Kitu Kimoja Ninachokusihi Wewe Rafiki Yangu Ufanye Kwa Mwaka Huu 2016 Ili Kuboresha Maisha Yako.

Habari za wakati huu rafiki?
Naamini mpaka kufika sasa umeshauzoea mwaka huu mpya na tayari kwa kasi sana unafanyia kazi yale malengo makubwa uliyoweka mwaka huu. Kama bado hujaanza kufanyia kazi unasubiri nini? Mwaka tayari umeshazeeka na kadiri unavyochukua hatua mapema na kukomaa ndivyo utakavyoweza kuona majibu mazuri baadae.
Rafiki yangu naweza kukuhakikishia kitu kimoja, kama utaendelea na maisha yale uliyokuwa unaishi 2015, kufanya mambo yako kwa mtindo ule ule, basi mwaka huu 2016 hautakuwa na tofauti kubwa kwako. Utapata kile ulichokuwa unapata 2015. Na kwa bahati mbaya sana utapata chini ya pale kwa sababu kwenye maisha hakuna kusimama, kuna kwenda mbele au kurudi nyuma. Na kama huendi mbele, moja kwa moja unarudi nyuma.
Ndio maana nakusihi sana wewe kama rafiki yangu uchukue hatua. Chukua hatua kwenye kile ambacho unataka kukifanya au kukipata mwaka huu 2016.
Unataka kuanza biashara? Basi anza, anza na wazo lolote, anza kidogo na utajifunza kadiri unavyoendelea kufanya. Acha kuongelea kuingia kwenye biashara na ingia kwenye biashara. Acha kufikiria ni vitu gani unakosa ndio maana huingii kwenye biashara na anza kutumia vile ambavyo unavyo sasa kuanza biashara.
Unataka kuongeza kipato chako? Anza leo, anza kwa kuongeza thamani ya kile unachotoa, iwe ni kazi au biashara au umejiajiri. Jua ni kitu gani ambacho unakitoa na ongeza thamani yake. Kipato chako kinatokana na thamani unayotoa. Kama una kipato kidogo maana yake unatoa thamani ndogo. Na ili upate kipato kikubwa anza kwa kuongeza thamani ya kile unachotoa.
Unataka kuboresha mahusiano yako na familia? Hili ni muhimu sana kwa mwaka 2016. Kwa sababu familia yako inahusika sana kwenye mafanikio yako. anza leo kufanyia kazi lengo hilo, anza leo kwa kutenga muda wa kuwa na familia yako, anza leo kujali kuhusu familia yako.
Chochote unachotaka kipo upande wa pili wa kuchukua hatua. Unaweza kuchukua hatua sasa na ukafurahia matunda baadae au unaweza kuendelea kuongelea kuchukua hatua na ukawa mtu wa maneno tu.
Mimi kama rafiki yako nakuambia kitu kimoja, chukua hatua, acha kuongelea sana ana anza kufanyia kazi. Hiyo ndiyo njia pekee ya wewe kutoka hapo ulipo sasa.
TAARIFA MUHIMU.
Kwa wale ambao wamejiunga na semina ya 2016 NI MWAKA WANGU WA MAFANIKIO MAKUBWA, leo asubuhi umetumwa ujumbe wa email wenye maelekezo kuhusu semina hii. Nenda kwenye email yako na utakuta email hiyo ya maelekezo na kisha fuata maelekezo yale.
Kama hujapata email hiyo ya maelekezo tafadhali niandikie ujumbe mara moja kwenye namba 0717396253.
TAARIFA MUHIMU ZAIDI.
Kutokana na watu wengi kuwa bado hawajachukua hatua ya kujiunga, leo natoa nafasi ya mwisho kabisa ya kujiunga na semina hii ya 2016 NI MWAKA WANGU WA MAFANIKIO MAKUBWA. Mwisho wa kujiunga ulikuwa jana lakini bado wengi wamekuwa wakituma maombi ya kujiunga.
Hivyo leo jumapili tarehe 03/01/2016 ndio siku ya mwisho kabisa ya kujiunga na semina hii.
Kujiunga tuma ada ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba 0755953887 au 0717396253 na kisha fungua maandishi haya na ujaze fomu kwa kuweka taarifa zako.
Baada ya siku ya leo hutapata tena nafasi ya kujiunga na semina hii muhimu sana kwa mwaka 2016.
Kwenye semina zilizopita, watu wengi wamekuwa wanakuja baada ya muda wa kujiunga kuisha na masomo kuanza. Tumekuwa tunawapokea lakini wamekuwa hawaendi vizuri na masomo. Kwa mwaka huu hatutafanya tena hivyo, kama utakosa nafasi hii kwa sasa itakubidi usubiri semina nyingine.
Hatutapokea mtu katikati kwa sababu semina ya sasa pia itatumia kuanza kujijengea nidhamu, na wale ambao hawataweza kwenda na kasi hii kwa siku kumi wataondolewa kwenye mafunzo haya.
Hii ni semina muhimu sana kwako kushiriki kwa sababu licha tu ya kupata mafunzo muhimu, pia utaanza kujijengea nidhamu binafsi.
Na kama bado una wasiwasi ikiwa utajifunza mambo mazuri, nakupa nafasi ya kufanya malipo, soma na kama mpaka mwisho utaona hujajifunza chochote muhimu kwako, niandikie kudai fedha uliyolipia. Nitakurejeshea fedha yako bila ya kukuuliza swali lolote. Naamini sana kile ninachokifanya kwa sababu kimenisaidia sana mimi binafsi, hivyo kama hakitakusaidia, nitakuwa tayari kukurejeshea gharama zako.
Fanya malipo na fungua hapa kuweka taarifa zako.
Nakukaribisha sana kwenye semina hii muhimu kwenye kuuanza mwaka 2016 na kuufanya mwaka wa mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: