Habari wanamafanikio?

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa ya mabadiliko madogo kwenye DARASA LETU LA JUMAPILI ambalo kwa mara nyingi limekuwa linafanyika jumapili jioni.

Lakini kutokana na kuwa na majukumu mengi kiasi, jumapili nyingi zimekuwa zinanikuta nimebanwa kwenye kazi. Hivyo tumekuwa tunakosa madarasa haya ambayo ni muhimu sana kwetu kwa mafanikio yetu.

Ili kuondokana na hali hii ya kukosa madarasa haya ya jumapili, tunafanya mabadiliko kidogo.

Kwanza jina litakuwa DARASA LA WIKI badala ya DARASA LA JUMAPILI. Hivyo kila wiki tutakuwa na darasa moja la pamoja kuhusiana na yale maeneo muhimu ya mafanikio kwenye maisha yetu.

Darasa hili litafanyika siku yoyote kwenye wiki husika, lakini mara nyingi itakuwa kati ya Ijumaa, Jumamosi au Jumapili. Muda wa darasa ni ule ule, kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku. Saa ya kwanza ya darasa itakuwa nafasi ya kupata kile kilichoandaliwa, na saa ya pili itakuwa kwa ajili ya mjadala, michango zaidi na maswali na majibu.

Ili kuhakikisha wote hatukosi madarasa haya, mwanzoni mwa mwezi nitakuwa natoa ratiba ya madarasa ya mwezi mzima na siku za madarasa hayo. Hii itatusaidia kujua kwa hakika lini tuna darasa na hivyo kuweka ratiba zetu vizuri ili tusikose darasa.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunaishi misingi mbalimbali ya mafanikio. Na yapo maeneo muhimu sana ambayo tunayasisitiza kwenye kila maarifa tunayoyapata. Haya ndiyo maeneo ambayo madarasa yetu yatajikita pia.

Maeneo muhimu kwetu kwenye KISIMA CHA MAARIFA na ambayo tutakuwa tunapata madarasa mara kwa mara ni haya;

 1. Maendeleo binafsi, hapa tutajikita zaidi kwenye kujijengea tabia za mafanikio kama nidhamu, matumizi bora ya muda, kuacha kuahirisha mambo, kuepukana na usumbufu mbalimbali.
 2. Fedha na uwekezaji, hapa tutajifunza mbinu zote zinazohusu kupata fedha zaidi, kudhibiti matumizi, kuwekeza na aina mbalimbali za uwekezaji.
 3. Afya, hapa tutaangalia maeneo matatu muhimu ya afya zetu, mwili, akili na roho. Kwenye afya ya mwili tutakuwa tukijadili magonjwa mbalimbali na jinsi ya kujikinga au kuondokana nayo, kwenye afya ya akili tutajifunza njia za kudhibiti fikra zako na kujenga uwezo wa kufikiri na usomaji wa vitabu. Kwenye afya ya roho tutajifunza kuhusu falsafa ya maisha, hasa falsafa ya ustoa na tahajudi.
 4. Biashara, moja ya mahitaji muhimu unayopaswa kukidhi ili kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni kuwa na biashara, hata kama ni ndogo kiasi gani. Kwa kuwa kuendesha biashara kuna changamoto nyingi, tutakuwa tunapata madarasa ya biashara, kuanzia kuanza mpaka kukuza biashara yako na maeneo muhimu ya biashara kama mtaji, masoko, mauzo, mzunguko wa fedha na kadhalika.
 5. Ushauri juu ya changamoto mbalimbali. Maisha yana changamoto na kadiri tunavyofanikiwa, ndivyo changamoto zinavyokuwa kubwa zaidi. Hivyo tutakuwa tunapata madarasa ya kujadili changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye maisha na hatua tunazoweza kuchukua. Changamoto hizi zitatoka kwa kila mmoja wetu na pia kwenye taarifa za mwezi za kila mmoja wetu.
 6. Ushuhuda wa wenzetu waliopiga hatua fulani. Hakuna njia bora ya kujifunza kama kutoka kwa yule aliyefanya kitu. Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unakuwa umezungukwa na watu ambao ni wafanyaji na siyo wasemaji tu. Watu ambao wanajaribu vitu mbalimbali kwenye maisha yao na vinawapa majibu ambayo yanawafundisha zaidi. Iwe ni majibu mazuri au mabaya, yote ni darasa. Tutakuwa tunapata madarasa ya shuhuda za wenzetu kutokana na yale waliyofanya na matokeo waliyopata, hata kama siyo matokeo mazuri, na tutajifunza zaidi na hata kushauriana zaidi.

Hayo ndiyo maeneo sita ambayo madarasa yetu ya wiki yatakuwa yakiegemea. Yatakuwa ni masaa mawili ya wiki ambayo kosa chochote kwenye wiki yako lakini usikose madarasa hayo, kwa sababu lazima kuna kitu utaondoka nacho na iwapo utakifanyia kazi basi utapiga hatua zaidi.

Kila siku nakazana kuhakikisha KISIMA CHA MAARIFA kinakuwa thamani kubwa sana kwa wale wote ambao wanajiunga na huduma hii. Ninachofikiria ni kila mtu apate thamani ambayo ni mara kumi ya ada aliyolipia. Hivyo kwa kushirikiana kwenye madarasa haya, thamani hiyo itaweza kupatikana.

RATIBA YA MADARASA YA MWEZI APRIL 2018.

Mwezi april 2018 una majuma manne ambapo tutapata madarasa manne.

Ratiba ya madarasa hayo itakuwa kama ifuatavyo;

DARASA LA UWEKEZAJI KUPITIA MIFUKO YA PAMOJA NA VIPANDE.

TAREHE; 07/04/2018 (JUMAMOSI)

MAMBO TUTAKAYOJIFUNZA.

 1. Maana ya uwekezaji na umuhimu wa kila mtu kuwa mwekezaji.
 2. Aina mbalimbali za uwekezaji na jinsi ya kuchagua aina inayokufaa kulingana na umri na kipato.
 3. Uwekezaji wa mifuko ya pamoja na vipande, maana yake na mifano yake.
 4. Jinsi uwekezaji wa mifuko ya pamoja na vipande inavyofanya kazi.
 5. Jinsi faida au ongezeko la thamani linavyopatikana kwenye uwekezaji wa mifuko ya pamoja na vipande.
 6. Mfuko wa dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT) na aina ya uwekezaji unaopatikana kupitia mfuko huu.
 7. Jinsi ya kutumia dhana ya uwekezaji wa mfuko wa pamoja kwenye kukuza mtaji wa biashara na hata uwekezaji.
 8. Mjadala, shuhuda, maswali na majibu.

DARASA LA CHANGAMOTO ZA SAFARI YA MAFANIKIO.

TAREHE; 13/04/2018 (IJUMAA)

TUTAKAYOJIFUNZA;

 1. Muhtasari wa taarifa zetu za maendeleo ya mwezi machi 2018 na robo ya kwanza ya mwaka 2018.
 2. Mambo ya tofauti ambayo wenzetu wanayafanya.
 3. Mambo mazuri ambayo wenzetu wanafanya ambayo tunaweza kufanya na kupiga hatua.
 4. Changamoto ambazo wengi wetu tunakutana nazo na jinsi ya kuzivuka ili kupiga hatua zaidi.
 5. Mjadala, shuhuda, maswali na majibu.

DARASA LA AFYA; HATARI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NA JINSI YA KUJIKINGA NAYO.

TAREHE; 22/04/2018 (JUMAPILI).

MAMBO TUTAKAYOJIFUNZA;

 1. Umuhimu wa afya imara kwa maisha ya mafanikio.
 2. Mabadiliko ya hatari kutoka magonjwa yanayoambukizwa kwenda magonjwa yasiyoambukizwa.
 3. Aina za magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni hatari kwa maisha ya wengi.
 4. Mitindo ya maisha inayokaribisha magonjwa yasiyoambukizwa.
 5. Jinsi ya kutengeneza mfumo wa maisha ambao unakuepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
 6. Mjadala, shuhuda, maswali na majibu.

DARASA LA FALSAFA YA USTOA NA MATUMIZI YAKE KWENYE ZAMA TUNAZOISHI.

TAREHE; 28/04/2018 (JUMAMOSI).

TUTAKAYOJIFUNZA;

 1. Historia fupi ya falsafa ya Ustoa na wanafalsafa wanne walioikuza falsafa hii.
 2. Misingi mikuu minne ambayo falsafa ya ustoa inasimamia.
 3. Mfumo wa maisha kwa wanafalsafa wa ustoa, ambao unakuandaa kukabiliana na magumu ya maisha.
 4. Jinsi unavyoweza kuitumia falsafa ya ustoa kwenye maisha ya kila siku.
 5. Mjadala, shuhuda, maswali na majibu.

Haya ndiyo madarasa ya wiki kwa mwezi April 2018,kama unavyoona, yapo mengi ya kujifunza na yote yana lengo moja tu, kuhakikisha tunapata maarifa sahihi, ambayo tunaweza kuyafanyia kazi na maisha yetu yakawa bora kabisa.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA ILI KUSHIRIKI MADARASA HAYA NA KUJIFUNZA MENGI ZAIDI.

Rafiki, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA basi unakosa mambo mengi na mazuri.

Unakosa maarifa sahihi ambayo yatakuwezesha kufanya bora yanayokuletea mafanikio makubwa.

Karibu sasa ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata maarifa haya mazuri na muhimu kwa maisha yako.

Nafasi za kujiunga zipo na unachopaswa kufanya ni kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/=. Ada hii unalipa mara moja kwa mwaka, na utalipa tena baada ya miezi 12 kuisha tangu ulipolipa.

Namba za kufanya malipo ni MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253, majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Baada ya kutuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili pamoja na email yako kwa njia ya wasap namba 0717396253 kisha utaunganishwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Rafiki, usikubali kuendelea kukosa maarifa haya bora na ya kipekee kwako, jiunge sasa na KISIMA CHA MAARIFA, tuwe pamoja, tujifunze na kuhamasika ili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yetu.

Rafiki na kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0