Habari rafiki yangu?
Kila mwezi nimekuwa nakushirikisha kitabu kimoja kizuri ambacho unaweza kujisomea na kikakupa maarifa ya kuweza kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio zaidi kwenye maisha yako.
Kitu kimoja ambacho mimi binafsi nakiamini sana ni usomaji wa vitabu. Hii ni njia rahisi na ambayo kila mtu anaweza kuitumia kutoka pale alipo sasa. Kuna maarifa mengi sana ambayo yamefichwa kwenye vitabu na kama mtu utaweza kuyapata basi maisha yako hayawezi kubaki pale yalipo sasa.
Kila zama zimekuwa na changamoto zake, tangu zama za mawe, zama za chuma, mapinduzi ya viwanda na sasa zama za taarifa. Tunaishi kwenye zama ambazo, kelele na usumbufu zipo kwenye kila eneo la maisha yetu. Tunalala na kelele hizi na tunaamka zikiwa zinatusubiri pembeni ya vitanda vyetu.
Kifaa kidogo sana tunachokiita simu janja, yaani smartphone ndiyo kimeleta mvurugo mkubwa sana kwa wengi. Hii ni kwa sababu kifaa hichi kidogo, kimeweza kutuunganisha dunia nzima, na hivyo kwa masaa 24 ya siku, siku saba za wiki, tuna kila habari inayoendelea duniani.
Kwa mtazamo wa haraka tunaweza kuona kifaa hichi ni ukombozi wa kipekee, kwa kuweza kufanya mawasiliano kuwa rahisi sana kwa dunia nzima. Lakini tunapoangalia kwa undani na kufanya tathmini, ndipo tunapoona kwamba kifaa hichi kinakuja na hasara nyingi pia, ambazo kama mtu hutazijua, basi utaishia kuwa mtumwa na kushindwa kufanikiwa.
Mwandishi na mhadhiri Cal Newport amekuwa akiwashangaza watu kwa namna anavyoendesha maisha yake kwenye zama hizi. Kwanza huwa hatumii kabisa mitandao ya kijamii, anatumia email kwa kiasi kidogo sana, na kazi zake anazifanya kwa muda wa kazi, na baada ya hapo, kila saa kumi na moja jioni anakuwa nyumbani.
Licha ya kuwa mhadhiri wa chuo kikuu, Cal hajawahi kuonekana yupo ‘bize’ kwa kubanwa na kazi zake mpaka kuhitaji kufanya kazi kwa muda wa ziada. Wala huwa hashindwi kukamilisha majukumu yake kwa muda alioupanga.
Amekuwa akiweza kutimiza yote hayo kwa sababu amejifunza misingi ya maisha ya mafanikio kwenye zama hizi za kelele. Na misingi hiyo ameieleza kwa kina kwenye kitabu DEEP WORK ambacho anatuonesha ni kwa namna gani mtu unaweza kuweka akili na nguvu zako kwenye kile unachofanya, kuepuka usumbufu na kuweza kukifanya kwa ufanisi wa hali ya juu.
Najua kwa sasa changamoto za wengi wetu ni muda na mambo mengi ya kufanya. Hii ni changamoto ambayo tumekuwa tunajitengenezea sisi wenyewe kwa kukosa maarifa sahihi ya namna ya kuweka vipaumbele vyetu na kuepuka usumbufu.
Ni kupitia kitabu hichi cha DEEP WORK ambapo tunaweza kuzama kwenye kile tunachofanya na kuweza kupata matokeo bora sana.
Nakusihi sana rafiki yangu, soma kitabu hichi kwa mwezi huu wa Februari na mwaka huu 2018 utaweza kufanya mambo kiutofauti na kupata matokeo bora kabisa.
Jinsi ya kupata na kusoma kitabu hichi.
Unaweza kukipata kitabu hichi kwa nakala tete popote mtandaoni panapouzwa au kupatikana kitabu hichi.
Lakini pia utaweza kukipata kwenye kundi la KURASA KUMI ZA KITABU. Hili ni kundi maalumu la kusoma vitabu ambalo nimelianzisha na ili uwe kwenye kundi hili, lazima kila siku usome angalau kurasa 10 tu za kitabu. Kurasa kumi tu na ndani ya mwezi mmoja utakuwa umemaliza kusoma kitabu kimoja.
Ili kujiunga na kundi hili, unapaswa kulipa ada ya mara moja ambayo ni tsh 10,000/=
Karibu sana kwenye kundi la KURASA KUMI ZA KITABU na mwezi huu wa Februari tusome kitabu DEEP WORK.
Kujiunga tuma fedha, tsh 10,000/= kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenye namba 0717 396 253, ujumbe uwe na majina yako kamili na maneno KURASA 10. Muhimu, ujumbe tuma kwenye wasap namba 0717396253.
MUHIMU KABISA; Unapojiunga na kundi la KURASA KUMI ZA KITABU, maana yake unajijengea tabia ya kusoma kila siku, angalau kurasa kumi. Lakini pia unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wasomaji wengine kwa yale wanayoshirikisha. Hivyo unakuwa kwenye mazingira mazuri ya kujifunza kwa kusoma na kupitia wengine pia.
MUHIMU ZAIDI; Ndani ya kundi hili unaweza kuchagua kusoma kitabu chochote unachotaka wewe na kwa lugha unayotaka wewe. Vitabu vingi ninavyopendekeza vya kusoma ni vya kiingereza, lakini haimaanishi kama hujui kiingereza basi kundi halikufai. Badala yake unahitaji kutafuta vitabu vya Kiswahili na kuwa unavisoma kila siku. Muhimu kwenye kundi ni uwe una vitabu unasoma angalau kurasa 10 kila siku na kuwashirikisha wengine kile ulichojifunza.
Kama hujui unaweza kupata wapi au kupataje vitabu vya kiswahili, nitakushauri zaidi kwenye hilo.
Karibu sana kwenye kundi la KURASA KUMI, na karibu sana kwenye kusoma kitabu cha DEEP WORK. Kama utasoma kitabu hichi, ukakielewa na kufanyia kazi yale utakayojifunza, basi mwaka huu 2018 utaweza kufanya makubwa sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha
Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog