Habari za siku mpendwa msomaji wa AMKA MTANZANIA, naamini unaendelea vizuri hasa kipindi hiko cha msimu wa sikukuu.

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kukutakia kila la kheri katika msimu huu wa sikukuu, mapumziko ya krismasi yameisha hivi karibuni na yaliongozana na mapumziko ya mwisho wa wiki. Wakati huu pia tunasubiri kusherekea kumalizika kwa mwaka 2014 na kuuanza mwaka 2015. Hivyo bado mawazo yetu yamekaa kisikukuu sikukuu.

Naamini pia kuna ambao hawakupata nafasi ya kupata mapumziko haya ya sikukuu kwa sababu moja au nyingine. Kuna ambao ilibidi wawepo kazini au kwenye biashara zao, kuna ambao walikuwa kwenye matatizo mbalimbali kama magonjwa au misiba ya watu wa karibu. Kwa vyovyote vile ni jambo la kushukuru sana kama mpaka sasa unaweza kusoma hapa, kwa sababu sio wote wamepata nafasi uliyopata wewe.

Kwa wiki moja iliyopita nilikuwa likizo na hivyo nilipanga kupata muda wa kutafakari mwaka unaoisha 2014 na pia kujipanga kwa mwaka unaokuja 2015.

Mwaka 2014 umekuwa mwaka wa mafanikio sana kwa AMKA CONSULTANTS, tumeweza kuongeza wigo na kuwafikia watu wengi zaidi na pia kuandika makala ambazo zimekuwa msaada kwa watu wengi zaidi.

Ni mwaka huu ambapo tulianzisha KISIMA CHA MAARIFA, jumuia ambayo imekuwa msaada mkubwa sana kwa kila aliyejiunga nayo. Kuna mambo mengi sana ambayo tumefanikiwa kuyakamilisha kwa mwaka huu 2014, na yote haya yasingewezekana kama isingekuwa wewe msomaji ambaye umekuwa nasi kwa kipindi chote hiki.

Shukrani kubwa kabisa ni kwako wewe msomaji ambae tumekuwa pamoja kw akipindi chote hiki cha mwaka 2014, nimepokea maoni mengi mazuri kutoka kwenye wasomaji ambayo yamekuwa muhimu sana kwenye mafanikio yetu.

Pia wewe msomaji umekuwa balozi mzuri kwa kuwaambia wengine watembelee mtandao huu, asante sana na endelea kufanya hivi kila siku.

Mwaka 2015 utakuwa mwaka bora zaidi kwetu na hata kwako pia msomaji. Mwaka huu 2015 kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili kuweza kuwafikia na kuwasaidia wengi zaidi kufikia malengo yao. Pia tutaendelea kuboresha makala tunazoandika ili ziweze kuwa msaada zaidi kwako msomaji. Pia huduma nyingine za AMKA CONSULTANTS kama MENTORSHIP PROGRAM zitafanya kazi kwa karibu zaidi na wale ambao wapo tayari kubadili maisha yao na kuweza kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Kila penye mafanikio hapakosi changamoto. Mwaka huu 2014 umekuwa na changamoto kubwa kwetu pia. Baadhi ya mipango tuliyokuwa tumeweka kwa ajili ya mwaka huu haikuweza kufanikiwa. Moja ya mipango hiyo ilikuwa kuendesha semina nne za moja kwa moja kwa mwaka 2014.

Changamoto nyingine imekuwa ni kubadili kutoka mfumo wa zamani wa KISIMA CHA MAARIFA ambao ilikuwa mwanachama analipa ada mara moja tu na kuingia kwenye mfumo mpya ambapo mwanachama atalipa ada kila mwaka. Ilikuwa ni changamoto ambayo pia huenda imepoteza wasomaji kiasi, lakini ndivyo mabadiliko yalivyo.

Tumetumia changamoto hizi kama sehemu ya kujifunza ili kuwa bora zaidi na kutorudia makosa ambayo yalipelekea kutokea kwa changamoto hizo.

Jambo moja muhimu la wewe kufanya.

Usiingie mwaka 2015 kwa mazoea, hii itakugharimu sana kama ambavyo imekuwa inakugharimu miaka iliyopita. Tenga muda na kaa peke yako ukitafakari umefanya nini mwaka 2014 na kujua ni kipi utafanya mwaka 2015. Angalia kila eneo la maisha yako, uko wapi kwa sasa na unataka kufika wapi. Angalia kuhusu fedha(kipato), kazi au biashara, familia, afya na hata imani. Haya ni maeneo muhimu sana kwako ili kuweza kuwa na maisha ambayo yamekamilika pande zote.

Baada ya kufanya tathimi hii kwenye maisha yako, jiunge kwenye semina ya siku 21 itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina hii ni kwa ajili ya kukuandaa wewe kwa mwaka 2015, kukuwezesha kuweka malengo makubwa mabayo utaweza kuyafikia, kuongeza ufanisi wako na kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa. Semia hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao na kila msiriki atatumiwa email yenye mafunzo kila siku ya semina. Ili kujiunga na semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253/0755953887 na kisha tuma jina na email yako. Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 31/12/2014 hivyo una siku mbili tu za kupata nafasi hii nzuri ya kuleta mabadiliko kwenye maisha yako mwaka 2015, wahi sasa ili usije kukosa nafasi hii nzuri.

Imani yangu.

Hiki ndicho ninachokiamini mimi na kinachonisukuma kila siku kufanya kile ambacho ninafanya;

Naamini kila mtu ana uwezo mkubwa ndani yake wa kuweza kuwa bora zaidi ya alivyo sasa.

Naamini kuna fursa nyingi sana zinazomzunguka kila mtu pale alipo ambazo zinaweza kumsaidia kuboresha maisha yake zaidi.

Nafanya kazi na watu kuwawezesha kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yao na fursa zinazowazunguka ili kuweza kuboresha maisha yao na kufikia mafanikio makubwa.

Hiki ndio ninachokiamini, hii ndio itakuwa sala yangu kila siku kwa mwaka 2015.

Nataka wale ambao wanahitaji mabadiliko kweli kwenye maisha yao wakaribie kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tufanye kazi pamoja.

Nakutakia kila la kheri katika zoezi utakalokwenda kufanya la kutathmini maisha yako. Pia nakutakia kila la kheri katika siku chache zilizobakia kuumaliza mwaka huu 2015.

Nakusubiri kwa hamu na shauku kubwa kwenye semina ya siku 21 na baadae kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

TUPO PAMOJA.

Usisahau kutoa maoni yako na ushuhuda wako jinsi ambavyo AMKA MTANZANIA imebadili maisha yako. Bonyeza hapa na ujaze fomu, maoni yako ni muhimu sana.

kitabu-kava-tangazo4322