Rafiki yangu mpendwa,

Zipo sababu mbalimbali za kuingia kwenye biashara, wengi wanaingia kwa sababu hawana cha kufanya na wanataka fedha zaidi. Na wapo wanaoingia kwa sababu wanataka kufanikiwa zaidi, wanataka kutengeneza kitu kitakachosimama kwa miaka mingi zaidi.

Nimekuwa nawaambia kitu kimoja, biashara yoyote unayotaka kujihusisha nayo, angalia miaka 50 ijayo, kama huwezi kuendelea kuifanya kwa miaka 50 inayokuja, achana nayo, siyo biashara sahihi kwako.

Watu wengi wanaoingia kwenye biashara hawana maono makubwa na ya muda mrefu. Wanachoangalia wao ni matokeo ya haraka wanayoweza kupata, faida ya haraka wanayofikiria kupata na kuishi maisha wanayotaka. Lakini huu siyo uhalisia, na sababu ya biashara nyingi kufa ni watu kuishi maigizo ya aina hiyo.

Leo napenda nikushirikishe kitu kimoja muhimu sana kufanya kwenye miaka 10 ya mwanzo ya biashara yako kama unataka mafanikio makubwa. Jambo unalokwenda kusikia hapa siyo zuri wala la kufurahisha, na kama huna ngozi ngumu utachukia na kujisikia vibaya. Na kwa kuwa huwa siandiki kukufanya ujisikie vizuri, bali kukupa ukweli, halafu wewe uchague unafanya nini na huo ukweli, nitakupa ukweli kama ulivyo.

Chochote

Miaka kumi ya mwanzo ya biashara yako, unapaswa kurudisha asilimia 80 ya faida unayoipata kurudi kuikuza biashara zaidi. Hii ina maana kwamba, sehemu kubwa sana ya faida unayoipata kwenye biashara, inapaswa kurudi kuiboresha na kuikuza zaidi biashara yako.

Wewe kama mmiliki wa biashara unapaswa kutumia sehemu ndogo sana ya faida unayopata kwenye biashara, chini ya asilimia 20 kwenye matumizi yako binafsi. Lakini sehemu kubwa, asilimia 80 inapaswa kurudi kwenye biashara, ili kuiboresha na kuikuza biashara zaidi.

Lakini hivi sivyo watu wanavyofanya, watu wanaanza biashara leo, na hata mwezi haujaisha wanatumia faida yote inayopatikana kwenye biashara hiyo. Na kama faida haitoshi kwenye matumizi yao, wanakwenda mbali zaidi na kutumia mtaji wa biashara.

Unafikiri kwa nini biashara nyingi zinakufa? Biashara haifi kwa sababu mauzo ni madogo au faida ni ndogo, biashara inakufa kwa sababu mtaji unatumika kwa mambo yasiyohusu biashara. Pale mtaji unapotumika na mwenye biashara kama sehemu ya kula, au unapotumika kulipa kodi au gharama nyingine za biashara, lazima biashara ife. Na kama umewahi kuanzisha biashara na ikafa, angalia kwa kina na utagundua ulianza kutumia mtaji kwa shughuli zisizohusisha biashara moja kwa moja.

Lakini Kocha asilimia 20 ni ndogo sana kuendesha maisha, maana nategemea biashara kuendesha maisha.

Najua asilimia 20 ya faida ni ndogo sana, na hapo una mambo mawili muhimu ya kufanya.

Jambo la kwanza ni kurahisisha maisha yako, kwa miaka 10 ya kwanza ya maisha yako, hupaswi kununua kitu ambacho usipokinunua hutakufa. Unajenga himaya, unahitaji kuweka nguvu zako zote pale, usitawanye fedha yako kwa vitu vya kupita.

Hivyo maisha lazima yatakuwa magumu, na yatakuwa magumu kweli, hutaweza kununua chochote unachotaka, na pia wengi watakuona kama unajitesa, lakini wewe unajua nini unafanya.

Hichi ni kipindi ambacho unahitaji kujifunga mkanda kweli, na muda wako mwingi unapaswa kuwa kwenye biashara na hapo hutapata muda wa kununua vitu ambavyo havina maana kwako.

SOMA; Tofauti Ya Kusudi, Dhumuni Na Lengo La Biashara Na Jinsi Ya Kutumia Hayo Matatu Kukuza Biashara Yako.

Jambo la pili na la muhimu sana ni kuongeza faida kwenye biashara yako. Kuna kiwango cha chini kabisa cha kuishi kwa ugumu, ambapo huwezi kwenda chini ya hapo. Kwa mfano lazima ule, lazima familia yako ipate matumizi ya msingi. Na kama asilimia 20 ya faida ni ndogo sana kuweza kuhudumia hayo muhimu, hupawi kuchukua zaidi kwenye biashara yako, bali unapaswa kuongeza faida zaidi.

Hapa ndipo muhimu sana, maana ndipo utakapoiwezesha biashara yako kukua zaidi na zaidi. Ukipata hasira kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu sehemu kubwa ya faida inarudi kukuza biashara, usipunguze faida hiyo, bali iongeze zaidi.

Kwa mfano, ukiongeza faida ya biashara yako kwa asilimia 50 kwa mwaka, maana yake utakuwa umeongeza kipato chako kwa nusu, yaani ile asilimia 20 unayojilipa, itaongezeka zaidi. Kwa mfano kama umekuwa unapata faida ya milioni 20 kwa mwaka, asilimia 20 ya faida hiyo itakuwa milioni 4. Kama utaongeza faida hiyo kwa asilimia 50, ukapata faida ya milioni 30 kwa mwaka, asilimia 20 yake itakuwa shilingi milioni 6. Sasa unaona hapo jinsi umeongeza kipato chako bila ya kugusa faida inayorudi kwenye biashara yako?

Sasa najua nini unafikiria, najua unasema huwezi kuongeza faida kwa asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja. Najua unafikiria ukijitahidi sana unaweza kuongeza asilimia 20. Na hapo ndipo ninapotaka kukusaidia, ndipo ninapotaka upate maarifa sahihi, ili biashara yako ikue sana na wewe uwe na maisha bora pia.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji