Kama Unataka Kuwa Tajiri Katika Maisha Yako, Hakikisha Unaishi Maisha Haya.

Kwa kawaida wengi wetu, tunapenda kufikia viwango fulani vya mafanikio ambavyo tunavitaka katika maisha yetu. Ni maisha ambayo tumekuwa tukiyatamani kila mara, hali ambayo hutufanya tufanye kila linalowezekana ili kufikia maisha hayo tunayoyataka ili yawe upande wetu!
 

Pamoja na kutaka maisha hayo ya mafanikio, wengi wetu tumekuwa tukiishi maisha ambayo hayaendani na kile tunachokitafuta ili kufikia viwango hivyo vya mafanikio. Hilo ndilo kosa kubwa ambalo tumekuwa tukilifanya mara kwa mara, hali ambayo hupelekea juhudi zetu nyingi tunazofanya zinakuwa kama bure.
Ili tuweze kufanikiwa na kutimiza kile tunachohitaji, tunalazimilka kuishi maisha yanayoendana na kile tunachokihitaji katika maisha yetu na si vinginevyo. Kwa kadri unavyoishi maisha yanayoendana na kile unachokihitaji na kusahau maisha ambayo umekuwa ukiyaishi kwa muda mrefu na yamekufikisha hapo ulipo, ndivyo utakavyojikuta unasogea karibu na malengo yako makubwa uliyojiwekea.
Kama una ndoto kweli za kufikia viwango vya juu vya mafanikio na hatimaye kuwa tajiri. Haya ndiyo maisha ambayo unalazimika kuyaishi ili uwe tajiri. Ni lazima ufate na utengeneze mfumo mpya wa kuishi maisha ambayo yatakufikisha kwenye ndoto zako na sio kukwamisha. Kwa leo naomba nikutajie aina ya maisha unayotakiwa uishi wewe ili uwe tajiri.
Haya ndiyo maisha unayotakiwa kuishi ili uwe tajiri:-
1. Ishi maisha ya kufanya kazi kwa bidii.
Ili uweze kufanikiwa na kufikia malengo makubwa uliyojiwekea, unalazimika kuishi maisha ya kufanya kazi kwa bidii kubwa na maarifa, hilo halina ubishi. Watu wenye mafanikio wote ni wachapakazi wazuri. Hakikisha unatenga muda wa kutosha katika kutekeleza majukumu yako uliyojiwekea kila siku. 
Kitu cha msingi ili kufanikiwa kwa hili, jifunze kutenga muda wa kufanyia kazi ndoto zako kila siku. kama utafanyia kazi ndoto zako kila siku hata kama ni kwa kidogo kidogo ni lazima matokeo utayaona, hiyo sio sawa na kukaa tu. Ukiwa na tabia hii ya kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka, safari ya kuelekea kwenye utajiri ni yako. 
 

 

2. Ishi maisha ya kuwa na nidhamu binafsi.
Ni muhimu kuishi maisha ya kuwa na nidhamu binafsi ili uweze kufanikiwa na hatimaye kuwa tajiri. Wengi  kwa bahati mbaya hawana nidhamu binafsi katika maisha yao na ni kitu ambacho kimekuwa kikiwakwamisha na kupelekea ndoto zao nyingi kutotimia. Ni lazima uwe na nidhamu binafsi katika matumizi ya pesa, muda wako, na malengo yako pia.
Unaposhindwa kuwa na nidhamu binafsi utajikuta wewe matumizi yako ya pesa yanakuwa mabovu, unatumia muda vibaya na pengine  unakuwa huna malengo maalum kila kitu unachokiona unakuwa unataka ukifanye tu. Kwa jinsi utakavyomudu kuwa na nidhamu binafsi katika maeneo hayo machache niliyoyataja, utajikuta ndivyo unavyomudu kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Kama katika maisha yako huna nidhamu binafsi, hakikisha unajifunza jinsi ya kumudu kuwa nayo, kama unashindwa kabisa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA, huko utajifunza vizuri tabia hii itakayokuongoza kwenye kilele cha mafanikio unayoyataka uwe nayo katika maisha yako ya kila siku.
3. Ishi maisha ya kuwa na mipango imara.
Kama unataka kuwa tajiri, ni muhimu kuwa na mipango ya kukutoa pale ulipo na kukufikisha sehemu nyingine tofauti na ulipo sasa. Hata kama huna kitu kwa sasa, hilo lisikutishe ni kitendo cha kuamua unataka maisha yako yaweje baada ya miaka mitatu, minne au mitano ijayo. Ukishaamua maisha unayotaka uishi anza kujipanga taratibu hadi ufikie malengo yako.
Inawezekana ukawa hauna mtaji wa kuanzisha biashara unayotaka hilo nalo pia lisikutishe, unaweza kuwa na mipango madhubuti ya kukutoa pale ulipo kwa kuweka akiba hata kidogo, mpaka pesa unayotaka kwa ajili ya mtaji itimie. Kumbuka ukiishi maisha haya ya kuwa na mipango kila siku uwe na uhakika utafanikiwa, anza na kidogo tu ulichonacho mwisho kitakuwa kikubwa.
4. Ishi maisha ya kuwa king’ang’anizi.
Katika maisha changamoto ni moja ya kitu muhimu ambacho hakikwepeki . Unapokutana na changamoto, hakikisha unakabiliana nazo na wala zisikukwamishe wala kukurudisha nyuma na ukaamua kuachana na ndoto zako. Utafika tu katika mafanikio ya juu kama utakuwa ni mtu wa kung’ang’ania ndoto zako. 
Ukishapanga malengo yako, kwenye akili yako weka neno lazima“nitimize ndoto zangu, hata iweje”. Ukisha amua hivyo bila kuacha, mafanikio utayaona. Kama ikitokea umekutana na changamoto nzito jifunze kitu juu ya changamoto hizo na kisha songa mbele. Acha kulaumu na kuachia ndoto zako kirahisi tu, eti kwa sababu ya matatizo. Hakuna tatizo au kitu chochote kinachoweza kukuzuia ndoto zako zaidi yako wewe.
5. Ishi maisha ya kujifunza kwa kujisomea kila siku. 

Ni watu wachache sana wenye tabia ya kujisomea na kujifunza vitu vipya katika maisha yao. Kama huna tabia hii ya kujisomea ambayo ni muhimu kwa maendeleo binafsi sahau kitu kinachoitwa mafanikio makubwa katika maisha yako.
Watu wengi wenye mafanikio makubwa duniani pia ni wasomaji wazuri wa vitabu. Tunaposoma vitabu tunakuwa tunajifunza mambo mengi na kwa muda mfupi sana. Pia inakuwa ni rahisi kutofanya makosa ambayo yamefanywa na wengine kwa kuyarudia. Kama huna tabia hii unaweza kuianza leo angalau kwa kusoma kwa dakika thelathini tu kila siku, baada ya muda utazoea na yatakuwa ndiyo maisha yako.
Kumbuka kujenga utajiri unaotaka inawezekana kabisa ikiwa utafanya kazi kwa bidii, utajitoa mhanga, kuwa king’ang’anizi wa ndoto zako na zaidi kuwa na nidhamu binafsi. Hayo ndiyo maisha unayotakiwa kuishi ili kuwa tajiri.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuelekea kwenye utajiri.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU – 0767048035/ingwangwalu@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: