Kitabu Cha Mwezi Oktoba; DEAD AID (Kwa Nini Misaada Sio Suluhisho Kwa Nchi Masikini Na Nini Cha Kufanya.)

Baada ya vita vya pili vya dunia na kuundwa kwa vyombo vya kuunganisha mataifa duniani kama umoja wa mataifa, mataifa yaliyokuwa na nguvu yalifikia maazimio ya kusaidia nchi ambazo zimekuwa na hali ngumu. Na njia bora ya kusaidia nchi hizi ilionekana ni kutoa misaada.

 
Hivyo tangu miaka ya 1950 misaada mingi sana imekuwa inatolewa kwa nchi masikini. Misaada hii ilionesha mafanikio mazuri kwa baadhi ya nchi za ulaya zilizopata misaada hii, na nyingi ziliimarisha uchumi wao.
Kwenye miaka ya 1960 ambapo nchi nyingi za Afrika zilianza kupata uhuru, nchi nyingi zilikuwa na hali ngumu sana kiuchumi. Zilikuwa zina umasikini mkubwa sana. Hivyo mataifa makubwa na umoja wa mataifa wakakubaliana kwamba njia pekee ya kusaidia nchi masikini za Africa ni kutoa misaada.
Hivyo misaada ikaanza kumiminika kwa kasi sana huku afrika kuanzia miaka ya 1970 na mpaka sasa. Ukiangalia kwa juu juu unaweza kuona misaada hii imesaidia sana nchi za Afrika kuimarisha uchumi wao. Lakini hii si kweli.
KITABU CHA SEPTEMBA; Guide To Investing(Muongozo Wa Uwekezaji).
Mchumi wa kimataifa mwenye asili ya Afrika, raia wa Zambia anayefanya kazi marekani, Dambisa Moyo alikaa chini na kufuatilia kwa makini tangu misaada ilipoanza kuja Afrika mpaka sasa hivi. Na alichogundua ni kwamba, misaada inayokuja huku Afrika haikuzi uchumi wala kuondoa umasikini, bali imezidi kuongeza umasikini.
Mwandishi huyu amechambua sana ujio wa misaada na jinsi ambavyo imeshindwa kufikia lengo ambalo ilikusudiwa mwanzoni. Yote haya ameyachambua vizuri sana kwenye kitabu chake chenye jina DEAD AID.
Hiki ni kitabu ambacho natamani sana kila Mwafrika akisome, hasa watengeneza sera na hata sisi wananchi kwa ujumla. Tumekuwa tukiona viongozi wetu wa kubwa wa nchi wakijisifu kwamba wamekwenda nje ya nchi na kupata misaada. Na wakati mwingine wamekuwa wakisema hatuwezi kufanya kitu fulani kwa sababu tutakosa misaada. Misaada hii tunayoona ni keki kwetu imegeuka kuwa laana kwetu.
Kupitia kitabu hiki, Dambisa ameeleza vizuri sana jinsi ambavyo misaada imechochea ufisadi kwenye nchi za Afrika. Akitoa mfano wa aliyekuwa kiongozo wa Congo, Mobutu Seseko, ambaye inasemekana alifanya ufisadi mkubwa kuliko fedha ambazo zililetwa nchini kwake kama msaada.
Kuna vitu vingi sana ambavyo vipo nyuma ya misaada ambavyo kama hujui huwezi kuona madhara yake kwenye uchumi.
Kwa mfano, kuletwa kwa vyandarua vya msaada unaweza kuona ni msaada mkubwa sana kwetu. Lakini kuja kwa vyandarua hivi, ambavyo vinatolewa bure vimeua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza vyandarua kwenye baadhi ya mataifa ya afrika.
Pia misaada hii ambayo imekuwa inakuja kwa fedha za kigeni imekuwa inashusha dhamani ya fedha husika, na imekuwa inaongeza mfumuko wa bei. Dambisa ameeleza vyema sana kwenye kitabu hiki, na ukisoma utaelewa vizuri.
KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
Mwisho kabisa ameeleza ni njia gani ambayo mataifa ya Afrika yakitumia yanaweza kuondoka kwenye umasikini, na njia hiyo sio misaada. Ni njia ambayo ni bora sana kama ikiweza kutumika vizuri. Sitakuambia njia hiyo hapa, bali pata kitabu hiki uweze kuisoma na kuielewa vyema.
Kwenye kitabu hiki Dambisa amezungumzia misaada kwa ngazi ya mataifa, lakini kwa nilivyokisoma kinaweza kukusaidia kwenye ngazi ya mtu binafsi. Kama hapo ulipo unafikiri ukipata msaada ndio maisha yako yatakuwa bora, unajidanganya sana. Soma kitabu hiki na utapata fikra bora sana za jinsi gani unavyoweza kuondokana na mawazo hayo ya kutegemea msaada na kuanza kujitegemea wewe mwenyewe na kuweza kukuza uchumi wako binafsi.
Kwa mwezi huu wa kumi, nakusihi sana usome kitabu hiki, kitakupa mwanga mkubwa sana kwenye uchumi kwa ngazi ya nchi na hata ngazi ya mtu binafsi.
Jinsi ya kupata kitabu hiki.
Kama ulishajiunga na AMKA MTANZANIA kwa email tayari umeshatumiwa kitabu hiko kwenye email yako.
Kama bado hujajiunga, BONYEZA MAANDISHI HAYA NA UWEKE EMAIL YAKO  kisha nenda kwenye email yako udhibitishe kujiunga na utatumiwa kitabu hiko na vingine saba kwenye email yako
Hakikisha huachi kusoma kitabu hiko ambacho kitakupatia mwanga sana juu ya misaada.
Nakutakia kila la kheri kwenye kufanyia kazi haya ambayo unajifunza.
TUPO PAMOJA.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: