Tofauti Hizi Ndogo Ndizo Zinakufanya Ushindwe Au Ufanikiwe Kwenye Maisha Yako.

Yapo matokeo ambayo katika maisha yako wewe huwezi kuyaona hapo hapo, wala mwingine pia hawezi kuyaona kwako. Kwa mfano, unaposoma kitabu huwezi kuona matokeo yake leo au kesho, inachukua muda fulani.

Kwa hiyo unaona kama yapo matokeo ambayo huwezi kuyaona moja kwa moja, hapa ndipo unapotakiwa kuwa mwangalifu sana hata na maamuzi yako yote hasa katika vile unavyovifanya katika maisha yako.

Utake usitake, maamuzi yoyote yatakupa matunda au matokeo hata kama ni kidogo sana. Hapa sasa ndipo unapotakiwa ujue mafanikio kama mafanikio yanajengwa kwenye mstari mwembamba sana ambao wengi wanashindwa kuuona.

Walioshindwa

Tofauti ya tajiri na maskini ndipo huanza kujitokeza, kwa mfano matajiri hujali sana kupata matokeo yasiyoonekana, tofauti na watu maskini ambao wao hutaka papo kwa papo, hutaka mambo yaonekane tu tena wakati mwingine kwa haraka.

Kuwa makini sana na mambo unayoyafanya, kila jambo lifanye kwa faida. Ili ukianza kuvuna matokeo usiyoyaona miaka kumi ijayo usije ukashikwa na mshangao, kwamba ‘alaa hivi kumbe nilikosea wapi.’

Ndio maana tunasema hivi hata yale maamuzi unayoyafanya leo, yale mambo madogo unayoyafanya leo na unaona hayana uwezo wa kuathiri maisha yako kesho, kesho kutwa au mwakani, ila matokeo ya mambo hayo au maamuzi yako unaweza ukaanza kuyaona hata baada ya miaka mitatu, miaka mitano au hata zaidi ya hapo kabisa.

SOMA; Uongo Mkubwa Unaojidanganya Kila Siku Na Unakupotezea Mafanikio Yako Kabisa.

Kila wakati kuwa makini na maamuzi yako, kuwa na maamuzi ya busara. Kama utakuwa na maamuzi mabovu usishangae ukaja kukuta maisha yako tayari yameshaharibika na itakuwa ngumu sana kwako kuanza upya kurekebisha kwani itachukua muda pia.

Hakuna wa kukufanya ushindwe au kukuonea kwenye maisha yako. Kila kitu unacho wewe. Tambua kabisa yapo matokeo yasiyoonekana leo kwenye maisha yako, angalia matokeo hayo yasiweze kukupoteza.

Chunga matumizi yako ya pesa, angalia uhusiano wako na watu wengine, fanya kila unavyoweza kufanya kila kitu kiwe kwa ubora kwako hata kama huna matokeo yasiyoonekana. Matokeo hayo ipo siku yataonekana na yatakuwa nje.

Sasa usije ukawa miongoni mwa wale watakao lia na kujilaumu kwa sababu ya kuvuna matokeo mabovu, ya mambo ambayo hawakutarajia yatakuja kuonekana. Fanya vitu vyenye maana, upate matokeo yanayoonekana mbeleni.

Vile vitu vidogo vidogo sana ambavyo huvichukulii umakini au tahadhari yoyote, hivyo ndivyo vinavyoleta tofauti ya maisha kati ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Kushindwa au kufanikiwa kwako kunatengenezwa na tofauti hizi ndogo.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

One thought on “Tofauti Hizi Ndogo Ndizo Zinakufanya Ushindwe Au Ufanikiwe Kwenye Maisha Yako.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: