Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Ten Roads To Riches(Njia Kumi Za Kuelekea Kwenye Utajiri).

Habari msomaji wetu wa makala hizi za mambo 20 kutoka kwenye kitabu. Leo hii tutajifunza kwenye kitabu kinaitwa the ten roads to riches ambacho kimeandikwa na tajiri ken fisher. Kitabu hiki kinazungumzia njia 10 za kuelekea kwenye utajiri. Mwandishi anasema kwamba watu wengi wanatamani kuwa matajiri ila wachache ndiyo wanafahamu njia sahihi za kuelekea huko, na baadhi wanafahamu njia moja, ambayo pia ameichambua, na anaiita njia inayotumiwa na wengi. Njia hii ni ile ya kubana matumizi na kuweka akiba, kisha kuwekeza. Ila mwandishi amechambua njia nyingine 9 ambazo wengi hawazifahamu. Japo pia anatoa tahadhari, sio kila njia itakua nzuri kwako. 

 
Karibu sana tujifunze baadhi ya vitu vichache kutoka kwenye kitabu
1. Wajasiriamali wanaibadilisha dunia au wanaleta mabadiliko kwenye dunia kwa njia mbili: wanatengeneza huduma au bidhaa mpya kabisa ambazo hazikuwepo awali, ama wanaboresha bidhaa au huduma ambayo ipo, wanaifanya kua nzuri zaidi na kuongeza ufanisi wake. Kama huwezi kutengeneza kitu kipya kabisa, basi waweza kuboresha kilichopo na ukafanikiwa vizuri sana tu. Wapo wajasiriamali wakubwa katika dunia hii ambao walichofanya ni kuboresha bidhaa, au huduma iliyokuwepo.
2. Kama wewe ni mwajiri, kamwe usimpandishe cheo mfanyakazi ambaye hajawahi kufanya kosa, yaani hajawahi kukosea, maana utakua unampandisha cheo mtu ambaye hajafanya vitu vingi. Kukosea ni ishara ya kujaribu vitu vingi, na pia kukosea ni njia ya kujifunza, kama mtu hajawahi kukosea ina maana anajua vichache na hana uwezo wa kuhimili mambo magumu.
3. Mafanikio hua yanavutia washambuliaji (attackers). Baada ya juhudi nyingi za kufanikiwa, unapofanikiwa, wapo watu watakao kushambulia, aidha kwa maneno, au hata kwa kukudanganya ili wanufaike na mafanikio yako. Watu wa namna hii wanakua na wivu au chuki na wewe bila hata sababu za msingi. Wakati mwingine wanaweza hata kusuka mikakati ya kukuporomosha hapo ulipo, na ni lazima uwe shupavu vya kutosha kuhakikisha hawakuzidi akili. You must be tough
4. Kuna aina mbili za biashara au kampuni unazoweza kuanzisha. Unaweza kuanzisha kampuni kwa ajili ya kuja kuiuza baadaye, au unaweza kuanzisha kampuni ya kudumu ambayo utaimiliki maisha yako yote na hata kuirithisha watoto. Ukiwa na maono ya kuanzisha kwa ajili ya kuuza baadaye ni vyema ufikiri kama mnunuzi, ila kama unataka kudumu nayo basi lazima ufikiri kama mmiliki. Ipo mifano mingi ya biashara zilizoanzishwa na kuuzwa, mojawapo ni kama whatsapp, ambapo mwanzilishi wake aliuza kwa mr. Mark ambaye ndiye mmiliki wa facebook. Whatsapp iliuzwa kwa dola billion 19 zaidi ya trilioni 38 za kitanzania.
5. Mafanikio yanahitaji muda, hivyo basi tafuta kufanya kitu ambacho unakipenda ambacho hutachoka kuwa mvumilivu. Huwezi kupata mtoto kwa mwezi mmoja kwa kuwapa wanawake 9 ujauzito. Lazima ujue kuna vitu vinahitaji muda, na unahitajika kuwa mvumilivu. Kwa hiyo katika safari ya kuelekea mafanikio chagua njia nzuri kwa kufanya kile unachopenda, maana kitu unachopenda kuvumilia sio kazi kubwa kama kuvumilia kitu usichopenda.
SOMA; Mambo Kumi(10) Muhimu Ambayo Kila Mhitimu Wa Elimu Ya Juu Mwaka 2015 Anatakiwa Kuyafahamu.
6. Sifa moja ya muhimu zaidi kwa mkurugenzi ni uongozi. Kama huwezi kuongoza basi huwezi kua mkurugenzi. Kua kiongozi sio lazima uwe umezaliwa na sifa ya uongozi, japo wapo wanaozaliwa na sifa za uongozi. Lakini unaweza kuijenga sifa ya uongozi kwa kujifunza. Vipo vitabu vingi vinavyoelezea jinsi gani ya kua kiongozi, hata jinsi gani ya kua mkurugenzi. Tenga muda wa kujifunza na kufanyia kazi unavyojifunza.
7. Katika maisha unapata kile unachopanda. Hii ndiyo kanuni. Ukitaka kuvuna mafanikio lazima upande mbegu za mafanikio. Huwezi kufanikiwa wakati kila mara wewe ni mtu wa kulalamika na kulaumu. Wewe sio mtu wa kuchukua hatua na unatoa udhuru kila wakati, halafu utegemee maisha yakunyookee? Ukipanda udhuru maisha nayo yatakupa udhuru. You get out of life what you put into it.
8. Jifunze kuongoza ukiwa mbele. Maana huwezi kuongoza ukiwa nyuma. Falsafa ya kuongoza ukiwa nyuma ilikua ikitumika hasa kwenye vita, ambapo mbele wanatangulizwa wale askari wa kawaida, halafu viongozi wanabaki nyuma. Falsafa hii ina lengo la kuwalinda viongozi, ili kama ni kufa basi viongozi wawe wa mwisho. Lakini falsafa hii inawafanya askari wajione wao ndio wanawekwa kwenye hatari zaidi. Ila kwa yale majeshi ambayo viongozi ndio wanakua mstari wa mbele, ndiyo yenye kushinda, maana askari wanakua na morali, ujasiri, na wanapambana kwa nguvu zaidi maana wanawaona viongozi wao, wako mstari wa mbele wakionyesha kwa vitendo. Hivyo kama wewe ni kiongozi lazima uongoze timu yako ukiwa mbele na sio ukiwa nyuma kwa kuwaamrisha. Show them you care—by leading from the front.
9. Sehemu kubwa ya kazi ya mkurugenzi ama ceo (chief executive officer) ni kuwatengeneza watu kuwa bora zaidi ya walivyokua mwanzo. Kama wewe ni ceo, lazima utambue kwamba kwa kadri watu unaowaongoza wanavyokua bora, ndivyo kazi yako inakua nzuri zaidi, na mafanikio yanaonekana. Kua ceo si suala la kwamba wewe ni bosi tu, lazima watu wako waongezeke viwango vya ubora.
10. Ili uwe ceo mzuri unatakiwa uweze kuchangamana hata na yule mfanyakazi wa chini kabisa kwenye kampuni. Uwe mtu wa kujali, na usiweke utofauti mkubwa na wafanya kazi wengine. Hata kama ni chakula kula wanachokula wengine. Uwe wa kwanza kufika ofisi na wa mwisho kutoka. To be a hero-ceo, spend time with your smallest customers and lowest employees.
11. Olewa au oa vizuri. Hapa mwandishi anasema kua unaweza kufanikiwa kwa kuoa au kuolewa na tajiri. Pia anatoa mbinu mbalimbali ambazo mtu anaweza kuoa au kuolewa na tajiri. Japo mtazamo huu kwa hapa tanzania unaweza ukaonekana sio sawa. Ila wapo baadhi ya watu wenye mtazamo huo, wa kuolewa na matajiri, wapo hata vijana wa kiume ambao wanaoa wazungu. Hata hivyo sio tatizo maana hakuna sheria wanayovunja. Mwandishi anasema ukitaka kuoa au kuolewa na tajiri, kwanza tambua sehemu ambapo hua wanapenda kuwepo. Mfano ni hoteli za hadhi gani ambazo ni rahisi kuwakuta matajiri. Mfano huwezi kwenda kwenye migahawa ya vichochoroni au hoteli za kawaida halafu ukutane na matajiri. Matajiri utakutana nao kwenye hotel kama za hadhi ya juu serena hotel, mount meru hotel, palace hotel na nyingine za hadhi hiyo.
SOMA; Unatumia Nguvu Kubwa Kulinda Unachodhani Ni Cha Thamani Wakati Unawaachia Watu Wachezee Kilicho Cha Thamani Zaidi.
12. Unaweza kutumia umaarufu kua tajiri au unaweza kutumia umaarufu wa utajiri kuendelea kuwa tajiri. Njia hii inatumiwa sana na wachezaji au wanamuziki. Mfano kwa hapa kwetu kama kina diamond, rose mhando. Kwa vile ni maarufu kila atakachokifanya, ana uwezo wa kukifanya kiweze kumuingizia kipato. Mifano mingine ya watu waliotumia umaarufu kutajirika ni kama kina oprah winfrey, david beckham, michael jordan n.k
13. Jifunze kuuza kwanza na vingine vitafuata. Kuuza ni taaluma ambayo kila mtu anapaswa kujifunza, maana kila mtu anauza. Hata kama wewe ni mwajiriwa unauza ujuzi wako na muda wako ndio unapata mshahara. Hata kama ni kibarua, unauza nguvu kazi yako ili upewe fedha. Hivyo kujifunza jinsi ya kuuza ni muhimu sana. Ujuzi wa kuuza ni wa muhimu na unapaswa kua kitu cha kwanza, maana vingine vitajengwa katika msingi huo. Unapoanza mapema kujifunza kuuza au ukiwa bado mdogo ndivyo inakua ni rahisi na haraka kujifunza, kuliko kujifunza kuuza ukiwa mtu mzima. People in their 40s who have never sold can learn, but it ’s harder, takes longer, and feels unnatural
14. Njia ambayo inayotumiwa na wengi kupata utajiri, ni kwa kuweka akiba na kuwekeza. Njia hii ndiyo njia inayotumiwa na wengi kusafiria kwenda kwenye utajiri. Japo njia hii itahitaji ujibane sana katika matumizi, na lazima uwe na kipato kikubwa. Kama kipato chako ni kidogo, itakuchukua muda mrefu sana kufikia uhuru wa kifedha.
15. Sehemu ya fedha unayoweka akiba iwekeze kwenye soko la hisa, na wekeza kwa muda mrefu. Ukiwekeza kwa muda mfupi ni vigumu sana kupata faida. Wanaonufaika na soko la hisa ni wale wanaofanya uwekezaji wa muda mrefu. Mifano ipo mingi sana yana matajiri ambao wamefanikiwa kupitia uwekezaji h wa aina hii. Ila mmoja ambaye ni maridadi sana kwenye uwekezaji wa aina hii ni warren buffet, tajiri wa 3 wa dunia. Yeye anasema anapowekeza anakua na malengo ya miaka hata zaidi ya 20. Ukinunua hisa leo na utegemee kuuza mwezi ujao, ni rahisi sana kupata hasara, na wahanga wengi wa soko la hisa ni wale wawekezaji wa muda mfupi.
16. Anza kidogokidogo lakini fikiri kwa ukubwa. Hata kama ni biashara ndogo kiasi gani, fikiri jinsi gani unavyoweza kuitanua na kuikuza zaidi. Mfano mcdonald, ni moja wa matajiri wanaomiliki migahawa. Migahawa yake imesambaa maeneo mengi ya dunia, kwa sasa imeshaenea takribani nchi 119, na amekua maarufu kwa migahawa. Start small —think huge.
17. Katika kupata mtaji, unaweza kutumia fedha zako ulizodunduliza au kuchukua mkopo kutoka benki au kwa wawekezaji. Ila unapochukua mkopo unakua huna uhuru na umiliki wa biashara yako. Ni vyema ukaanza mapema kudunduliza fedha zako, hata kama bado hujapata wazo la biashara. Hii itakusaidia pindi unataka kuanza kutekeleza wazo lako la biashara, unakua angalau na mtaji wa kuanzia. Kuliko ile ya kusubiria unaanza halafu ndio unaanza kuhangaika kutafuta mtaji kwa kukopa.
18. Fanya kile unachopenda, ila itakua vizuri zaidi kama kile unachopenda kinalipa vizuri. Maana kama unachokipenda ndicho utakachotumia muda mwingi kukifanya, kama hakilipi vizuri basi itakua vigumu kutajirika au itakuchukua muda mrefu sana. Do what you love—but it’s better if what you love pays really well.
SOMA; Acha Kujiua Mapema Kabla Ya Muda Wako.
19. Bobea kwenye kile unachofanya. Hakikisha unafika kwenye viwango wa juu kwenye kile unachofanya. Mfano mgonjwa mwenye tatizo la mifupa, atapendelea kwenda kwa daktari bingwa wa mifupa, kuliko kwenda kwa daktari wa kawaida. Hivyo hivyo ukiwa bingwa (mbobevu) kwenye kile unachofanya ni rahisi zaidi kupata wateja wa kununua huduma au bidhaa unayouza, maana watu watakua na imani na wewe maana ni daktari bingwa kwenye hilo eneo.
20. Linda wazo au biashara yako kisheria. (patent it or otherwise protect it). Ukilinda wazo lako la biashara, kama kuna mtu atataka kutumia wazo lako, mfumo wake, itabidi akulipe, kwa kuingia mkataba wa kisheria. Ila usipolinda kisheria ni rahisi mtu kuiba wazo lako na kupata utajiri huku wewe ukibaki maskini. Ndiyo maana kampuni au biashara zinakua na wanasheria. Hakikisha unakua na wanasheria maridadi sana, hata kama gharama zao ni ghali. Gharama utakazotumia kwa kua na wanasheria wazuri ni ndogo sana ukilinganisha zile ambazo unaweza kupoteza kwa kukosa wanasheria wazuri wa kulinda biashara yako.
Kama utapenda kupata kitabu hicho niandikie email kwenye dd.mwakalinga@gmail.com nitakutumia kitabu hicho.
Asanteni sana
tukutane wiki ijayo
makala hii imeandikwa na ndugu daudi mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe
daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: