Jinsi Unavyoweza Kufanya Maisha Yako Yakawa Ya Mafanikio Tena.

Kipo kipindi katika maisha yako, ambapo kutokana na changamoto za hapa na pale, ni rahisi kuona kila kitu umepoteza na huwezi kufanikiwa tena.
Hiki ni kipindi ambacho huwaweka wengi sana njia panda ya kimaisha na kushindwa kujua sasa wafanye nini?
Unapokutana na hali kama hii,elewa kabisa ipo namna unavyoweza kufanya maisha yako yakawa ya mafanikio tena. Huna haja ya kuendelea kukata tamaa.
Kivipi hili linawezekana? Hebu fuatana nami katika makala haya, kujifunza jinsi unavyoweza kufanya maisha yako yakawa ya mafanikio tena.
1. Acha kulalamika tena au kulalamikia hali yoyote katika maisha yako. Sasa wajibika na kubali kuchukua hatua. Kulalamika hakutakusaidia kitu.
2. Fanya kila siku, kitu cha kukusogeza kwenye ndoto yako. Usiache hata siku moja ikapita bila kufanya jambo la kukusogeza kwenye ndoto yako.
3. Endelea kufanya jambo unalolifanya sasa hata kama halikupi matokeo ya haraka. Kuna wakati matokeo yanachelewa kufika. Hivyo usikate tamaa mapema sana.
4. Jifunze kuwekeza, hata kama ni kitu kidogo, wewe wekeza. Acha kuishi maisha ya kiholela. Usiishie kulalamika tu, wekeza na utavuna mafanikio.
5. Anza kufanya mambo yale ambayo ulikuwa umeahirisha kwa muda mrefu. Wakati wako wa kufanya ni sasa na si kusubiri kesho au siku nyingine.
6. Tengeneza maisha yako kwa kuyawekea vipaumbele. Bila kuweka vipaumbele, itakusumbua sana kufikia mafanikio yako.
7. Andika malengo yako muhimu unayotaka kuyatimiza, kisha baada ya hapo yafanyie kazi kila siku mpaka, uone ndoto yako inatimia.
8. Kuwa jasiri katika kutekeleza ndoto zako, ondoa hofu na woga. Najua zipo changamoto nyingi katika maisha, lakini zikabili kwa ujasiri.
9. Fanya kazi kwa juhudi zako zote kwa jinsi utakavyoweza. Ipo wazi kabisa njia kubwa ya kukutoa kwenye umaskini ni kufanya kazi bidii zote.
10. Tupa kila kitu ambacho unakiona kinakurudisha nyuma kwenye safari yako ya mafanikio. Tupa marafiki, tupa mawazo mabovu na tupa kila aina ya takataka ambayo unaona inakuzuia kufikia mafanikio yako.
11. Tumia na tunza muda wako vizuri kila wakati. Muda huo utakusaidia wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa sana.
12. Amua kujifunza na kuchukua hatua kila siku. Maisha yako hayawezi kubadilika, ikiwa eti utaamua kubaki hivyo kama wewe na kukataa kujifunza.
Kwa kuhitimisha, hayo ndiyo mambo unaweza kuyafanya na yakakusaidia kwa sehemu kubadili maisha yako.
Nikutake siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa.
Endelea kutembelea www.amkamtanzania.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s