Kuwa na malengo na hatimaye kuweza kutimiza malengo hayo uliyojiwekea huwa ni vitu viwili tofauti. Wengi wetu huwa ni watu wa kujiwekea sana malengo katika maisha yetu, lakini kwa bahati mbaya malengo mengi huwa hayafikiwi kama ambavyo ilikuwa imetarajiwa.

Unaweza ukathibitisha hili kwa kuangalia maisha yako mwenyewe binafsi, ni mara ngapi umekuwa ukisema kuwa mwaka huu nitafanya hiki na kili na kile. Lakini inapofika mwisho wa mwaka unashangaa yale malengo yote mazuri uliyokuwa umejiwekea unakuwa hujayatimiza kwa sehemu kubwa. Na kuna wakati umekuwa ukijiuliza nini tatizo ama sababu inayopelekea ushindwe kufikia ndoto zako?

Katika makala hii tutakwenda kujadili mambo yanayokukwamisha na hadi kujikuta kushindwa kufkia malengo yako muhimu uliyojiwekea. Mambo haya yamekuwa sumu kwako na kimekuwa kikwazo kinachokufanya ushindwe kufikia ndoto zako na uendelee kuishi maisha yale yale siku zote, kitu ambacho ni hatari sana kwako kwa maendeleo yako.

Yafuatayo  Ndiyo Mambo 8 Yanayokufanya Ushindwe Kutimiza Ndoto Zako.

1. Kuahirisha mambo.
Hiki ndicho moja ya kitu kikubwa ambacho kimekuwa kikiua ndoto na malengo  ya watu wengi bila kujijua. Hii huwa inatokea kwa sababu jinsi ambavyo unavyozidi kuahirisha mambo yako, kwa kawaida kile kitu huwa kinaanza kukosa hamasa na mvuto polepole, mwisho wa siku hujikuta unaacha kabisa. Kama unataka kutimiza malengo yako na kuweza kufika kwenye kilele cha mafanikio, kitu muhimu ambacho unatakiwa uachane nacho na kukisahau kabisa ni tabia ya kuahirisha mambo yako mara kwa mara.

SOMA; Jinsi ya kuondoa tabia ya kuahirisha mambo.

 

2. Kuwa na hali ya uvivu. 
Kuna watu ambao katika maisha yao hawezi kufanya kitu mpaka wasimamiwe. Watu hawa kama hawajisamiwa kiuhalisia mambo huwa hayaendi sawia na utakuta vitu vingi vinaharibika,  ndiyo maana ni hatari sana kuwa mjasiriamali kama kama maisha yako kwa sehmu kubwa unahitaji kusimamiwa. Kutokana na hali hii mara nyingi ndiyo huwa inaua ndoto za watu wengi sana katika maisha ya kila siku. Malengo ama ndoto nyingi huweza kufa kwa sababu hakuna kinachoweza kufanyika katika maisha ya mtu kama wewe umetawaliwa na uvivu kila wakati na kusubiriwa usimamiwe.

SOMA; Kama unasumbuliwa na uvivu hii hapa ndio dawa yake.

3. Kukata  tamaa mapema.

Wengi huwa ni watu wa kuua ndoto zao wenyewe kutokana na  kukata tamaa mapema kwa kile wanachokifanya. Kuna wakati bila kujua unaweza ukaamua kukata tamaa, lakini kumbe jibu ama mafanikio uliyokuwa ukiyatafuta  ulikuwa ndio unakaribia kuyafikia kabisa. Jifunze kung’ang’ania ndoto zako hata pale unapokutana na magumu vumilia na komaa, lakini unaposhindwa kufanya hivyo inakuwa ni rahisi sana kwako kukata tamaa na mwisho wa siku unajikuta huwezi kufanikiwa tena.

4. Kuwa na visingizio.
Kuna visingizio vingi sana ambavyo watu wengi huwa wanajiambia kila siku kama sababu ya kutokufanikiwa kwao. Hata ungekuwa una sababu nyingi na nzuri vipi haziwezi kukusadia hata kidogo zaidi ya kuua ndoto zako. Ulimwengu ambao upo haujui wala hautambui sababu zako, unachohitaji kwako ni wewe kuwa mtu wa mafanikio. Jiulize utaendelea kuwa na visingizio mpaka lini? Kama utaendelea kuwa mtu wa visingizio katika maisha yako, elewa kabisa utaua ndoto zako nzuri ulizonazo.

5. Kuwa na mawazo hasi sana. 
Tabia ambayo naweza kukupa uhakika  wa asilimia mia moja inayoua ndoto na malengo yako kwa sehemu kubwa ni wewe kuwa na mawazo hasi. Kama umejawa na mawazo hasi na kufikiria chanya kwako ni kama bahati mbaya nakuhakikishia unaua na kufuta ndoto zako kaisa na pia sahau kuhusu mafanikio katika maisha yako. unapokuwa mtu wa mawazo his unakuwa ni mtu wakijicho, tamaa, wivu na ambaye kuna wakti unakuwa hutaki kuona wengine wanafanikiwa. Kutokana na hali unakuwa wewe ni mtu wa kuumia na huwezi kufanya jambo la kukusaidia wewe na mwisho wa siku utajikuta unaua ndoto zako.

SOMA; Kama na wewe una mawazo haya sahau kuhusu mafanikio.

6. Kuwa na matumizi mabaya ya pesa. 
Malengo yoyote unayojiwekea kwa kawaida huwa yanaendana na pesa. Pesa hapo inakuwa inatumika kama chombo muhimu cha kutusaidia kuweza kufikiaa malengo tuliyojiwekea. Sasa kama utakuwa unatumia pesa zako hovyo ambazo zingeweza kukusaidia katika suala zima la kutimiza malengo yako, itakuwa ni sawa na wewe mwenyewe kuamua kuua ndoto zako ulizojiwekea. Ndoto zakozitakuwa zinakufa kwa sababu kitu ambacho kingekusaidia kutimizahizo ndoto zako unakuwa umekipoteza, hivyo kujikuta hauwezi kufanya kitu  na ndoto zako zinaanza kufifia na mwisho kuzipoteza.

SOMA; Jinsi ya kutunza fedha ya akiba kama una matumizi mabaya ya fedha.

7. Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. 

Kama wewe ni mlevi wa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, linken na mingineyo kuanzia sasa elewa kabisa unaua ndoto zako. Ninaposema mlevi, namaanisha ukiingia kwenye mitandao hiyo unakuwa unapoteza muda sana na wala hutaki kubanduka. Kumbuka kuwa unavyozidi kutumia muda mwingi huko, ndivyo unavyozidi kupoteza muda mwingi ambao hata ungeweza kuutumia kujifunza vitu vya manufaa kwako kama kujisomea. Acha kuua ndoto zako kwa sababu ya facebook au twitter, sio nakwambia usitumie hapana, tumia ila kwa kiasi.

SOMA; Tumia mitandao ya kijamii kwa umakini, inaweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Malengo na mipango yako uliyojiwekea haitaweza kutumia kama utaendelea kushikilia mambo hayo yanayoweza kuua ama kuzuia ndoto zakozisiweze kutumia. Chukua hatua muhimu juu ya maisha yako, achana na mambo hayo yanayozuia ili ndoto zako zisitimie.

Nakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA  kila siku, kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

 IMANI NGWANGWALU,