Vitu 10 Unavyotakiwa Kujua, ili Mwaka 2015 Usiwe Wa Majuto Kwako.

Habari za leo, mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA. Ni matumaini yangu ya kuwa umzima na unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako ya kila siku. Karibu sana katika safu hii ambapo leo tutaangalia vitu kumi unavyotakiwa kujua, ili mwaka 2015 usiwe wa majuto kwako.  Ni ukweli usiofichika wengi wetu tunapoanza mwaka huwa tunakuwa tumejiwekea mipango na malengo makubwa ambayo huwa tuna nguvu nayo sana kuyatekeleza. Lakini kwa bahati mbaya kadri siku zinavyozidi kwenda hujikuta ni watu wa kujisahau kwa kile tulichokuwa tumepanga mwanzo wa mwaka.

Hali hii inapotokea hujikuta tumemaliza mwaka na kushindwa kutimiza kile tulichokuwa tumepaga mwanzo. Kutokana na hili kumia na kujuta kwingi huanza kujitokeza ndani ya mioyo na  nafsi zetu. Ni kitu ambacho kimekuwa kikijitokeza mara kwa mara katika  maisha yetu ya kila siku kwa wengi na kimekuwa kikitokana na wengi kutokujua au kusahau baadhi ya vitu muhimu. Je, unajua ni vitu gani unavyotakiwa kujua ili mwaka 2015 usiwe wa majuto kwako? 

Ni muhimu kuwa kiongozi na mwamuzi wa maisha yako. Hiki ndicho kitu muhimu unachotakiwa kukijua na kukizingatia, ili maisha yako yasiwe ya majuto ifikapo disemba 31. Unapokuwa kiongozi wa maisha yako itakusaidia kuwajibika zaidi kuliko ambavyo ungetegemea watu wengine waongoze maisha yako. Acha tena tabia ya kutegemea mtu, serikali au kampuni yako ndiyo ikuamulie na kukuongoza katika maisha yako. Huu ni wakati wa kusimamia kwa miguu yako miwili na kuzifuata fursa ambazo zinakuzunguka.  Unapokuwa kiongozi wa maisha yako hii inakuwa nguzo kuu ya kukufikisha kwenye maisha ya mafanikio unayotaka.

 

2. Acha kujifunza tu, chukua hatua zaidi.

Ili kufikia malengo yako makubwa uliyojiwekea ni muhimu sana kwako kujifunza kila siku lakini usiishie hapo tu unatakiwa kuchukua hatua pia juu ya kile unachojifunza. Kama utakuwa unasoma tu halafu huchukui hatua ya kubadilika na kufanyia kazi vile ulivyojifunza ni ukweli usiojificha utaishia kuwa na maisha yaleyale kuwa magumu. Kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka huu JUST DO IT, jifunze kisha, fanyia kazi malengo yako acha kusubiri kitu. Ukiweza kufanya hivyo mwaka huu 2015 hautakuwa wa majuto kwako na kujilaumu kwingi kama ambavyo umekuwa ukilaumu mara kwa mara. Kumbuka, kuchukua hatua zaidi ya kujifunza na kufanyia kazi kile unachojifunza ni muhimu sana kwako.

3. Weka mkazo katika malengo yako makuu uliyojiwekea.

Ninajua yapo malengo mengi ambayo umejiwekea mwaka huu. Katika malengo hayo uliyojiwekea chagua yale ambayo ni yamuhimu kwanza ambayo umeyapa kipaumbele ndiyo uyatekeleze na kuyatilia mkazo kila siku zaidi. Sio kila lengo ulilojiwekea litakuwa la kipaumbele kwako hapana. Weka mkazo mkubwa kwenye yale malengo unayotaka kuyatimiza kwanza hii itakusaidia kuyafanikisha kwa urahisi. Kama wewe unataka  kuyatimiza malengo yako yote kwa pamoja, utajikuta kuna nguvu ya uzingativu itapungua hivyo utashindwa kufikia malengo yako kwa asilimia mia moja.

4. Kuwa wewe kama wewe.

Acha kutaka kumridhisha kila mtu kama ambavyo umekuwa ukifanya mara kwa mara. Elewa tu kuna watu ambao hawawezi kukubaliana na wewe kwa kile unachokifanya iwe kizuri au kibaya watu hawa wapo tu. Unapokutana na watu hawa acha kukata tamaa na ukajiona mnyonge. Ng’ang’ania kwa vile unavyofanya na hakikisha kuona ndoto zako zinatimia. Usifanye mambo yako kwa kujaribu kuridhisha wengine kuwa wewe ama wewe hii itakusaidia hautaweza kujuta katika maisha yako.

5. Jitoe mhanga kukamilisha ndoto zako.

Fanya kila linalowezekana kuhakikisha ndoto zinatimia. Usije ukakwamishwa kwa lolote na mwisho ukajikuta ndoto zako zimeyeyuka. Ukijitoa  mhanga kwenye ndoto zako hata ikitokea mambo kwako yamekwenda hovyo hutajilaumu kama ambavyo ungetulia.

6. Kubali kuna kukosea katika  maisha.

Kuna wakati  katika maisha huwa inatokea kuna makosa ambayo huwa tunayafanya bila kujijua sisi wenyewe katika maisha yetu. Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara unapokesea jifunze na kusamehe pia, kisha chukua hatua za kujifunza na kusonga mbele. Ukiamua kukubali kukosea kupo utajikuta unaishi maisha yako kwa amani bila kuwa na majuto ya aina yeyote ile.

7. Fanya vitu unavyovipenda.

Unapofanya vitu vile unavyovipenda hata inapofika ule wakati kuwa hujisikii ama huna hamasa ya kufanya jambo hilo huwa kwako ni rahisi kuendelea kufanya kuliko ambavyo ungefanya jambo ambalo hulipendi. Hili limekuwa likiongelewa na wataalamu wengi wa mafanikio kuwa ni muhimu kufanya jambo ambalo unalipenda kweli kutoka moyoni mwako ili uweze kupata mafanikio ya kweli ambatyo unayahitaji. Vinginevyo, ukiendelea kufanya mambo ambayo huyapendi utaendelea kujuta kila mara katika maisha yako na utakuwa huna wa kumlaumu.

8. Tumia muda wako vizuri na watu sahihi.

Ni jambo muhimu ambalo unalotakiwa kulizingatia kwa mwaka huu ili uweze kutengeneza mafanikio unayoyata. Acha kupoteza muda wako kuwa na watu ambao hawana msaada juu ya maisha yako. Ni wakati wa kuishi maisha ya kuwa na watu sahihi ambao hata wao wanapenda kuona mambo yako yanafanikiwa. Unapotumia muda wako vizuri na watu sahihi hii itakusaidia kusonga mbele zaidi kwa kile unachofanya katika maisha yako.

9. Ishi maisha yako sasa.

Wapo watu ambao katika maisha yao mara nyingi huwa ni watu wa kesho, kesho  kesho. Unataka kufanikiwa anza kuishi sasa. Kama kuna jambo ambalo ulitakiwa ulitimize au kuanza kulifanya anza kulifanya moja kwa kwa moja. Hakuna kesho katika maisha yako, kama unasubiri kesho kila siku itakuwa ni kesho na mwisho utajikuta hujatimiza kitu chochote katika maisha yako. Ishi maisha yako sasa kwa kufanya kila linalowezekaa kufanikiwa, hapo hautajuta wala kulaumu.

10. Kuwa mtu wa shukrani kwa kile unachopata.

Kila mtu kwa sehemu yake katika maisha huwa kuna vile vitu anavyotimiza hata kama ni kidogo. Unapofanikisha lengo Fulani hata kama ni dogo ni vyema ukajifunza kuwa mtu wa shukrani. Unaposhukuru hiyo inasaidia kufungua milango mipya zaidi. Inabidi ujifunze  kukubali kwa sehemu umepokea na upo tayari kupokea tena na tena, hii ni kanuni ya kimaumbile ambayo wewe kama wewe huwezi kuipinga. Ukifanya jambo hili utajikuta unamalaza mwaka ukiwa huru bila majuto.

Nakutakia mafanikio mema, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kupata maarifa bora zaidi.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO  kwa kujifunza na kuhamasika.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: