Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban.

Mark Cuban ni bilionea wa kimarekani ambaye amepata sehemu kubwa ya utajiri wake kupitia mtandao wa intanet. Mark ameanzisha makampuni kadhaa ambayo ameyauza kwa makampuni makubwa ikiwepo kampuni yake ya Micro Solutions aliyoiuza kwa kampuni ya yahoo kwa dola bilion 5.1 mwaka 1999.

CUBAN2

Katika uzoefu wake wa biashara, anawashirikisha wanaopanga kuingia kwenye biashara sheria hizi 12.

1. Usianzishe kampuni kama sio kitu unachokipenda.

2. Kama una mpango wa kuondoka mambo yakiwa magumu hujakipenda unachotaka kufanya.

3. Ajiri watu unaofikiri wanapenda kufanya kazi hiyo.

4. Jua ni jinsi gani kampuni yako itapata hela na jua ni jinsi gani utauza.

5. Jua ubora wako na uboreshe zaidi.

6. Tumia muda mwingi kadiri uwezavyo kwenye kufanya kazi.

7. Usiwe na ofisi, unahitaji kutengeneza timu nzuri. Kama kuna mfanyakazi anataka usiri mfundishe jinsi ya kufunga mlango wa chooni.

8. Kuhusu teknolojia tumia kile unachojua, itakupunguzia gharama.

9. Weka utawala wa ngazi moja, hakuna haja ya kuwa na bosi wa bosi.

10. Huna haja ya kununua swaga, usitumie fedha nyingi kutengeneza tishet za kampuni ukiamini wafanyakazi wako watazivaa nje ya kampuni kuitangaza.

11. Usiajiri kampuni ya mahusiano ya umma(PR), jua vyombo vya habari vinavyohusiana na kampuni yako na wasiliana nao kutoa mchango wako kuhusiana na sekta yako.

12. Fanya kazi iwe furaha kwa wafanyakazi. Punguza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi na wapongeze wanapofanya vizuri.

Print

Hizo ndio sheria 12 kwa wanaoanza biashara kutoka kwa bilionea Mark Cuban. Zitumie ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

Chanzo cha makala hii ni mtandao wa ENTREPRENEUR

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: