Niambie kama umewahi kukutana na hali kama hii;

Ndugu au rafiki yako wa karibu, ambaye mnaheshimiana sana na kushirikiana mambo mengi, anakupigia simu. Anakuambia kuna fursa nzuri sana ya kibiashara anataka mjadili kwa pamoja. Anakuambia ni fursa itakayokuwezesha kuuaga umasikini kabisa. Unahamasika, unamwambia akueleze kwa simu, anakuambia hapana, mpaka muonane ana kwa ana. Unahamasika zaidi, unaacha mambo yako na kupanga mnaonanaje.

Mnapanga kuonana, anakueleza fursa hiyo nzuri ya kibiashara, ambapo kuna bidhaa ambazo unatumia na kuwaambia wengine pia watumie na wajiunge. Anatumia karatasi na kalamu kukuonesha, kwamba ukiwaunganisha watu watano, unapata milioni, wale watano nao wakiunganisha watano, unapata zaidi. Na wale watano walioletwa na watano, wakileta watu watano, unapata mamilioni zaidi. 
 

Huh unahamasika, unaona utajiri huu hapa, umasikini baibai. Unaingia kwneye biashara, unahudhuria mafunzo, unapewa hamasa zaidi, unaoneshwa wengine ambao nao wamepata mamilioni hasa kupitia biashara hiyo. Unajiunga na kupata bidhaa zako, kazi sasa inakuwa kwako, kwenda kuwapata watu wa kujiunga na biashara hiyo.

Na wewe kwa hamasa uliyonayo, unaanza kuwapigia simu ndugu na marafiki zako, kuwapa fursa hiyo kubwa ya kibiashara. Unakutana nao, lakini unapowaambia wanakuambia aah, umetapeliwa, au huwezi biashara hiyo, au utakuwa machinga na mengine. Baada ya watu watano kukuambia hivyo, hamasa yote inazima, unaamua kuachana na biashara hiyo.

Sema ndiyo kama umewahi kupitia hali kama hiyo, au hata sehemu tu.

Wengi ninaowajua wamepitia hali hiyo,

Mimi binafsi nimepitia hali hiyo siku za nyuma.

Mpaka pale nilipokaa chini na kusema hebu nipate ukweli hasa wa hichi kitu kinaitwa BIASHARA YA MTANDAO, au NETWORK MARKETING. Hapo ndipo nilikutana na ukweli ambao sikuwahi kuambiwa wakati nashawishiwa kujiunga. Nilikuwa na hata wewe umekuwa unaelezwa upande mmoja tu, ule upande wa mamilioni ya fedha, na yanakuhamasisha.

Kumbe upo upande mwingine muhimu sana wa biashara hii ambao kwa kuuelewa, basi utaweza kuifanya vizuri na ukanufaika na vingi kabla hata hujayafikiria mamilioni unayoambiwa. Nilijifunza mengi ambao wengi hawaambiwi.

Na kwa kuwa naona bado watu wanadanganywa, na kupotezewa muda na fedha zao, nimekaa chini na kuandika kitabu kinaitwa IJUE BIASHARA YA MTANDAO. Kitabu hichi nimekupa misingi yote muhimu unayopaswa kuijua kwenye biashara hii. Kuanzia mifumo ya malipo kwenye hizi biashara, kujenga timu imara na hata kunufaika na mengine mengi, zaidi ya kumi, ukiondoa fedha pekee.

Kuna makampuni mengi sasa yanayofanya biashara kwa njia hii, kuchagua tu ni changamoto. Kupitia kitabu hichi, nimekupa vigezo KUMI vya kutumia kuchagua kampuni itakayokufaa wewe.

Na kwa kuwa kumekuwa na biashara nyingi za utapeli zinazoenda kwa jina la BIASHARA YA MTANDAO, nimekupa njia KUMI za kutofautisha biashara halisi ya mtandao na michezo hiyo ya utapeli. Kwa kusoma kitabu hichi, hutakuja kudanganywa KAMWE.

Hata kama huna mpango wa kufanya biashara hii, kuna misingi muhimu nimekushirikisha, ambapo unaweza kutumia dhana hii kukuza biashara yako ya kawaida. Pia zipo bidhaa nzuri unazoweza kutumia wewe mwenyewe na ukanufaika, hata kama hutauza na kuunganisha wengine.

Hivyo ninachokuambia ni hichi rafiki yangu, soma kitabu; IJUE BIASHARA YA MTANDAO, utapata maarifa sahihi ya biashara hii.

Kitabu kitatoka tarehe 01/06/2017, na kitakuwa kwenye mfumo wa nakala tete. Lakini nakupa fursa kubwa ya kukipata kwa urahisi zaidi, iwapo utafungua kiungo hichi na kuweka email yako. Hivyo fungua; https://goo.gl/1YXp4q na weka taarifa zako. Utapata kitabu hichi kwa punguzo kubwa.

Karibu sana upate maarifa sahihi kupitia kitabu hichi cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO.

Rafiki na kocha wako,

Makirita Amani.

N;B Usisahau kufungua kiungo hichi kupata kitabu; https://goo.gl/1YXp4q