Habari za leo rafiki?

Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA KOCHA ambapo tunakwenda kushirikishana maarifa muhimu kwa maisha yetu ya mafanikio. Kupitia kipindi hichi nakushirikisha mbinu na hatua za kuchukua ili kuhakikisha unafika kule ambapo unataka kufika.

Katika kipindi cha leo nimezungumzia kukatishwa tamaa na watu wa karibu, maana hii ndiyo sumu kali na hatari sana kwa mafanikio ya mtu yeyote yule. Watu wa karibu kwako ni watu ambao unawaamini sana, ni watu ambao mmefanya mengi kwa pamoja. Wanapotoa maoni yao juu ya unachofanya, unawasikiliza zaidi hata kama hawapo sahihi.

Na hii ndiyo inakuwa changamoto kubwa pale wanapokukatisha tamaa, kwa sababu ni watu unaowaamini, unakubaliana nao na kuacha kile ambacho ulipanga kufanya. Lakini mara nyingi watu hawa hawapo sahihi kwenye kile wanachotuambia. Na mara nyingi zaidi, kuna hisia zinakuwa zimewaingia hivyo kufanya ushauri wao au kukatisha kwao tamaa kusiwe sahihi.

Katika kipindi cha leo, nimekushirikisha hatua tatu muhimu za wewe kuchukua pale unapokatishwa tamaa. Hatua hizi zitakupa njia ya kusonga mbele licha ya kukatishwa tamaa. Pia nimekupa hatua nyingine moja ya ziada ya kuhakikisha unajifunza kupitia kile ambacho wengine wanakukatisha tamaa ili uweze kufanikiwa.

Nakusihi sana rafiki yangu, angalia kipindi hichi cha leo, kwa sababu wengi wanaishia kuzika ndoto zao kwa sababu ya wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu ambao wanawakatisha tamaa.

Moja ya vitu nitakavyokueleza kitakushangaza sana, hasa kwenye sababu halisi kwa nini watu wanakukatisha tamaa. Utaona ni kwa namna gani kinachowafanya wakukatishe tamaa siyo wewe, bali wao wenyewe. Hawataki wewe ufanye ili wao wasiumie.

Angalia kipindi hichi kizuri kwa kubonyeza maandishi haya.

Kama kifaa chako kinaruhusu, unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Haya ambayo unajifunza rafiki, yafanyie kazi ili uweze kupiga hatua.

Kuangalia vipindi vingine vya video tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/video

Kusikiliza vipindi vya sauti tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/podcast

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.