Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha How To Live On 24 Hours A Day.

Habari rafiki msomaji wetu wa makala za mambo 20 ya kutoka kwenye kitabu cha wiki. Ni matumaini yangu unaendelea vizuri sana. Kama ilivyo desturi yetu, leo tunajifunza mambo 20 kutoka kwenye kitabu cha wiki. Wiki hii kitabu chetu kinaitwa HOW TO LIVE ON 24 HOURS A DAY (jinsi ya Kuishi Kwenye Masaa 24 ya siku). Mwandishi wa kitabu hiki ni Arnold Bennett. Mwandishi anadadavua njia mbalimbali za kuweza kuyatumia masaa 24 ya kila siku kwa manufaa. Mwandishi anaelezea kwamba muda ndiyo bidhaa ambayo kila mmoja wetu hapa duniani anayo tena kwa kiwango sawa. Kila mtu anayo masaa 24 kwa siku. Lakini utoafuti wetu unatokana na jinsi kila mmoja anavyotumia hayo masaa 24.

 
Karibu sana tujifunze
1. Muda una thamani kuliko fedha. Japo kuna usemi unasema Muda ni Pesa. Lakini ukweli ni kwamba muda ni zaidi ya fedha. Ukiwa na muda unaweza kutengeneza fedha, lakini ukiwa na fedha huwezi kuongeza hata dakika moja ndani ya masaa 24 ya siku.
2. Muujiza wa muda ni kwamba, muda ni wa kwako binafsi na hakuna mtu anayeweza kukunyang’anya muda wako. Huwezi kutumia leo muda wa kesho, hata lisaa limoja la mbele huwezi kulitumia kwa wakati wa sasa. Muda sio kama fedha, kama vile fedha uliyoweka kwa matumizi ya kesho unaweza kubadili mawazo na kuitumia wakati huu, lakini kwa muda sio hivyo, huwezi kukopa muda ujao ili uutumie wakati huu.
3. Huwezi kupata muda wa ziada: “Nikipata muda nitafanya hivi na vile”. Wengi wetu hujifariji kwa kauli kama hiyo. Hua tunafikiri tunaweza kupata muda wa kufanya jambo, ukweli ni kwamba huwezi kupata muda wa ziada zaidi ya ulio nao. Chakufanya ni wewe kutengeneza muda, kwa kuachana na shughuli zisizo na manufaa na kufanyia kazi hilo jambo la muhimu. Ni kile unachofanya sasa ndicho kinachojalisha na si kile unachotarajia kufanya. We never shall have any more time
4. Kufanikiwa au kutofanikiwa kuko ndani ya hayo masaa 24. Yaani uchawi wote wa mafanikio upo ndani ya haya masaa 24 ya kila siku na si zaidi ya hapo. Vitu vinavyotutofautisha ni vile tunavyovifanya ndani ya siku. Kwa maana hiyo wewe na Bill Gate tajiri wa dunia mnatofautiana katika matumizi ya masaa 24.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha Ten Roads To Riches(Njia Kumi Za Kuelekea Kwenye Utajiri).
5. Ubora wa Siku yako unategemea ubora wa asubuhi yako. Asubuhi ni ya muhimu sana tena sana. Ukiiharibu asubuhi yako basi umeharibu siku nzima. Nini unacholisha ubongo wako wakati wa asubuhi na mapema? Mara nyingi tunaamka na kuanza kufikiria shida zinazotukabili, au changamoto tulizonazo sisi au ndugu zetu. Pia wengi wetu tunaamka na kusikiliza habari, kuangalia tv, kuperuzi mitandao n.k Bahati mbaya asilimia zaidi ya 90 ya taarifa hizo ni habari mbaya, na zisizokua na machango wowote kwenye malengo ya maisha yetu. Hivyo akili zetu zinalishwa taarifa mbaya asubuhi na mapema, hivyo tunaanza siku kwa kukosa hamasa, kua na hofu na hata kukosa matumaini. Ni vizuri ukaanza kuitengeneza siku yako kwa kuamka na hamasa asubuhi. Unapoamka tafuta kitu kizuri cha kukuhamasisha. Kumbuka kinachoanza kuingia akilini mwako cha kwanza ndicho kinadumu na kuendesha siku yako.
6. Tenga dakika 90 (Saa moja na nusu) kila baada ya siku moja (angalau siku tatu kwa wiki) muda huo ni ajili ya kuilisha akili yako. Kukua kwako kunategemea ukuaji wa akili yako, ubora wa akili yako unategemea na ubora wa chakula akili inachopata. Usipotenga muda na vitu vya kuilisha akili yako, basi akili yenyewe itajichagulia chochote kile. Unapoona mtu mzima lakini anaongea pumba, basi ujue akili yake imekua ikipata pumba. Kumbuka kimtokacho mtu ndicho kimjazacho.
7. Dhibiti mawazo yako (Control your thoughts). Unaweza kuthibiti jinsi ya kuwaza. Ndiyo ni kweli tunakutana na mengi, lakini wewe ndiye mwenye uwezo wa kuamua nini kiingie kwenye akili yako. Mawazo kwenye akili yako yanategemea na nini umeruhusu kuingia humo akilini. Akili ni rahisi kuweka mawazo hasi au mabaya kuliko kuweka mawazo mazuri. Hakikisha kila unachowaza kiko sahihi na kinaweza kukuletea matokeo chanya, kama sivyo badilisha haraka mawazo hayo. Mambo mengi yanayotutokea ni matokeo ya kuwaza kwetu. Ukiweza kudhibiti mawazo utakua umepiga hatua kubwa saana. Fanya mazoezi mpaka akili izoee kuwaza mawazo chanya yenyewe.
8. Akili ni mashine ambayo inahitaji uangalizi wa karibu sana. Unapoamka asubuhi na mapema kitu cha kwanza kukipa kipaumbele inapaswa kua ni hiyo mashine ya kufikiri (Akili au ubongo). Watu tukiamka tunajiandaa, mwilini tunatafuta nguo nzuri tunavaa halafu tunajiangalia kwenye kioo, halafu tunaendelea na shughuli za siku kama ni kazini tunakwenda kazini. Je kama vya nje vinapewa kipaumbele hivyo, kwa mashine inayokuendesha siyo zaidi? Hakikisha asubuhi akili yako iko sawa, na itakua sawa kutegemea imepata kifungua kinywa cha namna gani. Unapoamka soma kitu chenye kuleta hamasa, au sikiliza mafundisho mazuri ya kuhamasisha, halafu tumia hata dakika 10 tu, tulia kimya kwa utulivu, usifikirie matatizo uliyonayo au mipango ya siku hiyo iweke pembeni kwa wakati huo.
9. Tenga muda wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni kwa afya ya kimwili na kiakili pia. Ufanyaji kazi wa akili yako siku umefanya mazoezi ni tofauti sana na siku hujafanya zoezi. Hebu fanya jaribio hilo. Tenga muda wa asubuhi dakika chache za kufanya zoezi lolote lile lenye kufanya utoke jasho. Siku hiyo linganisha na siku ambazo hufanyi kabisa mazoezi, halafu utaona utofauti.
SOMA; Mambo 20 niliyojifunza kwenye kitabu 85 INSPIRING WAYS TO MARKET YOUR SMALL BUSINESS. (Njia 85 za kutangaza biashara yako)
10. Furaha haiji kwa kununua vitu vya kufurahisha au kupendeza. Furaha ya kweli inatoka ndani, na furaha sio hitimisho, furaha inapaswa kua ni safari. Kama utafurahi pale tu utakapokuwa umetimiza kitu Fulani au umepata kitu Fulani, basi utakua na furaha mara chache sana. Furaha inapaswa kuwepo katika safari ya kuelekea kwenye kile kitu tunachokitaka kukifanikisha. Mfano kama unataka kujenga nyumba, usisubiri uwe na furaha siku umekamilisha, unapaswa kuwa na furaha kwenye mchakato mzima wa kujenga, kuanzia kuweka msingi, kununua vifaa vya ujenzi, kupandisha kuta, kupaua, kuweka bati, kupiga rangi na hata kumaliza. Hatua zote hizo unapaswa kuwa mwenye furaha. Happiness is not a destination, is a journey
11. Kisababisho na matokeo (Cause and effect). Kila kitu kinachotokea kina kisababisho chake, kwa kujua au kutokujua, kila kitu ni matokeo ya kitu fulani. Habari njema ni kwamba visababisho vingi viko ndani ya uwezo wetu. Hivyo basi tuna mchango mkubwa sana kwenye mambo yanayotupata na kukutana nayo. Huwezi kubadili mambo kwa kupambana na matokeo (effect), kama kweli unataka kubadili mambo lazima ubadili chanzo au kisababisho (cause). Umasikini ni matokeo, hupaswi kupambana na umasikini, tafuta kisababisho chake.
12. Serious reading: Soma vitabu haswa, ila usitumie muda mwingi kusoma novel, kama kweli uko serious na unataka kubadili maisha yako, achana na novel. Soma vitabu vya kuhamasisha, vitabu vya fani unayotaka kuifanyia kazi. Pia mashairi ni mazuri sana.
13. Usomaji wa magazeti ni upotezaji wa muda. Magazeti yameandikwa haraka haraka kwa wasomaji wa haraka haraka. Hata habari zilizomo ni za haraka haraka tu. Na ndio maana kama gazeti ni la kila siku, ikipita siku hiyo halina thamani tena na haliuziki tena. Ni tofauti na vitabu, vipo vitabu vya karne kadhaa zilizopita lakini mpaka leo vina hazina kubwa.
14. Fanya tafakari ya kile unachokisoma. Kila unapomaliza tenga muda wa kutafakari ulichojifunza. Usisome tu ili kumaliza kitabu, chukua muda wa kutafakari, hebu angalia ni wapi unaweza kutumia yale uliyojifunza.
15. Tazama mazuri na sio mabaya. Moja ya mambo yanayosababisha watu kukosa furaha ni kutokua na shukrani kwa mambo mazuri, badala yake tunawaza mambo mabaya tu. Hata kuwepo hai tu ni jambo zuri. Shukuru kwa yale mazuri, na tumia muda wako kuwaza na kutegemea mazuri. Maana utakachotumia muda mwingi kukiwaza ndicho kitakachokupata, ukiwaza sana mabaya, ndipo utapata mabaya zaidi. Whata you focus on grows
16. Tuna uwezo mkubwa sana, kuliko ule tunaoutumia. Kila mtu anayo uwezo mkubwa na laiti tungekua tunalijua hili. Hakuna anayeweza kutumia uwezo wake wote aliokua nao, maana tungeona miujiza tu. Hii inatufunza kwamba yale mawazo ya kwamba maisha yetu hayafanikiwi kwa sababu eti ya Fulani, au Fulani hajakusaidia ni kujipotosha wenyewe. Unapoanza kutambua kwamba uwezo wa kubadilisha maisha yako uko mikononi mwako unakua umeanza safari muhimu sana kuelekea mafanikio.
SOMA; Mambo Nane(8) Yatakayokufanya Uwe Na Fikra Chanya Kila Wakati Ili Uweze Kufikia Mafanikio.
17. Fanya kazi kwa bidii, ila hakikisha hauchoshwi na kazi hadi kushindwa kufanya mambo mengine. Tengeneza uwiano mzuri wa kazi na mambo mengine ya msingi, Pata muda mzuri wa kupumzika. Akili inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama imepumzika vya kutosha.
18. Muda ni Mtaji. Mtaji sio pesa tu. Utakuta mtu amemaliza chuo, yupo mtaani hana kazi na hana shughuli ya kufanya, akiulizwa anajitetea “Sina mtaji”.. Sasa je mtaji ni fedha tu? Muda unaopoteza umekosa kabisa cha kufanya ili kuongeza thamani yako? Tumia muda ulio nao kujifunza kitu kipya kila wakati uone kama utabikia vilevile . Mtaji wako wa kwanza na wenye thamani ni muda wako. Unaposikia mfanyakazi anafanya kazi kwa masaa 8 kwa siku, ina maana anamuuzia mwajiri wake masaa 8 kila siku. Lakini thamani ya masaa 8 inatofautiana na mtu na mtu. Na kinachotofautisha ni thamani ya mtu. Mfano Wafanyakazi wawili wanaweza kua wanafanya kazi wote masaa 8 kila siku lakini mmoja analipwa Milioni 1 kwa mwezi mwingine laki 5.
19. Linda muda wako usipoteze kwa mambo yasiyokua na maana. Ukishapangilia siku yako, na muda wa kila shughuli, hakikisha unaulinda muda wako usitumike nje ya utaratibu uliweka. Kaa mbali na vishawishi vyovyote kama simu, mitandao ya jamii, kaa mbali na wapiga soga (wambea) n.k
20. Jiwekee kanuni, miiko na taratibu zako mwenyewe na uzifuate (principles, conduct). Jiulize Wewe binafsi tunu zako ni zipi? (what are your core values), je umeshawahi kujiwekea kanuni au taratibu na ukawa mwaminifu kuzifuata? Kitu kisichokua na kanuni hakina thamani, na pengine huna thamani hayafuati kanuni Mafanikio pia yana principles zake, Kuishi maisha ya furaha nako kuna kanuni zake… Weka kanuni na taratibu kulingana na unataka kua nani na unataka kufika wapi. Uhuru unapatikana katika kuelewa na kufuata kanuni, sheria na taratibu.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: