Habari rafiki?
Karibu kwenye utaratibu wetu wa kujisomea kitabu kimoja kila mwezi.
Kila mwezi nakupendekezea kitabu kizuri cha kusoma. Mapendekezo haya ni kwenye maeneo muhimu ya maisha yetu kama kazi, biashara, fedha, mahusiano, afya, imani, mawasiliano na uongozi.
Ninaamini sana kwenye usomaji wa vitabu, kwa sababu hatua yoyote niliyoweza kupiga kwenye maisha yangu, kwa sehemu kubwa imechangiwa na maarifa ambayo nimekuwa napata kwenye usomaji wa vitabu.
Vitabu nitakavyokuwa napendekeza kila mwezi huenda kuna ambavyo ulishasoma, lakini nitakushauri uvisome tena, kwa sababu kwa uzoefu wangu, kitabu huwa hakisomwi mara moja, unapaswa kukisoma tena na tena na tena.
Pamoja na umuhimu mkubwa wa kusoma vitabu, bado wengi wetu wanashindwa kusoma vitabu kwa sababu mbalimbali. Lakini kubwa zaidi ni kukosa muda. Wengi wamebanwa na kazi au biashara zao kiasi cha kushindwa kabisa kupata muda wa kusoma vitabu.
Na hapo ndipo mimi nakuja na msaada, wa kukuwezesha wewe kujenga nidhamu ya kusoma kitabu kimoja kila mwezi.
Hapa nimekuja na PROGRAM maalumu ya kusoma vitabu, ambapo kila siku mtu unasoma kurasa kumi pekee. Na kushirikisha chochote kidogo ulichojifunza, ambacho unakwenda kufanyia kazi.
Hata kama umebanwa kiasi gani, huwezi kukosa dakika 10 mpaka 20 za kusoma kitabu kila siku.
Na njia bora ya kufanya hivyo ni kugawa usomaji wako wa kitabu katika mafungu matatu, asubuhi dakika tano mpaka kumi unapoamka, mchana unapopumzika au kula, na jioni kabla ya kulala.
Katika program hii ya kusoma kurasa 10 za kitabu kila siku, utaweza kujijengea nidhamu nzuri ya kusoma vitabu na hata kufanya vitu vingine kama mazoezi, tahajudi na kadhalika.
KITABU CHA MWEZI OKTOBA 2017.
Mwezi huu wa kumi wa mwaka 2017 napendekeza usome kitabu YOU WERE BORN RICH kilichoandikwa na BOB PROCTOR.
Bob Proctor ni mmoja wa watu ambao wameisoma saikolojia ya fedha na kila kitu kinachohusu fedha kuanzia fikra zetu, matendo yetu na hata tabia zetu.
Kwa yote hayo, alifikia hitimisho kwamba kila mtu anazaliwa akiwa tajiri, lakini baada ya kuzaliwa, jamii inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watu wengi wanakuwa masikini.
Ni mara ngapi umesikia kauli kwamba matajiri ni watu wabaya? Au fedha ndiyo chanzo cha maovu?
Je umewahi kumwona mtu ambaye amekuzidi fedha na ukajiambia kwamba hana raha kama wewe ambaye huna fedha nyingi?
Au ukaona mwenzako amepiga hatua na ukaamini ametumia uchawi au njia za kishirikina kupata fedha hizo?
Je umekuwa unafanya kazi lakini mishahara haikutani? Yaani ukipokea mshahara unalipa madeni, halafu unakopa tena na kusubiri mshahara utoke ulipe?
Je unafanya biashara ambayo unachopata ni fedha ya kula pekee? Biashara ipo pale pale, vile vile haipigi hatua?
Kama umesema ndiyo kwenye swali lolote hapo juu, basi unamhitaji sana Bob Proctor, kwa sababu ana majibu sahihi ya hayo unayopitia.
Na majibu hayo yanaanzia kwenye kutibu fikra zako linapokuja swala la fedha. Ukishatibu fikra, unafungua mifereji ya kifedha kiasi kwamba unaweza kujiuliza ulikuwa wapi muda wote usijue hayo yote.
Soma kitabu hichi kwa mwezi huu wa kumi, kila siku soma kurasa kumi tu, na utakimaliza ndani ya siku 25 kwa sababu kina kurasa 240 hivi.
Pata kitabu hichi ukisome, unaweza kukitafuta bookshops kama unapenda hadcopy.
Kama unaweza kusoma softcopy, kwenye simu, tablet au kompyuta yako, karibu kwenye program ya kusoma kurasa kumi kila siku, utakipata bure.
Nakutakia kila la kheri katika usomaji wa kitabu hichi, fanyia kazi yale unayojifunza ili maisha yako yaendelee kuwa bora zaidi.
MUHIMU;
- Kama unapenda kujiunga na program ya KUSOMA KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0755 953 887 wenye maneno KURASA KUMI ZA KITABU, nitakupa maelekezo ya kujiunga na utaweza kupata kitabu hicho ukishajiunga.
- Kama changamoto kwako ni lugha, huwezi kusoma vitabu hivi vya kiingereza, usiwe na taabu, tembelea duka la vitabu popote ulipo, au tembelea maktaba ya karibu na ulipo, kisha chagua kitabu chochote kinachohusu fedha na kisome kwa mwezi huu wa kumi. Kama utajiunga kwenye program ya kusoma kurasa 10 kila siku, nitaweza kukushauri kitabu gani usome kati ya vile utakutana navyo.
- Kama una kasi kubwa ya kusoma, kama unaweza kusoma vitabu viwili kwa wiki, tuna kundi maalumu la usomaji kwa wingi linaloitwa TANZANIA VORACIOUS READERS, unaweza kujiunga lakini hakikisha unaweza kusoma sana kwa sababu sheria za ndani ya kundi hili ni kali, kama husomi unaondolewa. Kama ungependa kujiunga wasiliana na mwenyekiti wa kikundi Deo Kessy kwa njia ya telegram namba 0717 101 505. Uwe unaweza kusoma vitabu vya kiingereza na uweze kusoma siyo chini ya kitabu kimoja kwa wiki, na kuandika mambo 20 uliyojifunza kwenye kitabu ulichosoma.
Kama kuna sehemu moja ambayo uchawi wa maisha bora, ya furaha na mafanikio umefichwa, ni kwenye maandishi. Kama huamini anza kusoma, na fanyia kazi yale unayojifunza, utaona watu wataanza kusema kuna kitu unatumia, au kuna mbinu za siri unazo. Kumbe ni usomaji wako.
Karibu tusome vitabu, karibu kwenye kusoma KURASA 10 ZA KITABU KILA SIKU, tuma ujumbe kwa wasap 0755 953 887.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog