Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda. Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa misingi yetu ya Amka Mtanzania ya nidhamu, uadilifu na kujituma.

Rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena siku hii ya leo katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Kwa namna ya pekee rafiki yangu, nakusihi sana tusafiri pamoja hadi mwisho wa somo letu la leo ambapo leo tutakwenda kujifunza sehemu pekee ambayo huwezi kudanganya watu wote. Karibu sana tujifunze.

9bc1b-dunia

Tangu dunia ianze basi kitu pekee ambacho kimeweza kudumu mpaka leo ni ukweli. Ukweli huwa unajitetea wenyewe wala huhitaji kuupa rushwa. Ukweli ni kama uaminifu unapokuwa mtu mwaminifu unatenda mambo yako yote kwa uaminifu kuwe kuna mtu anakuona au kuwe na mtu hakuoni ila wewe kwa sababu unaishi uaminifu, unaishi uadilifu basi umeshachagua kuishi kwenye ukweli kwa sababu maisha yako binafsi yatajieleza yenyewe hakika mtu huyu ni mwaminifu.

Tunaweza kudanganya dunia lakini hatuwezi kujidanganya sisi wenyewe. Sisi tunajijua kuna wewe ambaye yuko ndani yako chochote unachofanya huwa anakuona hivyo wewe unaujua ukweli wote hata kama ukidanganya ila nafsi yako kupitia wewe anakusuta kabisa. Ukweli una gharama yake na kama umezoea maisha ya kuishi katika utapeli wa kudanganya watu ipo siku yatafikia kikomo kwa sababu huwezi kudanganya watu wote kwa muda wote bali unaweza kudanganya watu wachache kwa muda fulani.

Rafiki, aliyekuwa mwanamziki wa nyimbo za rege Bob Marley aliwahi kusema unaweza kudanganya watu wa chache kwa muda fulani lakini huwezi kudanganya watu wote kwa muda wote. Ukisema unaweza kuidanganya dunia kwa muda wote ni uongo kwa sababu uongo ni bidhaa ambayo hakuna mtu makini anayetaka kununua hivyo ukitegema uongo kumbuka kuwa uongo hauna thamani tena kwa dunia ya sasa. Unatumia nguvu nyingi kujitetea katika uongo lakini hutumii nguvu kuutetea ukweli kwa sababu ukweli huwa unajitetea wenyewe.

SOMA; Hii Ndiyo Hazina Kubwa Kuliko Zote Duniani.

Mpendwa msomaji, kama mtu amezoea kuishi kwa utapeli basi maisha ya utapeli huwa yana mwisho wake kwa sababu hakuna uongo unaodumu. Umezoea kudanganya watu itafikia mahali kila mtu atajua ukweli ni ngumu sana kudanganya watu wote kwa muda wote.

Hatua ya kuchukua leo, ishi uaminifu wako,ishi uadilifu wako kwani kupitia uaminifu utaweza kununuliwa kwa bei  ya juu sana kwa sababu uaminifu ni zawadi ghali mno huwezi kuipata kwa mtu wa kawaida au mtu rahisi kama alivyowahi kusema Warren Buffet. Uaminifu ni mtaji mkubwa sana katika mahusiano yetu kwani changamoto kubwa ya mahusiano ya leo ni kukosa uaminifu hivyo ukiwa ni mwaminifu basi utakuwa unaongeza uhai wa mahusiano yako.

SOMA; Huyu Ndiye Tapeli Mkubwa Anayewalaghai Watu Wengi Katika Maisha Yao.

Kwahiyo, kama unataka kupata umaarufu wa kudumu sema ukweli na kama unataka umaarufu kwa muda sema uongo. Utadanganya watu lakini kumbuka kuwa huwezi kudanganya dunia nzima kwa wakati wote. Udanganyifu ni maisha kifungoni kwani yanakunyima raha.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net  au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com kwa kujifunza zaidi. Asante sana.