Wajasiriamali wengi wamejikuta wakitafuta pesa kiasi cha kusahau afya zao. Kumbuka kwamba afya yako ni utajiri. Jee unapenda kuwa na afya njema? fanya yafuatayo;

Kunywa maji.

Watu wengi hawanywi maji hasa sehemu za baridi. Maji ni muhimu katika mwili wa binadamu asilimia 75% ya mwili wa binadamu ni maji. Maji husaidia kusaga chakula, hufanya mwili wako kuwa laini na husaidia kuweza kupata haja kubwa vizuri. Pia maji husafisha sumu mwilini. Kunywa maji angalau lita moja kwa siku.

Kula chakula bora (mlo kamili).

Chakula unachokula ni chanzo cha wewe kuwa na afya njema au mbaya. Kuna vyakula vibaya na vizuri. Vyakula vizuri ni matunda mboga za majani. Mboga za majani na matunda huwa zinasafisha tumbo kwa kuwa zina nyuzi nyuzi.  Pia unashauriwa vyakula asilia kama vile viazi vitamu mihogo navyo vina nyuzi nyuzi za kusafisha tumbo. Vyakula vingine vizuri ni Protini inayotokana na mimea mfano maharage kunde soya. Tumia nyama nyeupe mfano kuku na samaki aina hii ya nyama ni nzuri kwa afya yako ya moyo. Vyakula vibaya ni nyama nyekundu. Vyakula vinavyokaangwa kwa mafuta ikiwa ni pamoja na chipsi mayai hivi hufanya mwili kuongeza uzito na baadaye kuleta matatizo ya moyo. Kama unakula vyakula kama hivi vipikwe kama mchemsho au vibanikwe.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

 

Mazoezi.

Jee huwa unafanya mazoezi? Mazoezi ni mazuri kwa afya yako yanakufanya unatoka jasho na kuunguza mafuta ya ziada mwilini. Mazoezi huwa yanasaidia kujenga misuli na kukuongezea nguvu mwilini. Penda kutembea kwa miguu kama unakwenda umbali mfupi, unapopanda ghorofa jitahidi utumie ngazi badala ya lift. Unapokuwa nyumbani pendelea kufanya kazi za mikono kama vile kupanga vitu nk.

Fikiri vizuri

Jee unafikiri vizuri? Kama hujaanza kufikiri anza sasa kwa kujitambua, jifunze namna ya kufikiri vizuri itakuondolea hali ya kuwa na mtazamo chanya. Kama hujui mahali pa kuanzia unaweza kumtafuta mwandishi wa makala hii atakufundisha jinsi ya kufikiri vizuri. Mafanikio yako yatatokana na mtazamo wako na jinsi unavyofikiri. Unaweza kutafuta vitabu vinavyofundisha kufikiri vizuri; Kitabu cha Kiswahili –Maisha na mafanikio mtunzi Munga Tehnani. Vitabu vya kiingereza The power of positive thinking mtunzi Norman Vicent Pearl. Mtunzi wa makala haya yuko mbioni kuanzisha mafunzo ya utambuzi kupitia mtandao wa internet bila malipo uharaka wa swala hili utatokana na maombi yenu.

SOMA; Haya Ndio Matumizi Mazuri Ya Mshahara Wako Ambayo Yatakuletea Furaha Na Mafanikio.

Jee unamwamini Mungu?

Jee unamwamini Mungu ? Kama humwamini Mungu siwezi kukulazimisha ila nakushauri uanze tena kusali. Sala zinasaidia kuwa na mtazamo chanya katika maisha na pale mambo yanapokuwa magumu unaweza kumkabidhi Mungu kwa sala na maombi zinasaidia.

Vuta hewa safi kwa wingi

Hewa ya oksijeni ni muhimu katika mwili wa binadamu ukikosa hewa hii unaweza kufa. Kama unahitaji kuvuta hewa fanya mambo yafuatayo; Fanya mazoezi, lala katika nyumba yenye madirisha makubwa ambayo yanapitisha hewa safi. Unajua kwa nini watu wengine wakiamka asubuhi wanakuwa wamechoka sana ni kwa sababu wanalala kwenye nyumba ambazo zina madirisha madogo yanayopitisha hewa kidogo.

SOMA; UKURASA WA 83; Unahitaji Kuwa Sahihi Au Kuwa Na Furaha?

Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;http://tinyurl.com/mshauriwabiashara au Piga simu namba 0784394701

Semina ya ujasiriamali bila malipo tarehe 28/3/2015
Kampuni ya CPM Business Consultants, inayojishughulisha na kutoa mafunzo ya ujasiriamali na ushauri wa biashara, itatoa semina ya ujasiriamali kwa watu wote bila malipo yoyote siku ya Jumamosi tarehe 28/3/2015 saa 5.00 asubuhi katika ukumbi wa Hawaii Kimara Baruti. Katika semina hiyo tutatoa fursa kwa washiriki kununua vitabu vya ujasiriamali ambavyo gharama yake ni sh. 6,000 kwa wale watakaohitaji.
Mada zitakazotolewa ni;
– Namna ya kuanzisha biashara
– Namna ya kufanya utafiti wa soko na kutangaza biashara yako.
– Jinsi ya kutunza kumbu kumbu za hesabu za biashara yako.
– Fursa za biashara kulingana na mazingira yako.
– Maswali na majibu.
Kwa maelezo zaidi au kuthibitisha ushiriki kwenye semina, piga simu namba
0784394701. Tafadhali mwambie na mwenzako, sambaza ujumbe huu kadiri inavyowezekana.

mabadiliko cover EDWEB