Huu Ndiyo Uwekezaji Ambao Hutakiwi Kuukwepa Katika Maisha Yako.

Mara nyingi katika safari ya mafanikio tumekuwa tukiwekeza katika mambo mengi kama ardhi, majengo, hisa na mambo mengineyo. Huu ni uwekezaji ambao tumekuwa tukiufanya mara kwa mara katika maisha yetu. Na kwa kufanya uwekezaji huo umekuwa ukitusaidia kufikia mafanikio makubwa.
Pamoja na umuhimu huo lakini wengi tumejikuta tukiwa ni watu wa kusahau au kukwepa kuwekeza katika eneo lingine katika maisha yetu ambalo ni muhimu pia kwa mafaniko yetu ya kila siku. Ni uwekezaji ambao ni rahisi unaweza ukafanywa na kila mtu, lakini wengi wamekuwa wakiukwepa bila kujua. Je, unajua ni uwekezaji gani ambao hutakiwi kabisa kuukwepa katika maisha yako?
Huu Ndiyo Uwekezaji Ambao Hutakiwi Kuukwepa Katika Maisha Yako.
1. Tahajudi (Meditation)
Sio kila wakati ambapo utakuwa unawaza tu maisha. Kuna wakati ambapo unatakiwa kutuliza mawazo yako na kuongea na wewe mwenyewe. Hiki ni kipindi ambacho unalamikia kufanya ‘meditation’au tahajudi. Ni wakati ambapo mawazo yako unatakiwa kuyatuliza na kufkiria jambo moja tu, pengine juu ya maisha yako.
Huu ni aina ya uwekezaji ambao ni muhimu sana kwako kuweza kuufanya. Kwa sababu unapofanya ‘meditation’ kila siku hata iwe kwa dakika 15 yapo mambo mengi ambayo utajifunza ikiwemo pamoja na majibu ya mambo mengi ambayo unakuwa huna. Wanamafanikio wengi wanafanya sana tahajudi na pia ni tabia ambayo unaweza ukajifunza na kuiendeleza.
2. Kufanya mazoezi.
Kati ya kitu muhimu ambacho kinaweza kikakujengea afya bora ni mzoezi. Watu ambao wanatabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara, mara nyingi pia miili yao ina afya nzuri. Ni kitu ambacho unatakiwa kukilelewa kuwa bila kufanya mazoezi kwa vyovyote vile lazima mwili wako uwe na afya ambayo siyo nzuri sana.
Kumbuka tunahitaji miili yeye afya ili kufikia mafanikio. Sasa kama ni hivyo yapo mambo mengi yanayohitajika ili kuuipa miili yetu afya ikiwemo pamoja na  mazoezi. Wengi wenye tabia ya kufanya mazoezi huwa siyo rahisi kushambuliwa na mgonjwa. Kwa msingi huo unaona kwamba mazoezi ni jambo la lazima kwa mjasiriamali kufanya na kuwekeza kwa ajili ya kujijengea afya bora.
3. Kujisomea.
Hii ni moja ya tabia muhimu sana ambayo mjasiriamali yoyote yule analazimika kuwekeza ili kufikia mafanikio makubwa. Ni lazima kwa mjasiriamali kutambua kwamba anahitajika kujifunza tena kila siku. Kujifunza huku tena kunatakiwa kuwa kwa kasi ili kendana na mabadiliko ya dunia, vinginevyo atajikuta anabaki nyuma ktika safari yake ya mafanikio.
Kwa kadri utakavyozidi kuwekeza katika kujifunza, mambo mengi sana utajifunza kwa muda mfupi ambao hukutegemea. Hivi ndivyo ambavyo wajasiriamali wenye mafanikio wanavyofanya. Maisha yao karibu yote wamewekeza sana katika kujifunza. Na ni jambo ambalo hata wewe unatakiwa kulichukulia kwa umakini kwa ajili ya mafanikio yako ya leo na baadae.
4. Kupata usingizi wa kutosha.
Haitoshi tu kufanya mazoezi ili kujijengea afya bora. Halikadhalika pia usingizi wa kutosha unahitajikia ili kuwa na afya bora pamoja na akili yenye nguvu. Ninapozungumzia usingizi si maanishi unakuwa unalala tu kupitiliza, hapana. Unatakiwa ufikie mahali ambapo ukitaka kulala lala usingizi wa kutosha angalau masaa sita, ingawa kitaalamu unashauriwa kulala saa nane.
Wengi ambao wanakuwa wanalala usingizi ule unaohitajika hujikuta ni watu ambao akili zao zinafanya kazi sana vizuri. Hiki ni kitu mbacho utakiwa kukijua pia na ni aina ya uwekezaji ambao kwako ni lazima uufanye. Ili kuweza kufanikiwa katika hili ni muhimu kutambua kwamba unatakiwa kutunza muda wako vizuri, ili inapofika saa ya kulala na ulale usingizi wa kutosha.
5. Kuwa na mshauri wako ‘Mentor’
Ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa ni lazima kwako kuwa na ‘mentor’ au mshaui ambaye atakuwa anakuongoza kukuelekeza kwenye njia ya mafanikio. Hii itakuwa kwako ni njia rahisi ya kuweza kufika kule unakotaka na utakuwa umefanya uwekezaji mzuri ambao utakusaidia kufanikisha ndoto zako, kwani mambo mengi hutakosea sana kama ungekuwa peke yako tu.
Kwa kifupi, huo ndiyo aina ya uwekezaji ambao unatakiwa kuufanya pia katika maisha ili kujijengea mafanikio makubwa katika safari yako ya ujasiriamali.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikiona endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza na kuhamasika.
Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuboresha maisha yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: