Habari za leo rafiki yangu?

Kwa kipindi ambacho nimekuwa natoa huduma hizi za mafunzo ya mafanikio kwenye nyanja mbalimbali za maisha, nimekuwa naona namna ambavyo watu wengi wanapenda kupata haya maarifa.

Watu wengi sana wanahitaji kupata mafunzo kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Watu wana kiu kubwa ya mafanikio na wanakazana sana kuyapata.

Lakini kuna kitu kimoja ambacho wengi wana hofu nacho katika kupata maarifa haya. Watu wanaogopa kulipia huduma hizi za mafunzo au ushauri wakiona watapoteza fedha zao.

Wengi huona wakilipia fedha wanazoambiwa walipe, hawatapata thamani sawa sawa na walicholipia. Wengine pia wana historia ya kuwahi kulipia huduma kama hizi kwa watoaji wengine na hawakupata kile ambacho waliahidiwa kupata.

Hivyo wengi wanachagua kutokulipa, na wengine wanasema wazi, haya ninayopata bure yananitosha kabisa kufikia mafanikio makubwa. Huwa naumia ninapoona watu wenye uwezo wa kupiga hatua iwapo watapata maarifa sahihi wakiendelea kubaki pale walipo kwa sababu wanahofia kulipia ili kupata maarifa hayo.

Sasa kwa kuwa mimi nimejitoa kutoa huduma hii kwa kipindi chote ambacho nitakuwa hai, nimekuwa natoa nafasi ya mtu kupata mafunzo na hata ushauri ninaotoa bure kabisa. Ndiyo, zipo gharama za kulipa, lakini nawapa watu nafasi ya kupata bure kabisa, wasipoteze hata senti moja yao.

Na nafasi hii huwa ninaitoa kwa yeyote, ambaye anataka kunufaika nayo.

Ninachofanya ni hichi, ninakuambia wewe ulipie huduma yoyote unayotaka kulipia, kwa mfano kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ambapo unapaswa kulipa ada ya shilingi elfu 50 kwa mwaka, unalipa ada hiyo. Halafu unakaa mwaka mzima kujifunza na muda wowote, hata ile siku ya mwisho kabisa ya kumaliza mwaka tangu umelipia, unaniandikia na kuniambia, Kocha nililipie ada ya KISIMA CHA MAARIFA na kwa mwaka mzima hakuna chochote nilichojifunza, hivyo naomba kurejeshewa ada yangu. Na mimi, bila ya kukuuliza swali lolote, nakurejeshea ada yako kamili, bila ya kukata hata senti moja.

Sijui umenielewa hapo rafiki, yaani kama utalipia huduma yangu yoyote ile ninayoitoa, na ukawa hujanufaika nayo, yaani umejifunza, ukafanyia kazi laini hakuna manufaa yoyote unayoyaona kwako binafsi, unaniambia tu unataka kurejeshewa fedha zako na ninakurudishia.

Ndiyo huduma hizi zinanigharimu muda mwingi kuziandaa, lakini kitu cha kwanza ninachoangalia ni wale wanaozipokea kama zinawasaidia kwa chochote. Kama haziwasaidii hawapaswi kuzilipia, itakuwa ni wizi na haitajenga picha nzuri.

Hivyo rafiki yangu, kama unashindwa kulipia huduma kama ya KISIMA CHA MAARIFA kwa sababu unaona ada ni kubwa na huna uhakika kama utapata thamani halisi ya kile ulicholipia, wewe lipia kisha wakati wowote niambie tu kwamba huduma unazozipata hazina manufaa kwako na nitakurejeshea fedha zako, bila ya kukuuliza swali lolote.

Na kama huna fedha ya kujiunga, tafuta kwa namna yoyote ile, hata kwa kuomba au kukusanya michango, ili upate fedha hizo, kisha lipia na ukiona huduma hazikufai, niambie tu na nitakurejeshea fedha ulizotoa.

Kwa nini najiamini kiasi hichi, si watu watatumia nafasi hii vibaya?

Mtu mmoja aliwahi kuniuliza hivyo, kwa nini unajiamini hivyo? Huoni kwamba unawapa watu nafasi ya kukuibia, huoni kwamba mtu anaweza kulipia halafu akakaa mwaka mzima akaja kudai fedha zake?

Na mimi nikamjibu hivi kama mtu hataondoka ndani ya wiki moja, basi akikaa mwaka mmoja na akataka fedha zake, anastahili kuzipata, kwa sababu mimi ndiyo nitakuwa nimeshindwa. Kama kwa mwaka mzima nimeshindwa kutoa maarifa ya kumfanya mtu aondokane na fikra hizo basi nastahili kurejesha ada aliyolipa.

Kitu kikubwa ambacho nimekuwa nakiona kwa wengi wanaojiunga na huduma zangu, hasa KISIMA CHA MAARIFA, ni kadiri muda unavyokwenda, wanabadili namna wanavyofikiri na hata kufanya maamuzi kwenye maisha yao. Wanajikuta wanaweza kuzishinda hofu, wanapunguza sana tabia ya kuahirisha mambo na wanaanza kuona mambo yanawezekana.

Hata kama hawajapata fedha nyingi kwa kipindi hicho, wakijiangalia baada ya kujiunga na kabla ya kujiunga, kuna tofauti wanaiona. Na wengi wamekuwa wanasema, thamani wanayoipata, hailingani kabisa na fedha waliyolipa. Walicholipa ni kidogo ukilinganisha na namna maisha yao yalivyobadilika.

Kwa mfano, huyu ni mmoja wa watu waliojiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa kuwa nilisema wanaweza kurudishiwa fedha zao kama hawatanufaika, hivi ndivyo alivyoniandikia yeye mwenyewe;

Thamani ya Kisima cha maarifa

Kama unavyoona hapo juu rafiki yangu, hiyo ndiyo silaha yangu kwenye huduma ninayotoa, kuhakikisha watu wanapata thamani na kuweza kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.

Sikuahidi miujiza kwamba ukijiunga na huduma zangu hapo hapo utakuwa tajiri, matatizo yako yote yataisha na kuna njia za mkato za kufanikiwa. Ninachokuahidi ni kwamba, hatua kwa hatua, siku baada ya siku utaona mambo yako yanakuwa bora, kidogo kidogo. Kadiri unavyokwenda utakuwa unajiamini zaidi, kuona unaweza zaidi na hata kuzishinda hofu mbalimbali. Ukiongea mbele ya watu wataona una kitu cha tofauti, jinsi unavyofanya kazi au biashara yako itakuwa tofauti na wengine. Na hilo ndiyo muhimu sana.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na karibu sana kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018 itakayoendeshwa kwa njia ya wasap kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Nimekuandalia semina ya kipekee ya kuuanza mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa sana ambayo yanaanzia ndani yako mwenyewe.

Hii ni semina ambayo inafanyika mara moja tu na hupaswi kuikosa kama unapenda kupiga hatua na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.

Semina hii itakuwa ya siku tano na itaendeshwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, na kwa muda wako binafsi. Huhitaji kusafiri kwenda popote na huhitaji kuacha kazi zako ili kushiriki. Ni wewe kuhakikisha upo kwenye kundi na kufuatilia mafunzo kadiri ya muda wako.

Mada za semina.

Kwenye semina hii ya kuuanza mwaka 2018, tutajifunza mambo yafuatayo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Siku ya tano; hatua za kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo ni muhimu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 07/01/2018 ili uweze kujiandaa vyema na masomo haya ya semina.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

MUHIMU; Kama utalipia na kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na baadaye ukagundua kwamba huduma hiyo haikufai, nijulishe na nitakurudishia fedha zako. Ninachoweza kukuambia ni kwamba, neno langu ndiyo sheria yangu, na ndiyo imeniwezesha kuwa hapa na wewe, hivyo ninafanya kile ninachokuambia nitafanya.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, nafasi ni chache, chukua hatua leo, kwa sababu huna cha kupoteza.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,