Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Amka Mtanzania? Karibu tusafiri pamoja mpaka mwisho wa makala hii ili uweze kuchota maarifa na kwenda kuboresha maisha yako.
Moja ya changamoto inayowasumbua watu wengi kutofikia mafanikio katika kazi zao, biashara, ujasiriamali, familia hata kujenga mahusiano mazuri na watu na mambo mengine ni kukosa maarifa sahihi. Dunia yetu ya leo imejaa kelele za kila aina na kama ukiwa huna maarifa sahihi katika kile unachofanya basi utapotea njia, ndio maana kusema usemi unasema miluzi mingi humpoteza mbwa. Hizi sio tena zama za mawe au zama za mapinduzi ya viwanda bali hizi ni zama za taarifa, unahitaji taarifa sahihi ili uweze kupata maarifa sahihi na hatimaye uweze kufanikiwa.
Unahitaji taarifa sahihi na maarifa sahihi ili uweze kugundua au kuziona fursa katika jamii iliyokuzunguka. Bilionea namba moja nchini uingereza bwana Richard Branson aliwahi kusema hivi fursa ziko kama mabasi au magari moja linaenda na lingine linarudi. Lakini pia ubaya wa fursa una tabia ya kuingilia mlango wa nyuma na hivyo unahitaji maarifa na uwezo wa kuona kwa jicho la tatu ili uweze kuziona fursa. Sasa ili uweze kuziona fursa katika jamii yako iliyokuzunguka unahitaji uwe na maarifa sahihi kwani bila kuwa na maarifa ni vigumu kuziona fursa kwani zina tabia ya kuingilia mlango wa nyuma.
Katika kutafuta mafanikio haitoshi kufanya kazi tu kwa bidii au juhudi tu, ili uweze kufanikiwa unahitaji vitu viwili navyo ni kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, hii ndio njia sahihi kwani dunia imebadilika unatakiwa kuendana na wakati wa sasa. Maarifa ndio njia peke ya msingi ya kukupeleka wewe kwenye mafanikio makubwa na kuachana na hali ya kufanya kitu kwa hali ya mazoea. Watu waliofanikiwa ni watu wanaopenda kujifunza kwa nidhamu ya hali ya juu kupitia kusoma vitabu, kusikiliza vitabu vilivyosomwa, kuhudhuria semina mbalimbali nk. Hivyo basi maarifa yanapatikana kwa njia ya kujifunza na katika uwekezaji kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kuwekeza katika maarifa na haitoshi kuridhika na kuwa na elimu ya darasani tu na kuona ndio kila kitu kufanya hivyo utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe na huwezi kufikia mafanikio ya hali ya juu. Unatakiwa ujifunze vitu mbalimbali ili uweze kupata maarifa ya kutosha na katika kujifunza au kutafuta maarifa hakuna kikomo, ni kama umefunga ndoa na kujifunza katika kutafuta maarifa.
Kuna usemi wa lugha ya kingereza unasema hivi ‘’ if you think education is expensive try ignorance’’ ukimaanisha hivi kama unafikiria au unadhani ya kwamba elimu ni gharama basi jaribu ujinga. Kumbe basi, katika kutafuta elimu au maarifa yoyote yale ili kufikia mafanikio lazima ukubali kulipa gharama au bei ili upate huduma unayotaka na hakuna kitu cha bure waingereza wanasema there is no free lunch, kwa hiyo, kila kitu kina gharama na hutakiwi kujiuliza wala kusita pale unapotaka kuwekeza katika maarifa kwani maarifa ndio injini ya mafanikio yako hivyo jitoe kwelikweli katika kutafuta maarifa.
Hatua ya kuchukua; kuna usemi mmoja unasema hivi ukitaka kumficha mwafrika basi kiweke kitu hicho katika maandishi. Hivyo basi, usikubali kufichwa maarifa yako kwenye kusoma vitabu, na semina mbalimbali na kujifunza kwa watu mbalimbali waliofanikiwa katika kile unachofanya.
Kwa hiyo, ndugu msomaji anza utaratibu wa kujisomea vitabu angalau kwa wiki kitabu kimoja, soma makala chanya zitakazobadili fikra yako, sikiliza vitabu vilivyosomwa, hudhuria semina mbalimbali nk. Hivyo basi, haitoshi kufanya kazi kwa juhudi bali inatosha kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Habari njema kwako rafiki na mpenzi msomaji wa amka mtanzania kuna kitabu kizuri nimekuandalia ambacho kitakusaidia wewe kupata maarifa na kufikia mafanikio na kuacha tena kufanya kazi kimazoea. Kitabu hiki kizuri kimeandikwa kwa lugha nzuri na rahisi sana ya Kiswahili kiitwacho FUNGA NDOA NA UTAJIRI na kuupa umasikini talaka. Kitabu hicho kizuri cha funga ndoa na utajiri na kuupa umasikini talaka kinapatikana kwa mfumo wa nakala tete yaani soft copy pdf ambacho unaweza kukisoma kupitia simu yako ya mkononi smart phone, kompyuta na hata tablet pia.
Kitabu cha funga ndoa na utajiri ni kitabu kizuri sana ambacho kimegusa Nyanja zote za maisha anayoishi binadamu wa sasa.
Kwanini usome kitabu cha funga ndoa na utajiri na kuupa umasikini talaka?
Sasa unapoambiwa funga ndoa na utajiri basi maana yake ni funga ndoa na mafanikio katika nyanja zote za maisha anayoishi binadamu wa sasa siyo tu mafanikio ya kifedha bali pia mafanikio mengine. Haitoshi kuwa na mafanikio ya kifedha wakati unaishi maisho ambayo hayana furaha au familia yako ni mbovu na huna mahusiano mazuri na watu kwani mwisho wa siku fedha inakua haina tena msaada kwako. Hii ndio maana nimekuandalia kitabu hiki kizuri mpenzi msomaji. Funga Ndoa na Utajiri, lugha ya kifasihi iliyosheheni uhondo wa maarifa mbalimbali ambayo ukiyatumia na kutekeleza kwa vitendo yatabadili maisha yako na kukufanya tofauti na ulivyokuwa mwanzo.
Sababu kumi (10) kwa nini usome kitabu cha Funga Ndoa na Utajiri ; Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo kati ya mengi ambayo utajifunza kupitia kitabu hiki
1. Maana ya fursa na namna ya kugundua au kusoma fursa katika jamii yako
2. Namna ya kufanya maamuzi ya kuwa mwana mafanikio
3. Namna ya kupata mtaji wa biashara
4. Namna ya kuweka akiba na kujifunza nidhamu ya fedha
5. Namna ya kujilipa kwanza wewe ( pay yourself first)
6. Namna ya kuacha kuahirisha mambo ( procrastination)
7. Utajifunza falsafa katika maisha ya binadamu na jinsi ya kuishi kulingana na falsafa hizo
8. Namna ya kugawanya mshahara wako na kukuletea mafanikio makubwa
9. Mambo muhimu ya kuzingatia katika malezi ya watoto ili kuwa na maisha mazuri na mafanikio
10. Utajifunza maadui hatari sana wanaoharibu uhusiano katika ndoa na uchumba na kujifunza nguzo za kumpata mchumba makini.
Namna ya kupata kitabu hiki kizuri cha Funga Ndoa na Utajiri;
Unatuma pesa tsh elfu tano (5,000/=) kwa mpesa 0767101504 na tigo pesa kwa namba 0717101505. Baada ya kutuma malipo tuma email yako kupitia moja ya namba ulizotumia kutuma malipo na baada ya kukamilisha malipo na kutuma email yako utatumiwa kitabu. Majina ya namba hizo ni Deogratius Kessy.
Angalizo; kitabu hiki kinauzwa kwa punguzo la bei ambalo ni maalumu kwa wasomaji wetu wa AMKA MTANZANIA. Mwisho wa punguzo hili la bei ni wiki hii. Baada ya hapo bei itaongezeka ni muhimu kuchukua hatua mapema kabla bei haijaongezeka wiki ijayo.
Hitimisho, katika dunia ya sasa ili uweze kufanikiwa unahitaji maarifa ambayo yatakusaidia wewe katika kile unachofanya hatimaye kuwa na ufanisi na kuongeza uzalishaji na kupata matokeo mazuri. Kumbuka kuwekeza katika maarifa kwani maarifa yanalipa hivyo anza kuwekeza katika maarifa.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com