Kila mtu anapenda mafanikio na kila mtu ana ndoto yake hivyo katika ndoto tunatofautiana kati ya wale ambao wanachukua hatua na wale ambao hawachukui hatua yoyote. Hivyo ndoto zetu tunazipima katika uhalisia wa kuchukua hatua.

Kuchukua hatua ya kwanza ni kama kuondoa laana katika ndoto yako lakini hii hatua ya kwanza ndiyo inakuwa ngumu kwa watu wengi kwa sababu ya kusubiri kuwa na utayari. Jambo lolote ambalo unataka kulifanya basi chukua hatua ya kwanza utakua umeshaondoa laana. Laana za ndoto nyingi ziko katika kutochukua hatua ya kwanza, hatua ya kwanza inaonekana ngumu kwani wengi wanakuwa na hofu je watachukuliwaje badala ya kuendelea kufikiria ondoa laana na chukua hatua ya kwanza.

Kitu kikubwa kinachosababisha watu wengi kukata tamaa katika ndoto zao ni kutokuanza kuchukua hatua. Mtu yeyote mwenye ndoto kubwa halafu hachukui hatua basi ni rahisi kukata tamaa katika kile anachoota. Tunakata tamaa kwa sababu hatuchukui hatua ya kwanza. Hatua ya kwanza ndiyo inatupa mwanga inaondoa ukungu uliokuwa unakufanya usione mbele.

2017 kwenda 2018

Hatua ya kwanza inaondoa laana zote, inaondoa hofu zote zinazokukabili. Wewe usihofu chochote wewe chukua hatua ya kwanza na dunia itamua yenyewe. Watu wanakusibiri wewe uwaambie unauza nini hivyo chykua hatua peleka bidhaa sokoni na acha wanunuzi waamue wenyewe. Huwa tunahofia hata kuweka bidhaa zetu sokoni usiwe na hofu peleka ujuzi wako na soko litaamua wenyewe.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Own The Day, Own Your Life (Imiliki Siku Uyamiliki Maisha Yako).

Ulishawahi kujiuliza ni nani anayepanga bei ya nyanya, maembe? Soko lenyewe ndiyo linaamua hivyo wewe usijali  kama una kitu unataka kuanza wewe, ondoa laana hiyo leo kwa kuanza na subiria matokeo.

Kama kuna mtu ulikuwa unataka kumwambia kitu na unakuwa unasita kila siku ondoa laana leo kwa kuchukua hatua ya kumwambia.

Hatua ya kuchukua leo, chukua hatua katika ndoto yako, usipochukua hatua unaweka laana ya kutofikia ndoto yako lakini pia unajikatisha tamaa wewe mwenyewe.

Hivyo basi, ukiweza kuchukua hatua ya kuanza basi ni mwanzo wa kufanikiwa kwa ndoto yako. hatua ya kwanza ndiyo huwa inakuwa laana kwa wengi. Ukiendelea kukaa bila kuchukua hatua unakuwa unapoteza ndoto yako na lazima utakata tamaa.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !