Huu Ndiyo Mtaji Mkubwa Wa Mjasiriamali Katika Kufikia Mafanikio makubwa.

Ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio na kufikia mafanikio makubwa, huhitaji kuwa na mtaji mkubwa sana wa pesa ili kufika huko kama unavyofikiri. Unachohitaji ni kuwa na kitu kimoja tu ambacho wajasiriamali  wote wakubwa wanacho na ndiyo kimewafanya kufanikiwa zaidi. Kitu hiki sio kingine ni nidhamu binafsi na huu ndiyo mtaji mkubwa kwa mjasiriamali yoyote anayehitaji kufanikiwa.
Mara nyingi wengi tumekuwa tukiangalia nidhamu kwa masuala ya nje kama utii, heshima, unyenyekevu na mengine mengi yafananayo na hayo na kwamba kuwapo na dharau, kiburi, ufanywaji wa mambo ya aibu, unyama na mengine mengi pia huchukuliwa kwamba ni matokeo ya ukosefu wa nidhamu.
Ukiangalia suala la nidhamu katika nyanja zote za maisha yaani nidhamu binafsi, kimasomo, kikazi, kifamilia, muda na mengine mengi utaona nidhamu ya ndani ya mtu ndiyo inayoweza kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yake na kuleta ufanisi wa kazi au utendaji wa mambo ya mtu na kubadilisha mfumo mzima wa maisha.
Tatizo la wengi ni kule kuichukulia nidhamu kijuu juu sana kiasi cha kwamba kuiona ni kitu cha kawaida. Lakini kitu wasichojua kuwa, nidhamu inauwezo wa kumfanya mtu kufikia malengo yake na kuwa mtu wa tofauti kabisa na wengine wote wamzungukao. Kinachotofautisha mtu huyu na yule kimafanikio ni nidhamu binafsi na sio kingine.
Kama unaona ndani yako huna nidhamu binafsi. Nikiwa na maana nidhamu itakayokuongoza katika kufanya kitu sahihi na wakati sahihi ili kutimiza malengo yako halisi uliyojiwekea, basi mafanikio kwako itakuwa ni ngumu sana kuyafikia. Kinachohitajika ukiwa kama mjasiriamali ili uweze kufanikiwa unahitaji kwanza nidhamu hii binafsi tena ya hali ya juu.
Ni wazi kwamba watu wengi tumekuwa tukitafuta matokeo chanya katika elimu, kazi, biashara, jamii yaani kimaisha kwa ujumla, lakini imekuwa ni kazi nzito, ngumu na inayochosha sana kufikia malengo hayo kwa sababu ya kukosa nidhamu binafsi. Ukichukua muda na kujikagua kidogo utagundua maeneo mengi katika maisha yako yamekwama kutokana na wewe ulikosa nidhamu binafsi wakati fulani.
Juhudi zako nyingi na mipango uliyonayo mizuri haiwezi kukusaidia kitu kukuletea matokea mazuri unayotaka kama umekosa nidhamu ya kukufanikisha. Unahitaji nidhamu ambayo itakufanya ufanye mambo yako kwa usahihi na wakati sahihi. Wote wanaofanikiwa nataka nikupe ukweli huu hawabahatishi ndani yao wananidhamu binafsi.
Maisha kwa ujumla yanahitaji nidhamu ya hali ya juu ili kufanikiwa na kuwa miongoni mwa washindi. Vinginevyo utakuwa ni mtu wa kupoteza muda na kuwasindikiza wengine ingawa wewe mwenyewe binafsi unakuwa unajiona una juhudi za kutosha kumbe hakuna kitu. Ukosefu wa nidhamu ni adui mkubwa ambaye anazuia mafanikio makubwa ya watu wengi duniani bila kujijua.
Kabla hujaendelea na makala hii unaweza ukaishia hapa kwanza nakutafakari kwa muda kidogo tu kwa kujiuliza swali hili ‘Je, mimi fulani( Taja jina lako hapa) nina nidhamu binafsi? Kama ninayo katika maeneo gani? Au sina kabisa?’ Kama utagundua kuwa huna nidhamu binafsi inayokuongoza kufanikiwa katika maeneo mengi, basi utakuwa unapoteza muda kwa kile unachokifanya.
Ninasema hivyo kwa sababu ukosefu wa nidhamu unauwezo wa kuharibu na hata kufanya mipango ya mtu isitimie na hili ni jambo lipo wazi. Hata uwe na pesa au mtaji mkubwa vipi kama ukigundua ndani yako huna nidhamu nakupa uhakika wa asilimia zote huwezi kufanikiwa. Kwa sababu ni lazima pesa zote ambazo utazipata utazitumia vibaya utake usitake.
Kama nilivyoanza kusema mwanzoni kabisa mwa makala hii nidhamu ndiyo ngao na mtaji mkubwa wa mjasiriamali kufikia mafanikio makubwa. Haijalishi una mtaji au huna, wewe jiwekee nidhamu binafsi utaona mabadiliko makubwa yakitokea katika maisha yako. Wapo watu walianza chini kabisa lakini kwa sababu ya nidhamu waliokuwa nazo kwa sasa ni watu wenye pesa nyingi sana.
Kwa makala nyingine nzuri zaidi za TABIA ZA MAFANIKIO ikiwemo nidhamu binafsi hakikisha unajiunga na KISIMA CHA MAARIFA kuchota maarifa bora zaidi ya kuboresha maisha yako bila kupitwa.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hilo neno fuata maelekezo kwa ajili ya kujaza fomu. Baada ya hapo unatuma fedha kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 na unatuma username au email uliyojiunga nayo kwa meseji kisha unapewa ruhusa ya kusoma na kujifunza.
Nakutakia ushindi mkubwa katika safari yako ya mafanikio na pia tukutane katika DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: