Tabia 4 Zitakazokuongoza Kutambua Na Kutumia Fursa Vizuri.

Wengi wetu mara nyingi tunajua au tumeshawahi kusikia kuwa fulani ana bahati sana katika maisha yake. Ni kitu ambacho tumekuwa tukilishwa sana pengine tokea enzi za utoto wetu mpaka sasa, na kuamini kwamba wapo watu wenye bahati zao katika haya maisha. Hii ni imani ambayo imekuwa ikiwapoteza wengi na kusababisha wengi kushindwa kujituma na kusubiri huo muujiza wa bahati uwafikie.
Kitu cha kujiuliza hapa je, kuna ukweli wowote unaohusiana na hilo kuwa wapo watu ambao wanabahati sana katika maisha yao? Bila shaka hapa jibu ni HAPANA. Hakuna kitu kinachoitwa ‘bahati’ isipokuwa yapo maandalizi yanayayopelekea hiyo ‘bahati’ unayoiona kutokea. Kuelewa vizuri hili angalia wale wote unaowaona wana ‘bahati’, utagundua matendo na tabia zao ndizo zilizowafanikisha na sio kitu kingine.
Kwa maana hiyo zipo tabia ambazo kama mtu anakuwa nazo zinakuwa zinamwongoza kwenye hizo ‘bahati’, lakini zaidi pia hata katika kuzitambua na kuzitumia fursa vizuri zinazojitokeza. Watu wenye mafanikio makubwa mara nyingi wanazitumia tabia hizi kufikia malengo yao. Kitu kikubwa unachotakiwa kujua ni kuwa, huhitaji ‘bahati’ kama unavyofikiri ili kuweza kuzitambua na kutumia fursa vizuri. Kitu unachohitaji ni kujijengea tabia hizi.
Inawezekana ukawa ni miongoni mwa watu wanaotaka kuzitumia fursa vizuri tena na mapema kabla wengine hawajaziona. Nikiwa na maana unataka kuwa na jicho la tatu la kuona zaidi kabla ya wengine. Kama ni hivyo upo sahihi na ni kitu ambacho kinachowezekana. Kwa kuzijua tabia hizi zitakusaidia kuweza kuzitambua na kuzitumia fursa vizuri  hadi kufikia mafanikio makubwa uliyojiwekea. Na tabia hizo unazotakiwa kujijengea ni hizi hapa:-
1. Tabia ya kujifunza kupitia changamoto.
Ukijaribu kuchunguza watu wanaojifunza kupitia changamoto wanazopitia, bila shaka ni wachache sana. Wengi ni watu wakuhuzunika, kusononeka na kulalamika sana kila wanapokutana na changamoto katika maisha yao. Ili uweze kuziona fursa vizuri, jifunze kitu kupitia changamoto hizo ulizonazo.
Kwa kadri jinsi utakavyozidi kujifunza utagundua kwamba utaanza kuyaona mambo kwa utofauti hali itakayokupelekea kuwa mbunifu na pengine kutambua fursa nyingine. Acha yale mazoea ya kukaa na kuanza kualamika, jifunze kitu na mafanikio utayaona kwa utofauti.
2. Tabia ya kujiamini.
Hakuna kitu kikubwa utakachoweza kukifanikisha kama wewe mwenyewe utakuwa hujiamini kwa kiasi kikubwa sana. Mafanikio yote yanaanza wa kujiamini. Unapokuwa unajiamini zaidi unakuwa una uwezo wa kuona au kufanya mambo mengi ambayo siyo rahisi kufanywa na watu wengine hasa ambao hawajiamini.
Kwa kufanya mambo hayo ndivyo ambavyo utajikuta unazidi kugundua fursa nyingi zinazojitokeza kwa upande wako. Siyo rahisi sana kama hujiamini kutambua fursa nyingi zinazojitokeza. Hii ni kwa sababu kila utakachokiona kuwa ni fursa utakiona hakifai na kukiacha. Ni muhimu kujiamini ili kuzitambua fursa vizuri zinazojitokeza.
3. Tabia ya kuwa makini na mazingira yanayokuzunguka.
Mara nyingi mazingira yanayotuzunguka ndiyo ambayo yanatupa fursa tunazozitafuta kila siku. Wapo watu ambao mara kwa mara huwa ni watu wa kuangalia fursa zilizo mbali na pale walipo na kujikuta kusahau hata yale yaliyokaribu nao. Ni muhimu ukajiuliza ni kipi kinachokuzunguka ambacho unaweza kukigeuza kikawa fursa katika maisha yako?
Ni vizuri ukachukua muda ukajiuliza ni kipi ambacho utaweza kukitoa cha thamani katika mazingira uliyopo? Najua huwezi kukosa kabisa. kwa kufanya hivyo utakuwa unajitengenezea uwezo mwingine wa kugundua fursa zinazojitokeza na kuzitumia.
4. Tabia ya kuwa mbunifu.
Hiki ni kitu ambacho wengi wanakikwepa lakini ubunifu unapotumika husaidia kuweza kugundua mambo mengi ambayo kwa wengine siyo rahisi kugundua. Kwa sababu kila mara na kila wakati utakuwa unajitahidi kubuni kitu ambacho kitaenda sawa na wakati huo. Kwa ubunifu huo utakaouendeleza utakuwezesha wewe kuzitambua fursa nyingi zaidi.
Kwa kuzitumia tabia hizo na kuzifanyia kazi zinauwezo wa kukufanya na kuweza kutambua fursa kila zinapojitokeza.
Kwa makala nyingine nzuri tembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
TUNAKITAKIA USHINDI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO ULIYONAYO.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: