Tengeneza Kipato Cha Ziada Huku Ukiendelea Kufanya Unachofanya Sasa.

Habari za leo rafiki?
Naamini unaendelea vizuri sana, hongera kwa hilo.
Na pia nina hakika unaona tofauti ya maisha uliyokuwa unaishi kabla na maisha ambayo umeanza kuishi sasa baada ya kuanza kujifunza na kuchukua hatua.
Nina hakika kwa sasa umeanza kupata matumaini mapya, umeanza kupunguza hofu na pia umeanza kuvunja minyororo iliyokuwa inakuzuia kufikia mafanikio makubwa.
Sasa unaelekea kupata uhuru kamili wa maisha yako, kuishi vile unavyopenda na kuwa na mchango mkubwa kwa wengine. Hii ndio maana halisi ya maisha. Nakupongeza kwa hili. Na kama kuna wachache ambao hawakuelewi usiwe na shaka, endelea kuwa bora na wataelewa tu.
Juzi kwenye ukurasa wangu wa Facebook niliwauliza marafiki je mpango wa maisha wanaoishi sasa wameupata wapi? Je wameupata kwa wazazi, kwa marafiki, kwa kuangalia tamthilia au wamepanga wenyewe? Nawapenda sana marafiki zangu kwa sababu walikuwa wawazi. Wengi walisema wamepata mpango wao sehemu nyingine na sio mipango yao halisi.
Niliuliza swali jingine tena, ikiwa mpango wanaoishi sasa wanaufurahia na wameridhika nao. Wengi walisema hawajaridhishwa nao kabisa. Na pia nikauliza wanafikiri wakifanya nini watakuwa na mpango wa maisha ambao unawaridhisha? Hapa nilipata majibu mazuri sana. Wengi walisema wanahitaji kuweka juhudi zaidi kwenye kile wanachotaka na kutokukata tamaa. Ni hatua nzuri sana ambazo watu wanachukua.
Katika majibu ya marafiki hawa, kuna jibu moja ambalo lilinifanya nifikiri tofauti na pia nimeona kuna wengine wengi wanaweza kuwa kwenye hali hii. Rafiki aliandika;

Kazi ninayofanya ninaipenda, lakini nahitaji kufanya kitakachoniongezea kipato bila kuacha kazi ya sasa.

Nilimjibu rafiki baadhi ya njia anazoweza kutumia, lakini msingi mkubwa nilimwambia, hapo alipo ndipo mgodi wenyewe ulipo. Kama kazi anayofanya ndio anaipenda kweli, basi ni vyema akaanza nayo katika kuongeza kipato chake.
Nimeona nikushirikishe hapa na wewe rafiki huenda ukawa kwenye hali kama hii. Unafanya kazi unayoipenda lakini kipato hakikutoshi. Na unaangalia ni wapi pa kuweza kuongeza kipato hiko.
Sasa leo nakupa sehemu moja ya uhakika ya kuanzia kujenga msingi wa kuongeza kipato chako kama kweli unachofanya sasa unakipenda.
Kwanza kabisa jua hapo ulipo ndipo penye hazina kubwa. Unapokuwa unapenda unachofanya, haiwi tena kazi kubwa kwako bali inakuwa sehemu ya maisha yako. hata ukiamshwa usingizini saa tisa usiku na ukapewa kazi yako utakuwa unaifurahia kufanya.
Kama umeshafika kwenye hatua hii, nataka nikupe njia moja ambayo itakuweka wewe mbali sana na kukuandaa kupata mara dufu ya kipato chako cha sasa. Na njia hiyo ni kujitengeneza wewe kuwa Mamlaka(authority) kwenye ile kazi unayofanya. Hapa unakuwa bora sana kiasi kwamba mtu yeyote akitaka kujua chochote kuhusu kazi ya aina hiyo unayofanya, ni lazima akutafute wewe.
Hapa unajua vizuri kile unachokifanya, unajua kimetoka wapi, kwa sasa kipo wapi na hata mbeleni mwelekeo ukoje. Hapa utakuwa unajua changamoto ambazo watu wanapitia kutokana na kile unachofanya na njia ya kuepuka changamoto hizo. Yaani wewe ndio unakuwa kila kitu kwenye ile kazi unayofanya au utaalamu ulionao.
Unaanzia wapi sasa?
Unaanza kwa kuwa na blog. Blog hii utakuwa unaandika hayo tuliyojadili hapo juu. Unaandika kwa utaalamu na jinsi ambavyo jamii inaweza kufaidika kwa ile kazi au taaluma uliyonayo.
Kwa mfano kama unafanya kazi benki, unahusika sana na fedha au mipango ya fedha. Angalia ni jinsi gani mwananchi wa kawaida anaweza kunufaika na kile unachofanya. Kuna watu wengi hawana matumizi mazuri ya fedha, kuna watu wengi hawajui wanawezaje kunufaika na benki. Kupitia blog ambayo unaanzisha, unakuwa unaweka elimu ya aina hii na hivyo kujijenga wewe kuwa mamlaka ambapo mtu akiwa na shida anakutafuta.
Hivyo hivyo kama wewe ni injinia, afisa ustawi wa jamii, daktari, mwalimu na kadhalika. Chochote unachofanya unaweza kuinufaisha jamii na wengine wanaokifanya kwa kuwa mtaalamu kwenye eneo hilo.
Sasa ukishakuwa mtaalamu unanufaikaje? Kwanza thamani yako kwenye kazi inaongezeka. Wakati unajifunza ili uwashirikishe wengine, na wewe unayatumia kwenye kazi yako na hivyo utazidi kuwa bora, na kipato chako kitaongezeka.
Utapata watu ambao watahitaji uwashauri zaidi na huenda uwaongoze kutokana na changamoto wanazopitia, hapa napo utatoza ada kulingana na mipango yako.
Pia unapokuwa mamlaka unaweza kuandika kitabu na kuuza kwa kuanza na wasomaji wako na kikasambaa kwa wengine.
Unahitaji nini ili kuanza?
1. Unahitaji blog, ambayo itakuwa kama sehemu yako ya kujenga utaalamu huu na kuwashirikisha wengine.
2. Unahitaji kutenga muda angalau saa moja kila siku kwa ajili ya kuandika na kuwashirikisha wengine yale muhimu. Pia muda huu utautumia kufanya tafiti mbalimbali ili kile unachoandika kiwe bora zaidi.
3. Unahitaji uvumilivu na kujituma ambayo ni rahisi kama unachofanya unakipenda.

 
Lakini mimi sijui jinsi ya kutengeneza blog.
Usiwe na wasi wasi, hiyo tayari ni rahisi, kuna kitabu kinaitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWNEYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kitabu hiki kimeeleza vizuri kwa kiswahili rahisi na kwa njia ya picha jinsi unavyoweza kutengeneza blog yako wewe mwenyewe. Huhitaji elimu ya ziada, kama umeweza kusoma hapa basi ukipata kitabu hiko unaweza kutengeneza blog yako leo.
Sijui jinsi ya kuandika na sijawahi kuandika kabisa.
Hili pia sio tatizo, hiko kitabu hapo juu kimeeleza vizuri sana jinsi ya kuandika makala nzuri na zinazovutia na kuwafanya watu kuchukua hatua. Imeelezwa kwa lugha rahisi sana, ni wewe kusoma na kuchukua hatua.
Bado sijaelewa nitafaidikaje na blog.
Usiwe na shaka, kwenye kitabu hiki utajifunza kwa undani zaidi. Utaziona fursa nyingine nyingi na kwa mifano jinsi unavyoweza kugeuza ujuzi wako au uzoefu wako kuwa sehemu ya biashara.
Napataje hiko kitabu?
Vizuri, kitabu hiki kipo kwenye soft copy yaani pdf na unaweza kusomea kwneye simu, tablet au kompyuta. Kinatumwa kwa email hivyo unaweza kukipata popote pale ulipo na kwa haraka sana.
Gharama za kitabu hiki ni tsh elfu kumi(10,000/=). Kukipata tuma fedha hiyo ya kitabu, kwa namba 0755953887(mpesa) au 0717396253(tigo pesa na airtel money) halafu tuma email yako kwenye moja ya namba hizo na utatumiwa kitabu hiko mara moja.
Asante sana, nikiwa tayari tutawasiliana.
Pole, kwa uzoefu wangu, wote waliowahi kuniambia wakiwa tayari watanitafuta hawajawahi kufanya hivyo. Kama kweli unaona njia hii inaweza kuwa bora kwako, fanya maamuzi ya kupata kitabu hiki leo hii, sio kesho au ukiwa tayari, ni leo hii na anza kukisoma, leo hii na kuchukua hatua.
Umeshapoteza muda mwingi huko nyuma hivyo ni vyema ukaanza kuchukua hatua kabla hujaendelea kupoteza muda mwingi zaidi. Kumbuka muda haukusubiri.
Nimekuelewa, ninahitaji kitabu hiko ila leo sikuwa na ratiba hii ya fedha.
Karibu sana, niandikie ni lini utakuwa umeshaweka ratiba hiyo halafu nitakupigia simu kukumbusha. Niandikie email au meseji yanye jina lako na namba ya simu na niandikie labda; TAREHE 01/11/2015 nikumbushe kuhusu kitabu hiki cha blog. Na siku hiyo ikifika nitakukumbusha.
Nakushauri sana uniandikie nikukumbushe kwa sababu unaweza kusema utakumbuka mwenyewe, ila ukisharudi kwenye changamoto zako za maisha unasahau kabisa. Nakuambia hili kwa uzoefu, watu huja kuniambia baadaye nilisahau kabisa.
Chukua hatua sasa, hapo ulipo ndio mgodi wa mafanikio yako ulipo. Na huhitaji uwekezaji mkubwa kuanza kuufaidi mgodi huo. Chukua hatua sasa.
Nakutakia kila la kheri kwenye utekelezaji wa hayo uliyojifunza.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: