuna nguvu iliyobebwa na wazo hilo ambayo hatimaye hujitokeza katika hali halisi.
Na kwa kila neno tunalolitamka kuelekea kwetu wenyewe au kwa watu wengine kuna nguvu pia ndani ya neno hilo. Na kila hisia tunayoishi, kuna nguvu inayokuwemo ndani yake. ( Unaweza ukasoma pia Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Ubongo Wako Kukupa Utajiri Unaoutaka )
Kujitambua kwamba wewe umezaliwa ndani ya nguvu za kiubunifu za ulimwengu huu, ni jambo muhimu sana kwako. Kwani, unapotambua na kuamini kwamba, tuna fursa mbalimbali katika maisha na kwamba changamoto mbalimbali za kimaisha hazina nguvu dhidi yetu, kama tulivyokuwa tukiamini hapo kabla, basi maisha yetu yataboreka na kutajirika.
Kumbuka kwamba, nguvu ya ulimwengu huu wakati wote inamiminika kwenye vifaa hivyo. Jinsi unavyofikiria , unavyoongea na unavyohisi unakuwa unatumia vifaa hivi.  Kusudi kuu la vifaa hivi ni kukusaidia uweze kujua kwamba , nguvu ya ulimwengu huu inamiminika kupitia kwako.
Ni suala tu la kuelewa ukweli huo na kuanza kuufanyia kazi. Kwa kukubali na kuelewa kwamba, nguvu hiyo ipo, utaanza kuelewa kwa kina kwamba nguvu hiyo ndiyo uzoefu wako, na ndiyo muonekano halisi wa maisha yako na wewe mwenyewe. 
Hivyo basi, hatua za mwanzo kabisa unazopaswa kuzichukua ili uweze kuvitumia vifaa hivyo nilivyovitaja ni kujiambia wewe mwenyewe kwamba, unapaswa kuzingatia ubora wa nguvu hiyo inayotokana na mawazo yako. Jiulize iwapo mawazo yako hayo yanakupa nguvu ya kutenda, yanakuhamasisha na yanakubaliana na ndoto zako.
Je, mawazo hayo yanakuchochea na kukutia moyo wewe binafsi pamoja na wenzako? na yanakusaidia utazame mbele zaidi au yanaelekeza nguvu zote na nyingi kwenye mambo usiyoyataka? Je, mawazo hayo yanakudidimiza chini au yanakuinua juu? ( Soma pia Hizi Ndizo Fikra Zinazokuzuia Wewe Kufikia Viwango Bora Vya Mafanikio )
Nguvu hizi muhimu ambazo tunazo hutiririka kupitia kwenye maneno tunayoyatamka. Tunapaswa kuzingatia ubora wa nguvu hizo zinazoambatana na maneno. Tunapaswa kujiuliza kwamba, je maneno tunayoyatamka yanafungamana na yale tunayoyatamani katika maisha yetu?
Au ni maneno yanayotukumbusha yale tusiyokuwa nayo na yale tusiyoyataka? Je, maneno hayo yanaashiria kutokuwepo kwa matakwa yetu ya ndani kabisa au yanaashiria uwezekano wa ndoto zetu kutimia na kuwa kweli?
Na nguvu hizi pia humiminika kupitia kwenye hisia zetu. Vile vile tunapaswa kuzingatia kwamba, hisia zetu ni nguvu kamili iliyoko kwenye mwendo kasi. Hisia zetu ni ishara kamili inayotutambulisha mtikisiko , uchakavu, na hata kuinuka kwetu.
Unaweza kuitambua nguvu hii kwa kujiuliza je, hisia zangu zinafungamana na kufanana na yale unayoyataka au maisha ambayo unayotarajia kuyaishi? Je, unafanikiwa kuzifikia hisia ambazo zinahamasisha na ambazo zinakufanya ujihisi vizuri na ambazo zinakuongezea furaha?
Au je, unaendelea kuhisi uhitaji fulani ambao umezoea kuhisi katika maisha yako? Je, uko tayari kuchagua njia sahihi zitakazo kufanya ujihisi vizuri? Ni muhimu kukumbuka kuwa, kwa sababu tumezalishwa ndani ya nguvu hizo za ulimwengu, zenye uwezo wa kuumba, basi nasi pia ni waumbaji wa maisha yetu. 
Tunapaswa kuumba au kubuni kila wakati kile tunachotaka kiwe katika maisha yetu  na kuendelea kujibidiisha kwa kufanya hivyo. Tuchunguze na tukadirie ubora wa nguvu hizo tulizonazo na tujipe moyo na uzoefu wa kuendelea kuumba na kubaini kwamba, kwa kadri tunavyoendeleza uumbaji wetu, ndiyo nguvu zenye mtikisiko mkubwa huzalishwa na kuturudia tena.
Hivyo basi, kwa kutambua umuhimu wa thamani ya nguvu tulizonazo na kuzitumia kikamilifu kwa kusudi la kustawisha aina ya maisha tunayoyataka, ni hatua ya mwanzo kabisa itakayotusaidia kuelewa namna ya kuzigeuza nguvu hizo na kuwa maisha halisi ambayo siku zote tumekuwa tukiyafikiria na kuyatamani.
Huna haja ya kuendelea kuteseka  una kila kitu katika maisha yako unachohitaji, hizo ndizo nguvu tatu za kukupa maisha unayoyataka. Nakutakia mafanikio mema na ansante kwa kutembelea mtandao huu wa AMKA MTANZANIA, endelea kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU-0767 048035/ingwangwalu@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: