Habari rafiki?

Sheria ya asili inasema kila mtu anavuna kile alichopanda, na hiyo ipo wazi kwenye kila jambo tunalofanya kwenye maisha. Matokeo unayopata sasa ni kutokana na vitu ulivyofanya huko nyuma.

Kwenye kipato sheria hii iko vizuri kabisa, kipato chako ni matokeo ya juhudi unazokuwa umeweka, ujuzi ulionao kwenye kazi hiyo, uzoefu na mengine mengi. Yote hayo unakuwa umewekeza na baadaye yanachangia kwenye kipato chako.

Kadhalika, kwenye kutengeneza fedha kwenye mtandao wa intaneti, kuna uwekezaji ambao lazima ufanye. Wengi wamekuwa wanakimbilia fursa hii wakifikiri ni njia ya kutajirika haraka, ni mpaka wanapofanya ndiyo wanagundua kwamba hawakujipanga vizuri, mwishowe wanakimbia.

Ili wewe rafiki yangu usiishie njiani kama wengi, nimekuandalia somo la VITU VIWILI MUHIMU unavyopaswa kuwekeza ili uweze kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti.

Ninachoweza kusema kwako rafiki ni kwamba, kama hutawekeza vitu hivi viwili, ni bora usijisumbue kuingia kwenye biashara hii. Na habari njema kabisa ni kwamba vitu hivi ni rahisi sana kuwekeza, havihitaji uwe na elimu kubwa au uzoefu wowote.

Angalia somo hili la leo kujifunza kwa kina vitu hivi viwili. Unaweza kuangalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya, au ukaangalia moja kwa moja hapo chini.

Tumia mtandao wa intaneti kwa manufaa, uweze kujenga biashara yako, jina lako na hata kutengeneza kipato chako. Iwapo unahitaji ushauri zaidi kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao, tuwasiliane kwa njia ya wasap 0717396253. Karibu sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.