Habari za leo rafiki yangu?

Mwaka huu 2018 unaendaje kwako? Naamini bado unaendelea kuweka juhudi kuhakikisha unakuwa mwaka bora sana kwako. Naamini bado hujakata tamaa na kuona hakuna jipya kwenye mwaka huu. Kwani jipya kwenye mwaka wowote ule unalitengeneza wewe mwenyewe.

Huwa nina utaratibu wa kuandaa semina ya kuuanza kila mwaka, semina ambayo huwa inafanyika kwa njia ya mtandao kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Semina hizi huwa naziandaa ili kuwasaidia watu kuepuka makosa yanayofanywa na wengi kipindi cha mwaka mpya, kuweka malengo mengi kwa hisia ambayo hawawezi kuyafikia.

2018 best year ever

Kwa mwaka huu 2018, semina ya kuuanza mwaka itaanza jumatatu ya tarehe 08/01/2018, na itakwenda kwa siku tano.

Kumekuwa na maswali ambayo yamekuwa yanaulizwa sana na wale ambao bado hawajajiunga na KISIMA CHA MAARIFA wakitaka kupata ufafanuzi kabla hawajachukua hatua ya kulipa ada na kujiunga. Nimekuwa nawajibu wale wanaouliza lakini najua kuna wengine wana maswali lakini hawapati nafasi ya kuuliza.

Hivyo hapa nimeyakusanya maswali yanayoulizwa sana na kuyapa majibu. Naamini majibu haya yatakuwezesha wewe kuchukua hatua sahihi kwako.

Swali; ada ni kubwa sana, kwa nini usipunguze ili wengi wanufaike na huduma hii?

Jibu; ni kweli, ada ni kubwa, shilingi elfu 50 siyo fedha ndogo, ni fedha unayoweza kuwa na matumizi nayo kwa vitu vingi. Lakini hiyo ni ada ya mwaka mzima, ambayo ukigawa kwa miezi 12 unapata chini ya elfu 5 kwa mwezi, kiasi ambacho kwa mambo utakayojifunza, siyo kikubwa.

Swali; je naweza kulipa kidogo kidogo?

Jibu; ndiyo unaweza kulipa kidogo kidogo, lakini hutaunganishwa kwenye kundi mpaka pale utakapokuwa umemaliza kulipa ada yote kamili. Na tarehe yako ya kujiunga itahesabiwa pale unapokuwa umeunganishwa baada ya kumaliza ada.

Swali; siwezi kuendelea kupata mafunzo wakati naendelea kulipa ada kidogo kidogo?

Jibu; hapana, tumeshajaribu njia mbalimbali za malipo, kuanzia njia ya mwezi, njia ya kulipa kwa awamu na kadhalika, nyingi zinaleta usumbufu. Njia bora kwa kila mmoja wetu ni kulipa mara moja na kujifunza kwa mwaka mzima.

Swali; je baada ya semina kuna mafunzo mengine yanayoendelea kwenye hilo kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Jibu; ndiyo, yapo mafunzo mengine mengi yanayoendelea kila siku. Kila siku tunaanza kwa tafakari ambayo inatupa kitu cha kuifikiri kwa kina kuhusu maisha yetu na mafanikio. Kila mwisho wa siku tuna nafasi ya kushirikishana yale tunayojifunza, pamoja na kuuliza maswali kwa changamoto ambazo mtu unapitia. Pia kila jumapili tuna madarasa mbalimbali kwa ajili ya kujifunza na kuchukua hatua zaidi. Kwa kifupi, unapojiunga kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unakuwa umeingia KISIMANI kweli, wewe ni kuchota tu maarifa.

Swali; kwa nini usiweke kundi la watu kuweza kushiriki semina tu na wakalipia kiasi kidogo na mwisho wa semina ukavunja kundi hilo?

Jibu; moja ya vitu ambavyo watu wamekuwa wanavikosa ni ukaribu na walimu au washauri wao. Watu huwa wanahudhuria mafunzo mengi sana, wanahamasika kweli kweli, lakini siku mbili baadaye wanarudi kwenye maisha yao ya zamani. Mimi niliandaa KISIMA CHA MAARIFA kuwa kinyume na hili, hii ni njia ya kuwa karibu na wale wanaojifunza kupitia maarifa ninayotoa, na muda wowote unaweza kuuliza chochote na nikakujibu. Pia utaendelea kupata msisitizo na hamasa itakayokuzuia usirudi nyuma hata kama unakutana na magumu.

Swali; sina shughuli yoyote ya kuweza kuniingizia kipato, kwa nini usiniunge nikajifunza na kisha nikakulipa nikishaingiza kipato?

Jibu; kama huna njia yoyote ya kukuingizia kipato, hujafikia sifa ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Iko hivi rafiki, blog ya AMKA MTANZANIA, www.amkamtanzania.com ndiyo hatua yako ya kwanza kwenye huduma ninazotoa. Ni blog ambayo ina mafunzo mengi na yote ni bure kabisa. Hivyo unachopaswa kufanya ni kuanza na mafunzo yaliyopo kwenye AMKA MTANZANIA, kuyafanyia kazi na kuona yana matokeo mazuri kwako, hapo sasa ndiyo unakuwa na hakika kwamba huyu mtu ana kitu kinachonifaa, ndipo uchukue hatua ya kulipia huduma nyingine kama KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama huna njia ya kuingiza kipato, rudi kwenye AMKA MTANZANIA, kuna makala karibu elfu 2, soma zote halafu andika mambo kumi unayoanza kufanyia kazi mara moja mwaka huu 2018.

Swali; nikishajiunga na KISIMA CHA MAARIFA ndiyo nakuwa na mafanikio makubwa?

Jibu; hakuna kitu kinafanya kazi kwenye maisha kama wewe mwenyewe hutafanya kazi. Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA utapata maarifa sahihi ya mafanikio, utapata majibu ya maswali yako yote uliyonayo. Lakini maisha yao hayatabadilika kama wewe hutachukua hatua. Hakuna njia ya mkato kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hakuna muujiza ni kujenga nidhamu ya kuchukua hatua kila siku na kuweza kuboresha maisha yako.

Swali; umesema kundi la KISIMA CHA MAARIFA limejaa, je nikilipa nitaunganishwaje?

Jibu; ndiyo nilitoa taarifa kundi limejaa, lakini baada ya mwaka kuanza, kuna nafasi chache zimepatikana, baada ya baadhi ya watu kukosa sifa za kuendelea kuwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo nafasi hizi zipo na zikijaa tena nitawajulisha. Kuhakikisha hukosi nafasi hizi chache, chukua hatua sasa, maana siwezi kukuahidi ni mpaka lini nafasi hizi zitakuwa wazi. Anayewahi ndiye anayepata nafasi.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na karibu sana kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018 itakayoendeshwa kwa njia ya wasap kupitia kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Nimekuandalia semina ya kipekee ya kuuanza mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa sana ambayo yanaanzia ndani yako mwenyewe.

Hii ni semina ambayo inafanyika mara moja tu na hupaswi kuikosa kama unapenda kupiga hatua na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.

Semina hii itakuwa ya siku tano na itaendeshwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, na kwa muda wako binafsi. Huhitaji kusafiri kwenda popote na huhitaji kuacha kazi zako ili kushiriki. Ni wewe kuhakikisha upo kwenye kundi na kufuatilia mafunzo kadiri ya muda wako.

Mada za semina.

Kwenye semina hii ya kuuanza mwaka 2018, tutajifunza mambo yafuatayo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Siku ya tano; hatua za kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo ni muhimu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 07/01/2018 ili uweze kujiandaa vyema na masomo haya ya semina.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

MUHIMU; Kama utalipia na kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na baadaye ukagundua kwamba huduma hiyo haikufai, nijulishe na nitakurudishia fedha zako. Ninachoweza kukuambia ni kwamba, neno langu ndiyo sheria yangu, na ndiyo imeniwezesha kuwa hapa na wewe, hivyo ninafanya kile ninachokuambia nitafanya.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, nafasi ni chache, chukua hatua leo, kwa sababu huna cha kupoteza.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,