Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Saa Hili moja Kufikia Mafanikio Makubwa.

Bila ubishi, bila shaka yoyote unao uwezo mkubwa wa kufanikiwa na kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako kama utaamua kutumia vizuri saa hili moja kwa siku. Mabadiliko yoyote unayotaka katika maisha yako unaweza kuyafanya yatokee,  kama kila siku utakuwa una nidhamu binafsi itakayokuongoza kulitumia saa hili vizuri.
 

Saa hili moja ninalolizungumzia ni saa lako la kwanza kabisa kila unapoanza siku yako mpya, ndilo unalotakiwa ulitenge ili liweze kukuletea mafanikio makubwa. Nikiwa na maana pia kila unapoamka saa moja la kwanza ndilo linatakiwa liwe la kwako ulitenge kwa ajili ya ukuaji wako binafsi (Personal development growth) na kutafakari maisha yako kwa ujumla.
Kwa kawaida hili huwa ni saa ambalo linaweza kukupa na kukuletea mabadiliko makubwa katika maisha yako kwa sababu akili yako inakuwa imetulia, inakuwa inanguvu na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu tofauti na muda mwingine ambapo inaweza ikawa imechoka na kushindwa kutafakari mambo ya msingi. 
Watu wengi wenye mafanikio huwa ni watu ambao wanalitumia saa hili la kwanza vizuri na kujikuta wanaleta mabadiliko na mafanikio makubwa katika maisha yao siku hadi siku. Ni mabadiliko hayohayo ambayo hata wewe unaweza kuyafanya kama ukiamua leo. Unawezaje kulitumia saa hili moja la kwanza katika siku yako na kuweza kukupa mafanikio makubwa katika maisha yako?
Hivi ndivyo unavyoweza kutumia saa hili moja kufikia mafanikio makubwa. 
1. Kupanga na kuipangilia siku yako.
Watu wengi wenye mafanikio makubwa huwa wanalitumia saa hili moja kwa kutenga dakika chache kwa ajili ya kupanga na kupangilia kwa ujumla namna siku nzima itakavyokwenda. Huwa ni utaratibu ambao unaweletea matunda kwa sababu kila kitu kwa siku kinakuwa kinaenda kwa utaratibu maalum kama kilivyopangiliwa.
Mara nyingi unapokuwa unapanga na kuipangilia siku yako hiyo inakuwa inakusaidia sana kuweza kujua ni kitu kipi utaanza kukifanya na utamaliza na kitu gani kwa siku hiyo husika. Lakini, sio hivyo pia inakusaidia wewe kutumia muda wako vizuri kuliko ungeendesha mambo yako kiholela. Hivyo, ni muhimu sana kupanga na kuipangilia siku ili mambo yako yaende vizuri.
 
  
2.  Kuchukua jukumu zima la kujisomea.
Saa lako la kwanza ni muhimu sana kwako wewe ukalitumia kwa kujisomea ili kuweza kuongeza maarifa bora yatakayoweza kukusadia wewe kuweza kukabiliana na changamoto nyingi unaweza ukakutana nazo katika maisha yako ya kila siku. Unapokuwa unajisomea unakuwa unaongeza ujuzi na maarifa ambayo yatakusaidia kwa kile unachofanya.
Kwa kila siku jifunze kutenga muda kidogo ambao utaweza kuutumia kwa ajili ya kujisomea hata kama ni dakika thelathini tu zinatosha. Acha uvivu au kuwa miongoni mwa watanzania kwao kujisomea ni tatizo. Jenga hulka bora ya kujisomea itakayokuwezesha wewe kuvumbua maarifa bora kabisa yatakayokusaidia kufikia ndoto zao.
3. Kuendeleza vipaji vyako.
Unaweza ukatumia muda huu kuendeleza vipaji vyako binafsi ulivyonavyo. Watu wengi huwa wana vipaji vizuri ndani yao lakini tatizo kubwa huwa linakuja ni kushindwa kuendeleza vipaji hivyo walivyonavyo. Huu huwa ni muda mzuri wa kuendeleza vipaji vyako ulivyonavyo kama kweli utaamua kuutumia vizuri.
Kama unakipaji cha kuandika unaweza ukatenga muda huu wa kuandika hata maneno machache kwa siku na mwisho wa siku utajikuta unaweza kumudu kuandika maneno mengi zaidi. Chochote ulichonacho unaweza kukiendeleza kwa muda huu. Acha kufa na kuzikwa na vipaji vyako. Tumia muda huu kugundua vipaji ulivyonavyo na kuvitumia ili kukupa mafanikio makubwa katika maisha yako.
4. Kufanya tahajudi (Meditation)
Pia hili huwa ni saa muhimu sana kwako kwa ajili ya kutenga muda mchache kwa ajili ya kufanya tahajudi. Hiki huwa ni kipindi kizuri kwa ajili ya utulivu wake na inakuwa rahisi kwako kuweza kujisikiliza na kuvuta nguvu za ziada ambazo zinaweza kukusaidia kukuwezesha hata kupata kile unachokihitaji katika maisha yako.
Meditation ama tahajudi inakuwa ni muhimu kwako kwa sababu inakuwa inakujengea utulivu wa akili na kukufanya uweze kutafakari vitu vingi kwa mtazamo tofauti, kinyume na pengine usingeweza kufanya tahajudi kabisa. Jijengee na ujizoeze utaratibu huu ambapo wakati wa ‘kumeditate’ unakuwa unafunga ama kujizuia kuifikirisha akili yako kwa chochote kile.
5. Kufanya mazoezi.
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayoyahitaji ni muhimu kwako kuwa na afya bora. Utayafikia tu mafanikio hayo kama utakuwa kila siku mtu wa kutenga muda mchache, utakaokuwezesha kufanya mazoezi kidogo ambayo yataweza kukuweka vizuri na kukutengenezea afya bora, ambayo itakuwa ni muhimu kwa manufaa yako.
Si lazima ufanye mazoezi haya nje ama kwenye uwanja, hapana. Unaweza ukayafanyia hata chumbani kwako au kwenye sehemu ndogo iliyo nyumbani kwako yenye nafasi. Na mazoezi haya utayafanya kwa dakika chache tu kama tano au kumi ili kuweza kuamsha akili yako ilio kuweza kufanya mambo kwa utendaji wa hali ya juu zaidi.
Unaweza ukaleta na kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako, kama utaamua kulitumia saa hili vizuri kila siku katika maisha kwa kujitoa kila siku bila kuacha. Jifunze zaidi kutakari juu ya maisha yako ndani ya saa hili na jiulize mara kwa mara unalitumiaje saa hili ili liweze kukufanikisha zaidi katika maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
NAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.

 IMANI NGWANGWALU,

         

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: