Habari za leo rafiki yangu?

Ipo kauli moja ambayo imekuwa inawapoteza watu wengi sana kila mwaka, hasa mwanzoni mwa mwaka.

Kauli hiyo ni MWAKA MPYA MAMBO MAPYA.

Mwanzo wa mwaka wowote, watu huwa na hamasa kubwa ya kuuona mwaka. Na watu hufikiri kwamba kubadilika kwa mwaka basi ni kubadilika kwa maisha yao.

Hivyo huwa na matarajio makubwa kwa mwaka mpya, lakini siku chache zinapopita, wanakuwa wamerudi kwenye maisha yao ya awali na kusahau kabisa kwamba mwaka huo walikuwa na hamasa kubwa.

Kwa mfano nikikuuliza sasa kwamba mwaka 2017 kipi kikubwa umefanikisha, wengi, hasa wale ambao hawapo kwenye KISIMA CHA MAARIFA hawana kikubwa cha kuonesha.

Nasema hivi kwa sababu watu ambao wamekuwa wakiniandikia kuomba ushauri au msaada wa mawazo, ninapowauliza hatua ipi wamepiga wanakuwa hawana hatua waliyopiga kabisa.

Sasa jukumu langu kwako, ambalo nimejipa kwenye maisha yangu, ni kuhakikisha kila anayekutana na mimi kwa nia yoyote ile, anaondoka na maarifa na mbinu bora kabisa za kuyafanya maisha yake kuwa bora. Mtu asibaki kama alivyokuwa awali.

Na katika hili ndiyo ninataka nikusaidie usipoteze mwaka 2018 kama ambavyo wengi wamepoteza mwaka 2017, wale wanaosubiri uishe ili waanze mwaka mwingine wakiwa wamejipanga vizuri zaidi.

Habari moja muhimu kwako ni kwamba, huhitaji kusubiri mpaka tarehe isome 2018 ndiyo uanze kuchukua hatua, unahitaji kuchukua hatua sasa, na kama hujui wapi pa kuanzia, na hatua zipi za kupiga, nipo hapa kwa ajili yako.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye mwezi disemba 2017 ambao unaweza kuutumia kujipanga vyema na kuanza kuufaidi mwaka 2018 wakati wengine bado wapo kwenye usingizi wa kusubiri sikukuu za mwisho wa mwaka 2017 ziishe, halafu mwanzo wa mwaka 2018 waseme januari ngumu kweli.

Usomaji

Mwezi huu wa disemba natoa huduma zifuatazo;

Moja; MAKALA NA TAFAKARI.

Makala za kila siku kwenye www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz zinaendelea kama kawaida. Pia kundi letu la mafunzo la wasap la KISIMA CHA MAARIFA mafunzo yanaendelea kila siku.

Kusoma makala kwenye AMKA MTANZANIA ni bure kabisa kila siku. Ila kwenye KISIMA CHA MAARIFA unahitaji kulipa ada, nitatoa maelezo zaidi mwishoni.

Mbili; KITABU CHA MWEZI DISEMBA.

Kesho nitakutumia mapendekezo ya kitabu cha kusoma kwa mwezi disemba 2017. Na njia bora kabisa ya kusoma kitabu hichi ni kusoma KURASA KUMI KILA SIKU.

Njia hii itakuwezesha kumaliza kitabu kimoja kwa mwezi hata kama umekwama kiasi gani. Lipo kundi maalumu la wasap linalohusu kusoma KURASA KUMI KILA SIKU, ambalo ada ya kujiunga ni elfu kumi pekee.

Karibu sana tusome na kushirikishana pamoja yale tunayosoma.

Tatu; PERSONAL COACHING.

Mwezi disemba pia natoa huduma ya mimi kuwa kocha wako moja kwa moja. Hii ni huduma ambayo tunafanya kazi kwa karibu, kwa kitu ambacho unataka kufanyia kazi lakini unakwama.

Kwa huduma hii, chochote unachojiambia utaanza 2018, utaweza kukianza sasa 2017 na inapofika 2018 basi kinakuwa kimeshashika mizizi. Ni sawa na kusema utapanda mti mwaka 2018, ukiupanda sasa, inapofika 2018 unakuwa tayari una mizizi.

Hivyo kama umekwama na unataka kupiga hatua, hasa kwa mwaka 2018, wakati sahihi wa kuanza ni sasa, hivyo karibu kwenye huduma ya personal coaching tufanye kazi pamoja.

Nne; SEMINA YA KUUANZA MWAKA 2018.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tulishauanza mwaka mpya wa mafanikio 2017/2018. Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, tutakuwa na semina ya kuuanza mwaka 2018, ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao. Semina hii inafanyika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA ambapo ili uweze kushiriki unahitaji kulipa ada na kujiunga na kundi hili.

Huduma za GAME CHANGERS na LEVEL UP hazitakuwepo kwa mwezi huu wa 12. Lakini kwa wale wenye uhitaji wa huduma ya LEVEL UP unaweza kuweka miadi mapema kwa ajili ya mwezi januari 2018.

JINSI YA KUJIUNGA NA KULIPIA HUDUMA MBALIMBALI.

Malipo yote kwa huduma mbalimbali ninazotoa yanafanyika kwa njia ya huduma za fedha za simu.

MPESA namba 0755 953 887

TIGO PESA NA AIRTEL MONEY namba 0717 396 253.

Namba zote zimesajiliwa kwa jina AMANI MAKIRITA.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapaswa kulipa ada ya tsh elfu 50 (50,000/=) hii ni ada ya mwaka, ukilipa mwezi disemba 2017 ni mpaka mwezi disemba 2018. Malipo yanafanyika kwa namba zilizotajwa hapo juu. Ukishafanya malipo unatuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo na unapewa maelekezo zaidi.

Kujiunga na kundi la kusoma KURASA KUMI ZA KITABU kila siku unalipa tsh elfu kumi (10,000/=).

Kupata huduma ya PERSONAL COACHING tuwasiliane kwanza kabla hujalipa ada yake.

Mwisho kabisa, kama huna uwezo wa kulipia huduma yoyote kati ya hizo usione kama nimekutenga, bali endelea kutembelea www.amkamtanzania.com kila siku na utapata maarifa mengi kabisa bila ya kulipa ada yoyote. Ukishakuwa na uwezo wa kulipia huduma nyingine unakaribia na tunaendelea kuwa pamoja.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog