Hizi Ndizo Aina Tatu (3) Za Kushindwa Katika Maisha Na Kazi.

Kushindwa kwa jambo lolote huwa hakutokei ghafla tu kama wengi wanavyofikiri, bali huchukua muda na hatua. Kama ilivyo kufanikiwa kuna hatua zake, halikadhalika kushindwa katika maisha kuna hatua au ngazi zake. Wapo ambao hushindwa katika hatua za mwanzoni kabisa katika jambo wanalolifanya na wapo pia ambao hushindwa katika hatua za kati na mwisho.
Natambua umeshawahi kushindwa katika jambo fulani kwa namna moja au nyingine. Lakini inawezekana pia hukuelewa vizuri kwa nini ulishindwa kwa jambo hilo na ulishindwa kwa ngazi ipi. Kimsingi, upo uwezekano mkubwa wa kutambua kama utashindwa kwenye jambo unalotaka kulifanya hata kabla hujalianza ikiwa utaelewa vyema ngazi hizi za kushindwa jinsi zinavyofanya kazi.
Kwa kusomamakala haya itakuonyesha aina tatu za kushindwa katika kazi na maisha yako kwa ujumla. Hivyo, kwa kujua aina tatu hizi za kushindwa itakupa urahisi kwako wa kuweza kujua kama upo kwenye ngazi mojawapo ya kushindwa au haupo na juhudi gani uweke ya kuweza kukusaidia kufanikiwa tena. Mara nyingi, ikiwa imetokea upo hata kwenye ngazi mojawapo ya kushindwa inakuwa ni ngumu sana kufanikiwa.
Hebu twende pamoja tuangazie hatua ama aina kadhaa za kushindwa, jinsi zinavyotokea katika maisha na jinsi ya kukabiliana nazo.
1. Kushindwa katika maono (Vision)
Kufanikiwa kwa kitu unachokifanya kunakuja kutokana na maono ama ‘vision’ uliyonayo. Huwezi kufanikiwa kwa viwango vya juu kama huna maono. Hebu jaribu kuangalia watu waliofanikiwa sana utakuta ndani yao wana maono au ‘vision’ kubwa sana kwa kile kitu wanachokifanya. Kwa kila wanachokifanya wanajua kitawafikisha wapi baada ya muda fulani.
Unatakiwa kujua hili na kujiwekea maono yako ili usiweze kushindwa. Ni lazima ujue baada ya miaka mitatu mbele au mitano utakuwa wapi. Sasa watu mara nyingi hushindwa katika maisha kwa sababu ya kukosa maono yanayotakiwa kusaidia kufanikiwa. Kwa hiyo kama huna maono elewa kabisa  huwezi kufanikiwa hata ufanye kitu gani.
Kuwa na maono sahihi ili ufanikiwe.
Kitu cha kufanya.
Kuwa na maono katika maisha ni jambo la lazima sana. Viongozi wote na watu wenye mafanikio makubwa ni watu wa maono. Bila kuwa na maono inakuwa sio rahisi sana kuweza kufanikiwa katika jambo lako. Weka mikakati ya kujiwekea maono katika maisha yako bila kuacha.
2. Kushindwa katika mipango.
Kuna watu wanashindwa katika maisha si kwa sbabu hawana pesa bali ni kwa sababu hawana mipango mizuri ya kuwasaidia kuwafanikisha. Jaribu kujiuliza wale ambao huwa wanapata pesa za bahati nasibu, ni kitu gani ambacho huwafanya kushindwa? Hakuna sababu nyingine zaidi ya kutokuwa na mipango mizuri ya kufanikiwa kwao.
Unaposhindwa katika mipango. Unaposhindwa kujua ni kitu gani ufanye ni wazi lazima utashindwa. Watu ambao hawana mipango mara nyingi utawaona hata kwenye matendo yao . Hawa huwa ni watu wa kuuliza vitu au mambo ya kufanya bila utekelezaji. Matokeo makubwa ya kutokuwa na mipango huwapelekea wao kushindwa kwenye maisha na kazi.
Kitu cha kufanya.
Ni lazima ujiwekee mipango imara ya kukusaidia kufanikiwa. Ni lazima ujue mapema ni kitu gani kwako unachotakiwa ukifanye hata kabla pesa au mtaji hujafika mikononi mwako. Ukifanya hivi utaepukana na aina hii yakushindwa.
3.Kushindwa katika mbinu.
Unaweza ukawa una mipango mizuri na umeshajua ni kitu cha kufanya, lakini ukashindwa katika suala zima la kuwa na mbinu sahihi. Wapo watu ambao hatua hii huwa kwamisha pia. Kwa mfano unaweza ukawa umeanzisha mradi wako vizuri, lakini je, unazo njia au mbinu sahihi pengine za kuweza kukabiliana na soko hadi kuweza kufanikiwa?
Kama huna njia au mbinu nzuri za kukabiliana na soko ni lazima utashindwa katika kile unachokifanya. Wengi kutokana na kukosa au kuishiwa mbinu, hapa ndipo huanza kulaumu na kufikiri wamelongwa. Hili unaweza ukalifananisha na timu ya mpira. Inaweza ikaingia uwanjani ina mipango mizuri, lakini mbinu zikikosekana za kitaalamu uwanjani haiwezi kushinda. Na maisha yako hivyo hivyo bila mbinu sahihi, hakuna matokeo ya ushindi.
Kitu cha kufanya.
Ili uweze kushinda mchezo wa maisha ni lazima uwe na mbinu sahihi za kukuwezesha kushinda. Bila kuwa na mbinu hizo utashindwa kuwa mshindi katika maisha yako karibu kila siku.
Kwa kuhitimisha makala haya nimalizie kwa kusema hivi, kabla hujashindwa katika jambo lolote tambua zipo ngazi zake za kushindwa kwako. Kitu cha kufanya jiulize wewe binafsi umeshindwa katika ngazi ipi? Je, umeshindwa katika ngazi ya kukosa maono(Vision)  au umeshindwa katika ngazi ya kukosa mipango na mbinu? Baada ya hapo chukua hatua ya kubadili hali yako.
Tunakutakia kila la kheri katika safari ya maisha yako na endelea kujifunza kupitia AMKA MTANZANIA kila siku.
Kwa makala zaidi za mafanikio pia hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: