Habari za leo rafiki?

Umewahi kupanga vizuri kabisa namna ambavyo utachukua hatua ili kuboresha maisha yako? Namna ambavyo itaanza biashara yako? Au namna utakavyoanza kilimo ili uweze kujikwamua kimaisha? Unaanza kweli lakini unapata matokeo ya tofauti kabisa na ulivyotegemea. Na hapo umefanya kila kitu kwa usahihi kabisa, kama ambavyo ulipaswa kufanya, au wengine wanavyofanya, lakini wewe ukashindwa kupata matokeo bora! Je katika hali kama hii unajiona una bahati mbaya? Unajiona kama wewe ndiyo wa fungu la kukosa?

Leo nataka nikupe siri, siri hii ni ukweli wa wazi ambao wengi hawakuwahi kuung’amua kwenye maisha yao. Hivyo wamekuwa wanajaribu kila kitu, lakini hawapati matokeo wanayotaka wao.

Ukweli ni kwamba, kazi ya kwanza ya dunia, ni kukuzuia wewe kufanikiwa. Ni jambo la kushangaza, na hakuna anayejua kwa nini, ila ukweli ndivyo ulivyo. Kwamba kazi ya kwanza kabisa ya dunia ni kuhakikisha wewe hufanikiwi, ni kuhakikisha kama unajaribu jaribu tu inakukomesha. Kama unaanza biashara kwa kujaribu jaribu, bila ya kujitoa kweli, inahakikisha inakupa hasara nzuri tu ili ukimbie.

Hii ni siri nzito sana ambayo kwa kuijua, hutakuja kushindwa jambo lolote kwenye maisha yako hapa duniani, kwa sababu utaanza jambo lolote lile ukijua siyo majaribu, bali ni kujitoa kweli, kuweka juhudi kweli ili kuweza kupata unachotaka. Na hata unapofanya kila kitu, bado siyo uhakika wa wewe kupata chochote unachotaka.

Katika somo letu la leo la ONGEA NA KOCHA, nimekushirikisha siri hii kwa undani na hatua ambazo wewe unaweza kuchukua ili kufanikiwa. Hatua nilizokushirikisha hapa, ukizitumia kwa usahihi, dunia itakunyooshea mikono, na kusema huyu ameshindikana, tumwache aende zake, na hapo ndipo unayapata mafanikio mpaka unashangaa yalikuwa yamejificha wapi muda wote. Hapa ni pale dunia inapokuchoka na kusema haya chukua, wasioelewa ulikopitia watasema una bahati, lakini ukweli unaujua wewe mwenyewe.

Nisikuambie mengi hapa, bali bonyeza maandishi haya kuangalia somo hili na kujifunza siri hii kwa undani. Au unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Nina imani kwa somo hili la leo, utaondoka na maarifa sahihi ya mapambano, na kwenda kupambana hasa ili ufanikiwe. Kikubwa rafiki yangu, chukua hatua.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.