“Be patient and tough; one day this pain will be useful to you.” — Ovid

Amka mwanamafanikio,
Amka uipokee siku hii mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni siku bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUNA SIKU HAYO MAUMIVU YATALIPA…
Rafiki, safari ya mafanikio siyo rahisi, haijawahi kuwa rahisi na haitakuja kuwa rahisi.
Katika kuelekea kwenye mafanikio, kuna maumivu ya kila namna.
Maumivu ya kimwili kwa kuhitajika kuweka juhudi zaidi ya ulivyozoea,
Maumivu yanayotokana na kukosa unachotaka.
Maumivu yanayotokana na kushindwa.
Maumivu yanayotokana na kukatisha tamaa na wengine.

Licha ya maumivu haya, ambayo yatakiwa yanafuatana kila wakati,
Unahitaji kuwa mvumilivu na kuwa imara sana.
Maana maumivu yoyote unayopitia siyo ya kudumu,
Lakini pia hayataondoka kabisa, yatabadilishana na mengine.
Lakini kwa uvumilivu, subira na kuwa imara, utaweza kupata chochote unachotaka.

Kadiri unavyotaka makubwa zaidi, ndivyo utakavyoumia zaidi.
Na kama huumii, ni dalili kwamba hakuna makubwa unafanya, na hakuna dalili za wewe kufanikiwa.
Badala ya kutafuta njia isiyo na maumivu, au kuyakwepa maumivu, ni vyema ukajijenga kuwa imaranna ukawa mvumilivu.

Usipokimbia wewe, kile kinachokusumbua ndiyo kitakimbia.
Amka ukapambane na maumivu yakonya leo rafiki,
Na siki hii ikawe njema sana kwako.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha