Heri ya mwaka mpya mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, mwaka huu ni mwaka muhimu sana kwako kufanya mabadiliko na AMKA CONSULTANTS iko na wewe ili kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora kila siku.

Kwa wale ambao walipata nafasi ya kujiunga na SEMINA YA SIKU 21 itakayofanyika kwa njia ya mtandao na itakayoanza jumatatu tarehe 05/01/2015, napenda kuwafahamisha kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Ili kuhakikisha umejumuishwa kwenye semina hii tafadhali tembelea email uliyotuma wakati unajiunga. Katika email yako utakuta ujumbe wenye maelekezo kuhusu semina hii. Fungua ujumbe huo na uusome ili tuweze kujua kwamba umeingia kwenye program hii ya mafunzo.

Kama hujapata email hiyo ya mafunzo tuma email kwenda maarifa@kisimachamaarifa.co.tz Tumia email ambayo ungependa itumike kwenye mafunzo haya.

Tafadhali fanya zoezi hili mapema leo ili ujihakikishie kupata mafunzo haya mazuri.

Kuna baadhi ya watu ambao walituma fedha ila hawakutuma email, na wala hawapo kwenye mfumo wa email wa AMKA MTANZANIA naomba pia watu hawa tuwasiliane mapema.

Kwa ambao hawakupata nafasi ya kujiunga tunawakaribisha tena mwaka kesho wakati kama huu ambapo tutaendesha mafunzo mengine. Kwa sasa mnaweza kuendelea kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA, MAKIRITA AMANI na pia kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ambapo kutakuwa na mambo mazuri sana mwaka huu 2015.

Nawatakia wote kila la kheri,

TUPO PAMOJA.