Habari za wakati huu rafiki yangu?
Nina imani kubwa kwamba wewe rafiki yangu unaendelea kuweka juhudi ili kufanya maisha yako kuwa bora zaidi. Maana hiyo ndiyo njia pekee ya kuwa na maisha bora, siyo kusubiri, siyo kulalamika, siyo kulaumu, bali ni kufanya, kuweka juhudi, na matokeo utayaona.
Leo napenda kuchukua nafasi hii kukupa habari nzuri sana. Habari hizi ni kuhusu kuwepo kwa kundi la AMKA MTANZANIA kupitia mtandao wa TELEGRAM.
Hili ni kundi maalumu kwa marafiki zangu wote ambao ni wasomaji wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga na kundi hili hakutakuwa na gharama zozote zile, lakini pia nafasi ni chache. Telegram kwa sasa imeweka uwezo wa kundi kuchukua watu elfu tano na kuyafanya makundi kuwa bora zaidi kwa mijadala mbalimbali.
Faida za kujiunga na Kundi la AMKA MTANZANIA telegram.
1. Utapata taarifa za makala zote zinazokwenda hewani kwenye AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Utawekewa link na hivyo inakuwa rahisi kwako kusoma makala kila zinapotoka.
2. Utakuwa unatumiwa vitabu vya kujisomea bure kabisa. Telegram ina mfumo bora wa kutumiana vitabu na vitu vingine. Vitabu vyote vizuri ninavyosoma nitakuwa nawashirikisha kwenye kundi hili la telegram. Kila wiki huwa nasoma angalau vitabu viwili, na wewe utakuwa unavipata, na siyo lazima usome vyote, utachagua vile unaweza kusoma.
3. Kitabu cha mwezi kitakuwa kinatumwa kwenye telegram. Tumekuwa na utaratibu wa kutumiana kitabu cha kusoma kila mwezi. Kwa sasa kitabu hiki hakitatumwa tena kwenye email, badala yake kitatumwa kupitia telegram.
4. Nitakuwa nakushirikisha mambo mbalimbali ninayojifunza au kukutana nayo, ambayo sipati nafasi ya kuyaandikia kwa kina. Yaani hapa unakuwa umekaribia jikoni, na jikoni kuna mengi kabla ya chakula kuiva.
5. Huu ndio utakuwa mtandao wetu mzuri wa kijamii kati yangu na marafiki zangu wote. Hivyo tunaweza kuulizana na kujulishana mambo mbalimbali yahusuyo maisha ya mafanikio.
Vigezo na masharti.
Katika kundi hili, kigezo cha kujiunga na uwe msomaji wa AMKA MTANZANIA na/au KISIMA CHA MAARIFA.
Sharti ni moja tu, KITU CHOCHOTE AMBACHO HAKIFUNDISHI AU KUHAMASISHA HAKIRUHUSIWI KWENYE KUNDI HILI.
Jinsi Ya Kujiunga Na Kundi Hili.
1. Hakikisha unayo application ya telegram kwenye simu yako. Inafanana na wasap, hivyo kama simu yako ina wasap unaweza kuweka telegram. Kama huna nenda play store na search TELEGRAM, watakuletea TELEGRAM MESSENGER install hiyo application.
2. Ukishakuwa na app hiyo fungua link hii https://telegram.me/amkamtanzania au bonyeza maneno haya AMKA TELEGRAM kisha utafungua kundi na kisha bonyeza JOIN GROUP na utakuwa umejiunga.
3. Kama njia hiyo hapo juu itashindikana, save namba yangu ya simu ambayo ni 0717396253 kisha nitumie ujumbe AMKA MTANZANIA kupitia telegram na nitakuweka kwenye kundi.
Karibu sana kwenye kundi la AMKA MTANZANIA telegram na tujifunze kwa pamoja.
Kumbuka TUPO PAMOJA kuhakikisha kila mmoja wetu anakuwa na maisha bora, karibu tuwe karibu zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz