Kama Kitu Hiki Hakina Mwenyewe, Kitumie Vizuri Kikuletee Mafanikio Makubwa Katika Maisha Yako.

Nimekuwa nikifundisha na kutoa maelezo mengi juu ya mawazo, kwamba ni kitu gani na yako wapi. Watafiti na wanazuoni wengi wametoa maelezo na tafsiri zao mbalimbali juu ya mawazo. Mawazo yapo kwenye maumbile na kwa ujumla hayana mwenyewe. Hapa nina maana kuwa, hakuna mwenye mamlaka ya kumzuia mwingine kuwaza kama unavyowaza wewe au wanavyowaza wengine.
 

Kwa maana hiyo, yeyote Yule au wengine wanaweza kuwaza kitu kimoja kinachofanana kwa kila namna. Kinachotofautiana ni wakati wa kushusha hayo mawazo kwenye akili na kuyafanyia kazi kwenye vitendo. Ni vigumu kueleweka kwa maneno kwa kuwa tunahitaji kufikiri kwa undani zaidi, ili iwe rahisi kwako kuelewa dhana hii.
Hebu tuangaliae mfano huu ambao ulinitokea mimi mwenyewe siku za nyuma kidogo. Kuna wakati nikiwa na rafiki yangu mmoja hivi, tulipata wazo la kuanzisha  biashara ya mchezo wa pool table ambapo kipindi hicho huu mchezo ndio kwanza ulikuwa unaingia nchini. Tuliamua kwenda kuangalia eneo ambalo litatufaa na tulilipata na tuliweza kuwaona viongozi wa serikali ya mtaa kwa ajili hiyo, nao wakaturuhusu.
Wakati tunakagua eneo nilimwambia mwenzangu mawazo yangu kuhusu namna mpango utakavyokuwa, yaani meza itakaa wapi na mengine ya aina hiyo, ikiwemo hata rangi ya mwavuli tutakaotumia kama kivuli itakavyokuwa. Kilichokuwa kimebakia kwetu ilikuwa ni kumwona mwenye duka jirani kwa ajili ya kupata umeme jirani ambao tutakuwa tunatumia nyakati za usiku.

Baada ya wiki ya kutafuta namna ya kuanza zoezi lile, tulishangaa tuliporudi pale kukuta mtu mwingine na yeye kaweka pool table  palepale ambapo mimi nilipawazia na umeme kachukua kwa mwenye duka tuliyekuwa tunamwazia, rangi ya mwavuli aliyoweka ni ile ile niliyoifikiria. Jamani wazo hilihili tulilokuwa nalo kumbe kuna mwingine na yeye kwa kuliona eneo aliloliwazia kama sisi, kama kwamba tulipanga pamoja.
Mfano mwingine unaotutokea kila siku ni huu, unaweza ukawa unawaza kumpigia simu mtu Fulani, wakati ukiwa bado hata hajaanza kupiga, mara unashangaa mtu huyohuyo uliyekuwa unamwazia anakupigia. Mawazo yalikuwa ni kumpigia huyo ndugu sasa amekupigia yeye, hili hutokea kwa wengi na hii inaonyesha kuwa wazo halina mwenyewe yeyote anaweza kuwa nayo na kuyatumia kumfanikisha.
Hebu tujiangalie tutagundua kuwa mifano ya namna kama hii ni mingi sana na tunayo katika maisha yetu ya kila siku. Unaweza kufungua biashara ya chips mahali Fulani, ikipita baada ya wiki moja unakuta mwingine ameshafungua. Unawaza kuanzisha kitu Fulani ambacho wala hakijawahi kuwepo mahali Fulani, kabla hujafanya unakuta kuna mwingine anafanya. Mawazo yapo, yanaelea na kila mtu anaweza kuyadaka, kama atapenda kuyadaka.
Tatizo letu ni kwamba, kuna baadhi yetu ambao tunadhani mawazo ni mali ya mtu mmoja. Kwa hiyo, mtu anawaza kuhusu kitu au jambo Fulani zuri sana. Badala ya kulifanyia kazi, anasema ‘nitafanya’. Hatimaye anakuja kushangazwa na mtu mwingine, ambaye amefanya kama yeye alivyokuwa akifikiria. Mtu anapowaza kuhusu jambo ambalo anaamini linaweza kumsaidia yeye au wengine, anapaswa kulifanyia kazi sawia.
Kwa kusubiri, wazo hilo litapita kichwani kwa mwingine na atalidaka na kuanza kulifanyia kazi. Hii ndiyo nguvu ya mawazo, unaweza kuyatumia kukufanikisha kwa kadiri unavyoweza. Na kama hayana mwenyewe yatumie kukuletea mafanikio makubwa unayoyataka katika maisha yako.( Unaweza ukasoma pia Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia ubongo Wako Kukupatia Utajiri Unaoutaka )
Nakutakia mafanikio mema, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI NGWANGWALU
0713 04 80 35/ingwangwalu@gmail.com


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: