Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Amka Mtanzania?

Kama ungepewa nafasi leo  ya kuulizwa swali kwanini watu wa nchi hii wengi hawafaniki licha ya kuwa  na rasilimalii nyingi ukilinganisha na  nchi nyingine ungejibu nini?

Muda tulionao

Huenda utakuwa na majibu yako mengi sana juu ya swali hili ukipenda kunishirikisha juu ya jibu lako nitumie kupitia barua pepe yangu inayopatikana mwishoni kabisa wa makala hii. Kweli kwenye miti hakuna wajenzi na waswahili wanasema tena upele unamwota asiyekuwa na kucha.

Watu ambao wangezaniwa wangeweza kusaidia nchi yao kwa kufanya kazi na kuleta maendeleo  ni vijana lakini mambo yamekwenda tofauti. Badala ya vijana kutegemewa lakini inakuwa kinyume chake hii tunaweza kuita paradox yaani yule ambaye angepaswa kufanya ndiyo hafanyi na yule ambaye hakustahili kufanya ndiyo anafanya. Kwa mfano, yule ambaye alipaswa kufanya mazoezi kwa sababu ya kuwa na uzito mkubwa ndiyo hafanyi na yule ambaye hana uzito mkubwa ndiyo anafanya hii ndiyo tunaiitwa paradox.

Rafiki, ujana ndiyo fursa adimu sana ambayo ikienda hairudi tena. Hakuna watu wanaochezea fursa ya ujana kama vijana, ukitaka kujua ujana ni fursa nenda kamuulize mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 65, muulize tu swali hili je kama ungepewa leo fursa ya  kuwa kijana tena ungeweza kufanya nini ? utaona majibu yake kama ujana ni fursa au siyo fursa.

SOMA; Falsafa Bora Itakayokusaidia Kugusa Maisha Ya Watu Wengine.

Ujana ni fursa kwa sababu hiki ndiyo kipindi ambacho kijana yeyote anaamua kuishi maisha anayoyataka hapa duniani. Ni kipindi cha kutengeneza ramani ya maisha yake kwa ujumla, ni kipindi cha kutengeneza msingi wa maisha yake kwa ujumla. Ni kipindi cha kuamua hatima ya maisha yake, ni kipindi cha kuamua kuwa tajri au masikini kadiri ya mtazamo wake.

Ujana ni rasilimali nguvu nzuri ambayo usipoitumia vizuri ikienda utakuja kuumia sana baadaye. Kama leo uko kijana kumbuka kesho utakuja kuwa mzee je umejiandaaje na maisha ya uzee wako kama hujatengeneza leo ya ujana wako?

Vijana ambao wanategemewa ndiyo  wako bize na biko, kamari, tatu mzuka, starehe nyingi kuliko kufanya kazi.  Wanatamani maisha mazuri kwa kuongea huku wakiweka mikono mifukoni. Vijana wengi bado hawajajitambua kuwa kama ujana wao ni kipidni cha fursa ambayo ikienda hairudi tena.  Kazi ni rafiki mzuri amabye hajawahi kumuacha mtu hata siku moja, kazi ndiyo utu wa mtu usipofanya kazi utanuka na watu watakukimbia.

Hatua ya kuchukua leo, kama wewe ni kijana kumbuka unaishi mara moja tu na hakuna kipindi cha pili. Kama leo hutaki kulipia maisha yako ya ujana kwa hiyari utakuja kuyalipia ukiwa mzee tena kwa riba kubwa. Chochote unachokwepa sasa utafanikiwa kukikwepa lakini ni ngumu kukwepa matokeo yake. Hivyo wewe kama kijana amka na jitabue, wakati sahihi ni sasa usisubiri kupewa ruhusa.

SOMA; Kama Unafikiri Kwa Jinsi hii, Sahau Kuwa Tajiri.

Kwahiyo, kumbuka  kuwa mafanikio yoyote unayotaka katika maisha yako yanakuja kwa kutoa thamani. Hivyo kabla  hujapeleka fedha yako katika kamari je jiulize kuna thamani gani unayotoa kupitia mchezo huo.  Ili upate fedha unatakiwa utoe thamani na huo ndiyo msingi mkuu wa kupata fedha ukiona uko tofauti na njia hii ya kupata fedha basi uje unapoteza muda wako.

Ukawe na siku bora sana rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net kujifunza zaidi tembelea mtandao wa Kessy Deo ( www.mtaalamu.net/kessydeo )

Asante sana