Kama Unajiambia Hivi Mara Kwa Mara, Unaharibu sana maisha Yako.

Mara nyingi katika maisha yetu kama tuna kawaida ya kujiambia maneno au kauli za aina fulani, ni lazima tutajihisi kwa namna ile tunavyojiambia sisi mwenyewe. Kumbuka kujiambia huku huwa tunafanya kati yetu binafsi kila siku na kila wakati vichwani mwetu ambapo mazungumzo huwa yanaendelea huko, ambayo mara nyingi ni siri zetu.
 

Kama ikatokea tuna kawaida ya kujiambia maneno au kauli za aina fulani, ni lazima tutajihisi kwa namna tunavyojiambia. Hivyo, wakati mwingine kujiamini au kutokujiamini kwetu ni matokeo ya yale yanayoenda vichwani mwetu, yaani tunajiambia nini kuhusu sisi wenyewe. Kwa kujiambia kwa namna fulani, hisia, hali na mazingira yetu yatakuwa hivyohivyo.
Naomba nikufundishe jambo moja ambalo ni muhimu sana kwako kulijua. Kama kweli unataka kujiamini, ni lazima uanze kujichunguza namna au jinsi unavojiambia wewe mwenyewe. Kujichunguza huku maana yake ni kutambua, kufahamu na kujua kwamba, huwa kuna mazungumzo ambayo unayaendesha kichwani mwako kuhusu wewe mwenyewe.
Kumbuka kwamba, kile ambacho huwa tunajiambia, yaani yale mazungumzo tunayoyafanya vichwani mwetu, ambapo mara nyingi ni kujilaumu, kujishusha, kujikatisha tamaa na mengine ya aina hiyo, yanakuwa yana nguvu sana kwetu. Kwa nini? Ni kwa sababu, tunapojiambia mambo hayo inakuwa sawa kabisa na tunavyowaambia watu wengine.
Kasi ya kuzungumza, lafudhi na hata sauti tunayoitengeneza huko kichwani, havina tofauti sana na wakati tunapokuwa tunamwambia mtu mwingine kwa sauti tu ya kawaida ya mdomo. Ndiyo maana yanakuwa yana nguvu ya kutuathiri. Inakuwa ni kama kweli kabisa, ingawa ni ukweli kwamba hayo yote tunakuwa tumeyazungumzia vichwani mwetu.
Hivyo, tunapojiambia huko kichwani, ‘mimi ni bwege tu siwezi kufanikiwa’ au ‘mtu mbaya kama mimi nani atanipenda!’ ama ‘nitakufa maskini tu, si nimetoka familia maskini hata hivyo’, ni wazi hayo yatakufanya ujitoe thamani na kutokujiamini. Yanakuwa ni maneno ya kukuumiza wewe ni sawa kabisa na kama vile unaambiwa na watu wengine.
Mbaya zaidi pia ni kwa sababu ni sisi wenyewe, tunaojiambia mara nyingi tena na tena na athari zinakuwa kubwa zaidi kwetu kutokana na msisitizo tunaouweka bila hata kujua. Kama nilivyosema awali, unapaswa kujua kwamba unafikiri. Ukishajua, itakuwa rahisi sana kwako kujiuliza kama yale unayojiambia kuhusu wewe mwenyewe ndiyo unayotaka au hapana.
Kama siyo unayotaka, kwa kadri unavyojiambia ndiyo utakavyokuwa unazidi kupata hisia usizozitaka. Kama ukianza kutambua kwamba huwa unafikiri, itakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kubaini kuwa, huwa unajiambia nini juu yako mwenyewe ambacho kinaweza kukusaidia au kukuumiza na kuharibu maisha yako kabisa.
Kama unataka kujiondoa na janga la kujitia katika kutokujiamini, inabidi uchukue kalamu na karatasi, ujaribu kuandika kile usichokipenda ambacho huwa unajiambia kuhusu wewe, mara kwa mara au kile unachojiambia katika mazingira fulani. Kwa kujua kile unachojiambiwa mara kwa mara ambacho hukipendi, itakusaidia kuwa makini nacho na pengine kukiepuka kabisa katika fikra zako. 
Kwa mfano, huwa inatokea ukajiambia, ‘achia hapo usije ukaadhirika wewe’, au labda ‘usifanye tena si umeona ulivyoshindwa safari ile ‘, ama ‘ni kawaida yangu kukosea nimezoea’ ama ‘siwezi kumudu kwa sababu ni bwege basi’.
Kumbuka kwamba, maneno hayo ni mabaya na kamwe hayawezi kukusaidia kujiamini na kupata unachokihitaji. Ni maneno yenye nguvu sana ya kuweza kuingiza hisia usizozitaka ndani kabisa ya mfumo wako wa kufikiri. Kumbuka, siyo wakati huu, bali hata wakati mwingine, ukikutana na mazingira yanayokufanya ujiambie hivyo, utajihisi hovyo hivyohivyo.
Kwa kuyaandika na kuyaelewa na kuelewa ni wakati gani na kwenye mazingira gani huwa unajiambia maneno hayo, inaweza kuwa rahisi kwako kuanza polepole kudhibiti mazungumzo hayo hayaendayo kichwani mwako. Ukifanya hivyo, polepole, utaanza kujiamini. 
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza zaidi.
TUNAKITAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: