Mpendwa Rafiki,

Wote sisi ni binadamu lakini ulishawahi kujiuliza kwanini tuna tofautiana? Tuna watu tofauti katika jamii yetu wanaofanya kazi tofauti tofauti, wako walio jiajiri, wako walio ajiriwa. Lengo la kuajiriwa au kujiajiri ni kwenda kupunguza au kutatua changamoto fulani katika jamii yako inayowasumbua  watu na wewe unakwenda kama mtatuzi.

Achana

Kuna kitu kinaitwa ushindani na ushindani siyo mbaya kama unashindana na wewe mwenye kuwa bora na siyo kushindana na mtu mwingine. Wewe kama ni mfanyabiashara usipoteze muda wako kushindana na mshindani wako badala yake shindana na wewe mwenyewe kuwa bora. Wafanyabiashara wanashindana na washindani  wao  badala ya kushindana na wao binafsi kuwa bora.

Huu siyo ulimwengu wa kushindana na mshindani wako badala yake wewe unatakiwa kushindana na wewe mwenyewe kuwa bora, shindana na wewe kutoa huduma bora kwa mteja wako, shindana na wewe mwenyewe kuzalisha bidhaa bora. Ukikazana kushindana na mshindani wako utasahau kufanya ya kwako yaliyo ya msingi. Ukipigania kutoa huduma bora, kuzalisha bidhaa bora kwa mteja wako hapo ndiyo utakuwa umeongea lugha yako lakini kama wewe unakazana na kushindana na wengine unakuwa unaongea lugha za wengine na kusahau yako sasa sijui itaongelewa na nani kama wewe mwenyewe unaidharau.

SOMA; Hii Ndiyo Sababu Kuu Moja Kwanini Watu Wanaajiriwa Au Wanajiajiri Katika Maisha Yao.

Huu ni wakati wa kupigania kuwa bora kwenye kila kitu ndiyo silaha yako. ukiwa umeajiriwa au umejiajri hakikisha unakuwa bora kwenye kile unachofanya. Mwangalie sana mteja wako kwani mteja ni mfalme yeye haangalii upinzani wako na mshindani wako bali anaangalia huduma bora. Mteja yeye anataka kile anachokitaka wala hahitaji sababu zako binafsi.

Rafiki, tunapoamua kufanya kitu chochote kile basi tuangalie kufanya kwa kuleta ubora na siyo kushindana na mtu. Pigania maisha yako kuwa bora badala ya kupigania kushindana na mtu. Ubaya wa kushindana ni kwamba huwa lazima mmoja ashindwe na mmoja ashinde lakini ukishindana na wewe peke yako unakuwa mshindi wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo, ushindani bora ulionao dhidi yako ni wewe kuwa bora. Kushindana hakuna faida kama wewe mwenyewe huna ubora unaotoa. Mjali sana mteja wako kwani mteja ni mfalme na sifa ya mfalme ni kutaka kile anachokitaka bila sababu yoyote ile. Toa huduma yoyote kwa ubora na siyo huduma ya kushindana.

SOMA; Mambo 10 Ya Kujifunza Kuhusu Fedha Na Utajiri Kutoka Kwenye Orodha Ya Mabilionea Ya Mwaka 2018.

Kwahiyo, watumie washindani wako kukupa hamasa ya wewe kuwa bora na siyo kuwa kama wao kushindana kwa kile wanachokifanya. Njoo na upekee wako kwenye kitu chochote unachouza ndiyo njia nzuri ya kujitofautisha na mwingine. Usitegemee kupiga hatua kama unafanya kitu hiko hiko kwa namna hiyo hiyo na huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Kama unataka kuanza kuimba, kufanya biashara, kuandika njoo na upekee wako ndiyo utaleta ladha lakini kama unashindana kuwa kama  wengine utapoteza ladha.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu  kwa kutembelea  hii hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana !