Rafiki yangu mpendwa,

Hakuna kipindi kizuri kukuza biashara yako na kupata mafanikio makubwa kama kipindi ambacho ni kigumu kiuchumi. Hii ni kwa sababu watu wengi wanakuwa wamepoa, wanakuwa wamekata tamaa na kuona hakuna biashara. Hivyo sehemu kubwa ya soko inakuwa haijafikiwa.

Hali ngumu ya kiuchumi huwa inaleta sononeko kwa kila mtu. Pale biashara zinapokuwa zinafungwa na nyingine kupunguza wafanyakazi, hali ya sonona hutawala sekta nzima ya biashara. Watu wanakuwa hasi na vyombo vya habari vinakuwa vinachochea hali hiyo ya sonona na uhasi.

Kutokana na watu kukata tamaa na soko kuwa halijatawaliwa vizuri, wewe unaweza kutawala vizuri soko na ukapata mafanikio makubwa kwenye nyakati  ngumu kiuchumi na hata uchumi unaporudi vizuri unakuwa kwenye nafasi bora zaidi.

MIMI NI MSHINDI

Karibu kwenye makala ya leo rafiki yangu, ambapo nakushirikisha mambo matano muhimu kuzingatia ili kuendesha na kukuza biashara yako kwenye nyakati ngumu kiuchumi. Ukizingatia mambo haya, hutafunga biashara yako na wala hutapata hasara. Wakati wengine wanalalamika mambo ni magumu, wewe utakuwa unaendelea kufanya biashara kama vile hakuna kilichotokea.

Moja; usijiunge na kundi la kueneza habari hasi.

Hali ni ngumu kiuchumi, kila mtu anasema hivyo, vyombo vya habari vinahubiri hilo, wafanyabiashara wenzako wanazungumzia hilo na wateja wanatoa kama sababu kwa nini hawawezi kununua.

Sasa usikubali kabisa na wewe kuwa mmoja wa wanaohubiri kuhusu hali ngumu ya kiuchumi. Usitamke hilo kwako mwenyewe na usilitamke kabisa kwa wateja wako.

Katika wakati hasi kama huo, mteja anataka kusikia habari za matumaini, ameshasikia sana kuhusu hali mbaya ya uchumi, wewe kumwambia haimwongezei chochote.

Kuwa chanzo cha habari za matumaini kwa wateja wako.

Nyakati ngumu kiuchumi wateja wanajali sana vitu viwili, fedha na kile wanachotaka. Hivyo tumia muda mwingi kumwonesha mteja wako kwa nini akinunua unachouza, kitamsaidia kupata fedha zaidi au kupunguza matumizi yake ya fedha. Mwoneshe kwa nini akinunua bidhaa au huduma unayouza, itamtatulia matatizo na kumpa mahitaji yake, huku ikimwokolea fedha nyingi ambazo amekuwa anapoteza.

Wahubiri wa habari mbaya za uchumi wapo wengi, usiwe mmoja wao. Wafanye wateja wapende kuja kwako, kwa sababu wanajua kwako wanapata matumaini ya maisha yao kuwa bora.

SOMA; Tofauti Ya Kusudi, Dhumuni Na Lengo La Biashara Na Jinsi Ya Kutumia Hayo Matatu Kukuza Biashara Yako.

Mbili; wafikie wateja wengi zaidi.

Nyakati ngumu kiuchumi, wafanyabiashara wenzako wanakuwa wamekata tamaa, wanajua hakuna wanunuaji na hivyo hawajisumbui kuwafikia wateja wengi. Hapa ndipo unaweza kujijenga zaidi, wakati wao wamelala na kusononeka na hali mbaya ya kiuchumi, ni muda wako kutawala soko.

Ni muda wako wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kuhakikisha watu wengi zaidi wanajua kuhusu biashara yako na jinsi inavyoweza kuwasaidia. Katika nyakati hizo ngumu kiuchumi, ndiyo unapaswa kuwa na mpango wa masoko wa kukuwezesha kuwafikia wengi zaidi.

Tumia njia rahisi na njia za bure kuwafikia wateja wengi wa biashara yako. Katika wakati mgumu kiuchumi, hata gharama za kutangaza biashara yako zinakuwa rahisi. Na yapo mengi unaweza kufanya kuwafikia wateja wako.

Tatu; pangilia upya bidhaa na huduma zako kwa namna ambayo mteja anaweza kumudu.

Katika nyakati ngumu kiuchumi, wateja wanaogopa sana kutoa hela, kwa sababu hawana uhakika wa kupata tena fedha. Hivyo kama unauza bidhaa au huduma ambazo ni za bei ya juu, wateja wanaweza kuogopa kulipa gharama kubwa kwenye kile unachouza.

Wakati huu unahitaji kujua ni kiasi gani wateja wako wanaweza kumudu kulipa, kisha kupangilia bidhaa na huduma zako vizuri kiasi kwamba wanaweza kulipia. Unaweza kupunguza baadhi ya vitu au ukagawa kwenye makundi tofauti na kuuza kwa bei tofauti. Pia unaweza kuongeza thamani zaidi na kuuza kwa bei ile ile.

Kitu ambacho unapaswa kuepuka wakati huu ni kupunguza bei ya kile unachouza. Ukipunguza unaweza kuuza sana mwanzoni, lakini jua umeingia kwenye shimo la kuua biashara yako. Usipunguze bei kwenye nyakati ngumu kiuchumi, badala yake pangilia upya bidhaa na biashara yako, kiasi kwamba mtu analipa kiasi kile kile, ila katika mpangilio ambao unaonekana ni mdogo kwake na anaumudu.

Nne; tumia muda wa ziada ulionao kufanya mambo mengi zaidi.

Wanasema kwamba akili tupu ni karakana ya shetani na mawazo hasi. Katika nyakati ngumu kiuchumi, utakuwa na muda mwingi ambao huna cha kufanya, kwa sababu wateja ni wachache. Sasa usikubali kabisa ukae mtupu, ukifanya hivyo ndiyo utakaribisha mawazo ya kukata tamaa na kuanza kufanya kama wengine wanavyofanya.

Katika nyakati ngumu kiuchumi unahitaji kutumia muda wa ziada unaopata kufanya mambo mengi zaidi. Ratiba yako ya siku nzima inapaswa kuwa imejaa. Usikubali kabisa uwe na muda ambao umekaa tu au unaongea na waliokata tamaa au kusikiliza habari.

Ongeza shughuli nyingi za kibiashara, ondoka kwenye eneo la biashara na tembea zaidi kujifunza na kuwafikia wateja wako. Weka muda wa kujifunza kwa kusoma vitabu vinavyokufanya ufikiri chanya na kuona hatua za kuchukua.

Yaani hakikisha siku yako nzima imepangiliwa na kila saa na kila dakika una cha kufanya. Kwa namna hii hutapata muda wa kusononeka na hutapunguza bishara yako kama wengine wanavyofanya.

SOMA; SEMINA; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Tano; rudi kwa wateja wako wa zamani na wateja ambao hawakununua.

Wakati biashara inaenda vizuri, kuna wateja ambao umekuwa unawasahau. Kuna wale wateja ambao walishanunua kwako mara moja au mara chache, lakini hawajanunua tena. Na pia kuna watu uliwashawishi kuhusu biashara yako, lakini hawakununua.

Katika nyakati ngumu kiuchumi ni wakati wa kurudi kwa wateja hawa. Unapaswa kuwa na mawasiliano nao na hivyo kuwatafuta na kutaka kujua wanaendeleaje. Jua lile tatizo ambalo ulikuwa unawasaidia kutatua wamefikia wapi na kwa sasa bidhaa au huduma wanapata wapi. Jua changamoto zipi wanakutana nazo sasa na waulize kama kuna chochote wanachohitaji uwasaidie. Pia katika kuwasikiliza, utaweza kuona wapi unaweza kusaidia zaidi.

Kumbuka wakati mgumu kiuchumi una muda mwingi, hivyo wasiliana na wateja wako wengi wa zamani na jua nini kinaendelea kwenye maisha yako. Ukionesha nia ya kuwa tayari kuwasaidia, utaweza kuwashawishi na kurudi kuwa wateja wako tena.

Jali sana kuhusu maendeleo ya wateja wako katika nyakati ngumu kiuchumi, jali sana kuhusu wao kuokoa fedha au kupata fedha zaidi na jali kutatua matatizo wanayopitia.

Ukifanya hivyo, utawasikia wengine wakisema kuhusu ugumu wa biashara, wakati wewe biashara yako itakua kwa kasi kubwa sana katika kipindi hicho ambacho wengine wanafunga biashara zao.

Rafiki yangu, zingatia sana mambo hayo matano niliyokushirikisha hapo juu, na kama umejitoa kweli, kama kweli umepanga kuikuza biashara yako, iweze kudumu kwa nyakati ngumu na hata nyakati nzuri, nina kitu kizuri sana nimekuandalia. Soma maelezo yanayofuata hapo chini na chukua hatua leo hii ili uweze kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa sana.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog