Kikawaida, kama wewe ndiyo kwa mara ya kwanza unataka kukimbia mbio za mita mia nane na hujawahi kufanya hivyo, huwezi kukimbia mbio hizo kwa mara moja hata ufanyaje, badala yake ili zoezi hilo uliweze utatatikiwa kwanza uanze kukimbia mbio fupi ili zikusaidie kukimbi mita ndefu.

Pia kama umeenda ‘gym’ na unataka kunyanyua chuma chenye uzito wa kilo 250 na hujawahi kufanya hivyo awali, pia hutaweza kunyanyua chuma hicho, badala yake unatakiwa anze kunyanyua vyuma vidogo vidogo vya kilo 10, 15, 25 au 50 ili vikupe ukomavu wa kubeba vyuma ya kilo 250.

Hivyo ndivyo misuli ya kukimbia na misuli ya kubeba vyuma vizito inavyojengwa. Misuli hiyo inajengwa kwa kuanza kidogo kidogo na mwisho wa siku kujikuta wewe ni mkimbiaji maarufu au wewe ni mbeba vyuma mkubwa ambaye kila mtu akikuangalia anakushangaa ni kushindwa kuamini.

Vichocheo Saba Vinavyowasha Moto Wa Mafanikio Kwenye Jambo Lolote Lile.

Kama ilivyo kwenye kukimbia unaanza na kujenga misuli kidogo kidigo inayokuwezesha kukimbua mbio ndefu au kama ilivyo kwenye kunyayua vyuma kwa kuanza kunyanyua vyuma vidogo ndcvyo vitakavyokusaidaia kunyanyua au kubeba vyuma vikumbwa na vizito zaidi na swala zima la kufanikisha jambo lolote liko hivyo.

SOMA; Mambo 6 Unayotakiwa Kuyajua, Ili Kujenga Mtazamo Chanya Katika Maisha Yako.

Mara nyingi kwa jinsi ilivyo, huwezi kufanikiwa jambo lolote kubwa bila kuanza na kidogo. Lazima ujenge misuli ya mafanikio madogo kwanza na hiyo misuli ikue na ikuwezeshe kupata mafanikio makubwa. Kwa jinsi unavyoendelea kupata ushindi katika mafanikio madogo, ushindi huo ni muhimu sana kuweza kukupeleka kwenye mafanikio makubwa.

Ndiyo maana sio rahisi sana kuweza kufanikiwa kwenye mafanikio makubwa kama hukuwahi kuanza na kufanikiwa kwa kwa kidogo, kama utafanikiwa kwa ‘staili’ hio basi hata kuanguka tena ikitokea usishangae, hiyo yote ni kwa sababu unakuwa hauna pumzi au ‘stamina’ kubwa ya kukuwezesha kusonga mbele zaidi kimafanikio.

Kwa hiyo kwa vyovyote vile iwavyo unatakiwa kujenga misuli mkubwa ya mafanikio, lazima uwe na misuli imara ya mafanikio kwani misuli hiyo ndiyo itakayokusaidia kuweza kufanikiwa. Ni jukumu lako kila siku kujenga na kukomaza misuli ya mafanikio kwa kuhakikisha kila siku unapata angalau ushindi hata mdogo utakaokusaidia kusonga mbele.

Hivyo kila siku kabla siku yako haijaisha, angalia ushindi ambao umeupata, ushindi huo ni nguzo au misili bora kwako ya kukusaidia kuweza kufanikiwa zaidi na zaidi. Huhitji kusita sita ni jukumu lako kuchukua hatua ya kuweza kusonga mbele kwa kukuuza misuli yako ya mafanikio kwa kuhakikisha kila siku unakuwa mshindi kwenye mambo fulani.

Fanyia kazi haya na tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea http://www.amkamtanzania.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com