Rafiki yangu mpendwa,

Kuna sababu kuu mbili huwa zinawasukuma watu kuingia kwenye biashara, na sababu hizo huwa siyo nzito sana hivyo kupelekea biashara za wengi kuyumba.

Sababu ya kwanza huwa ni kwa sababu mtu hana kitu kingine cha kufanya. Labda mtu ametafuta sana kazi na kukosa, au alikuwa kazini lakini kazi imeisha, labda amestaafu, au amesimamishwa au kufukuzwa. Hapa ndipo mtu anasema labda nijaribu biashara, na anajikuta ameingia kwenye biashara.

Sababu ya pili ni kwa sababu mtu anataka kuongeza kipato chake. Maisha yamekuwa magumu, kipato alichonacho hakitoshelezi, mahitaji ni makubwa na hivyo anaona njia pekee ni kuwa na kitu kinachoingiza fedha, na hapo anaingia kwenye biashara.

Sababu hizi mbili hazina ubaya wowote, kwa sababu kama huna cha kufanya na kuna biashara unaweza kufanya, ni vizuri ukafanya. Na pia kama kipato hakitoshelezi, kuingia kwenye biashara ni mpango mzuri.

Tatizo ni kwamba sababu hizo mbili huwa zinakosa msingi na moto wa kumsukuma yule aliyeingia kwenye biashara. Ambapo kukosekana kwa msingi na moto huo, kunamzuia mtu kukua zaidi, au kunamfanya ashindwe anapokutana na changamoto.

Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yoyote unayofanya, au unayotaka kufanya, kuna mambo matatu unapaswa kuyajua, na kuyajua vizuri kwenye biashara yako. Mambo hayo ni KUSUDI, DHUMUNI na LENGO la biashara unayoifanya au unayotaka kuifanya.

Karibu tujifunze mambo haya matatu kwa undani, halafu uangalie unawezaje kuyatumia kwenye biashara yako;

MOJA; KUSUDI LA BIASHARA.

Kila biashara inapaswa kuwa na KUSUDI lake, kusudi ni kwa nini biashara ipo. Kusudi la biashara ni lile tatizo kubwa ambalo biashara inatatua, ile huduma kuu ambayo biashara inatoa kwa wateja wake. Kusudi la biashara ni muhimu sana kwa sababu ndiyo linaiwezesha biashara kukua na kudumu.

Unapoingia kwenye biashara, lazima ujue umeingia kwenye biashara kwenda kufanya nini. Kuna shida gani kubwa ambayo watu wanayo na biashara yako inakwenda kuitatua. Kuna uhitaji gani mkubwa ambao watu wanao na biashara yako inatatua uhitaji huo. Jua kusudi la biashara yako, maana hilo ndiyo litakutofautisha na biashara nyingine yoyote.

MBILI; DHUMUNI LA BIASHARA.

Kuwa na kusudi la biashara pekee hakutoshi kuifanya biashara iendelee kuwepo. Ili biashara iwepo, inahitaji kuwa na wateja ambao wanaitegemea biashara hiyo. Na hapa ndipo dhumuni la biashara linapoingia.

Dhumuni la biashara yoyote ile ni kutengeneza wateja wanaoitegemea biashara hiyo. Kuna wale wateja ambao huja kununua na kuondoka, na kuna wateja ambao wanakuwa sehemu ya biashara. Dhumuni la biashara ni kutengeneza wateja ambao wanakuwa sehemu ya biashara, wanaitegemea biashara kwa kufanya maisha yao kuwa bora.

Hapa ndipo utoaji mzuri wa huduma kwa wateja na kujali kunaisaidia biashara kukua na kuendelea vizuri hata kama mambo ni magumu.

TATU; LENGO LA BIASHARA.

Katika hayo mawili yaliyopita, tumeona biashara kupata na kuwabakisha wateja, lakini wateja kuwepo tu kwenye biashara haina msaada kama biashara haina lengo kuu ambalo ni kutengeneza faida. Ili biashara iendelee, lazima itengeneze faida. Kama biashara haitengenezi faida, haitachukua muda, itakufa.

Hivyo ni lengo la kila biashara kutengeneza faida, ambayo itaiwezesha biashara hiyo kujiendesha na kufanikiwa zaidi. Japo mwanzoni inaweza kuwa vigumu kutengeneza faida, lakini kama yale mawili ya mwanzo yamezingatiwa vizuri, basi biashara itaweza kutengeneza biashara na kujiendesha yenyewe na hata kukua zaidi.

Hayo ndiyo mambo matatu muhimu sana kuyazingatia kwenye biashara unayofanya au unayokwenda kuanza;

Jua KUSUDI la biashara hiyo, kwa nini iwepo na inajitofautishaje na biashara nyingine.

Jua DHUMUNI la biashara hiyo, ambapo unapaswa kuwa na mbinu za kuwafanya wateja wajione kuwa sehemu ya biashara hiyo.

Na muhimu jua LENGO la biashara hiyo, ambapo unapaswa kuwa na njia bora za kutengeneza faida endelevu kwenye biashara yako.

BIASHARA NDANI YA AJIRA SOFT

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog