Rafiki yangu mpendwa,

Karibu kwenye makala ya ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa. Kwenye makala ya leo tutakwenda kuangalia mambo muhimu ya kuzingatia ili kuweza kukuza biashara ya huduma.

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara kwa mara, zama hizi kila mtu anapaswa kuwa na biashara. Biashara siyo tu kitu cha kufanya kama huna kingine cha kufanya, au kitu cha kufanya ili kupata kipato cha ziada, bali ndiyo njia bora ya kujijengea uhuru wa kipato.

Ni kupitia biashara ndiyo unaweza kutengeneza kipato kisichokuwa na ukomo, hakuna wa kukupangia ulipwe kiasi gani, soko litakulipa kulingana na huduma unayotoa.

Lakini kuanzisha na hata kukuza biashara siyo rahisi, wengi wamejaribu na kushindwa. Ili wewe rafiki yangu usishindwe, nakushirikisha mambo muhimu ya kuzingatia pale unapoanza biashara ya huduma ili iweze kukua na uweze kufanikiwa sana.

BIASHARA NDANI YA AJIRA SOFT

Msomaji mwenzetu alikuwa na haya ya kutuambia alipotuandikia kuomba ushauri kwenye hili;

Naomba kufahamu vitu vya msingi wakati ukitaka kuanzisha biashara .Mimi ni fundi cherehani nifanye nini ili nipanue ofisi yangu. – Simon J. M.

Rafiki Simon pamoja na marafiki wengine, kuanzisha na kukuza biashara yoyote kunahitaji mtu kujua nini hasa unataka kufanya, kuweka juhudi kubwa mno kwenye kufanyia kazi na kuwa mvumilivu, kwa sababu itakuchukua muda kupata unachotaka.

Biashara yoyote haihitaji haraka na kutafuta njia za mkato, pia haihitaji mtu ambaye hajajitoa kweli, kwa sababu mwanzoni tu utakutana na changamoto ambazo zitakuondoka kama hujajitoa kweli.

Ili kuweza kukuza biashara ya huduma, na kwa upande wa cherehani kama mwenzetu alivyoomba ushauri yafuatayo ni muhimu kuzingatia;

  1. Bidhaa na huduma ziwe bora sana.

Lazima uanzie kwenye kile ambacho unakitoa, kiwe bora na kiwe cha kipekee. Lazima utoe kitu ambacho mteja siyo rahisi kukipata kwa watoa huduma wengine. Lazima ujijengee jina kama fundi au mtoaji wa huduma bora za mashono na hata bidhaa za nguo.

Lazima uweke viwango vikubwa sana kwenye kila unachofanya, usifanye kwa sababu tu unataka upate fedha, fanya kwa sababu unataka kuacha alama fulani.

Uzuri wa biashara ya huduma za ushonaji, matangazo ni bidhaa yenyewe. Ukimshonea mtu nguo nzuri, ambayo watu hawajazoa kuona, kila atakapoivaa watu watamuuliza umeshona wapi, na yeye atawaambia hivyo watakuja kwako. Hivyo kila nguo unayoshona, jua ni tangazo la kazi zako, itendee haki kwa kuifanya kuwa ya kipekee.

  1. Fanya neno lako kuwa sheria, timiza unachoahidi.

Watoaji wengi wa huduma za ufundi huwa hawaaminiki. Mpaka watu wamekuwa na kauli kwamba fundi wa kweli ni kinyozi, wengine wote ni wababaishaji. Usikubali kabisa mteja wako yeyote akaondoka na mtazamo huo. Kama unamwambia mtu atapata nguo baada ya wiki moja, mwambie kabisa siku na muda ambao atakuja kuchukua nguo yake. Na fanya kila unalopaswa kufanya kuhakikisha huzidishi hata dakika moja, mteja akija muda uliomwahidi akute nguo yake ipo tayari.

Yaani usifikirie hata kidogo sababu ya kumpa mteja, kwamba ulikuwa na kazi nyingi, au sijui ulikwama wapi. Ukianza kutoa sababu hizo, mteja anapata picha kwamba umeona kazi yake siyo muhimu, hujamthamini na hatorudi tena. Unahitaji kuwajengea wateja wako mtazamo kwamba neno lako ni sheria, ukisema kazi inamalizika siku fulani inamalizika kweli.

  1. Kuwa na watu wa kukusaidia, usikazane mwenyewe.

Kosa kubwa wanalofanya watoa huduma wengi ni kufanya kila kitu wao wenyewe. Unakuta fundi wa nguo anafanya kazi zote mwenyewe, hana wa kumsaidia na hilo linasababisha kazi za wateja wengi kuchelewa.

Kama unataka kukuza biashara yako, unahitaji kuwa na watu wa kukusaidia. Hata kama wewe ndiye unayeweza kukamilisha kazi vizuri, kuna kazi ndogo ndogo ambazo unaweza kuwapa watu wakusaidie.

Na njia bora ya kufanya hivyo ni kugawa kazi zako kiasi kwamba fundi wa kawaida anaweza kukusaidia. Mfano kuchora kitambaa kisha kumpa mtu akate kwa namna ulivyochora, au kushona baada ya kuwa umekata, na hata kufanya kazi za kumalizia kama kuweka zipu, vifungo na kadhalika.

Kuwa na wasaidizi wengi lakini mwisho kabisa kuwa mtu wa kuikagua nguo na kuhakikisha imefikia viwango ulivyojiwekea wewe mwenyewe.

Kadiri unavyokuwa na wasaidizi wengi, ndivyo unavyoweza kumaliza kazi nyingi na kutokuwaangusha wateja wako.

  1. Usisubiri mpaka wateja waje, wafuate kule walipo.

Kwanza kabisa andaa kielelezo cha kazi zako, kuwa na mitindo ya kazia mbayo unaifanya na andaa kijitabu chenye kazi zako bora kabisa. Sasa kipindi ambacho hakuna wateja wengi, unaweza kuzunguka maeneo ambayo wateja wako wanapatikana na kuwaeleza juu ya uwepo wako na aina ya kazi unazofanya.

Unaweza kutembelea maofisi mbalimbali na kuwaonesha wateja watarajiwa aina ya huduma unazotoa na kuwashawishi wawe wateja wako. Kwa njia hii utaweza kuwafikia wengi zaidi.

Pia unaweza kutumia mitandao ya kijamii kuonesha kazi zako bora na kuwafanya wateja wajue uwepo wako.

Muhimu zaidi tumia wateja ambao tayari wameshapata huduma kwako kuwafikia watu wengi zaidi. Kila anayepata huduma kwako, anawajua watu wengine ambao watafurahia huduma zako, waombe wakuunganishe na watu hao.

  1. Toa huduma bora sana kwa wateja.

Jinsi unavyowapokea watu kwenye biashara yako, jinsi unavyowahudumia, jinsi unavyopokea malalamiko yao na jinsi unavyowafanyia kazi zao kunaweza kuwafanya wateja wakupende na kuipenda biashara yako au waichukie.

Unahitaji kutoa huduma bora sana kwa wateja wako, wateja wajisikie vizuri wanapokuja kwenye biashara yako, wateja wajisikie ni wa kipekee kabisa. Wateja wako wanapaswa kuona wanathaminiwa na wanapata siyo tu kile walichotegemea, lakini zaidi ya hapo.

Unapaswa kuwafanya wateja wako waone kama wamekuibia, waone thamani waliyopata haiendani kabisa na gharama walizolipa, kwa njia hii utawafanya warudi tena na tena na kuwaleta wengine pia.

Pamoja na hayo muhimu sana kwenye ukuzaji wa biashara yako, kuna eneo moja unapaswa kuliangalia kwa kina sana. Eneo hilo ni kutengeneza faida kwenye biashara yako. kama biashara haipati faida, itakufa, haijalishi ni nzuri kiasi gani, faida ndiyo damu na pumzi ya biashara. Hivyo unapaswa kuiendesha biashara yako vizuri na kutengeneza faida kubwa.

Ili kuweza kuongeza faida kubwa kwenye biashara yako, nimekuandalia mafunzo maalumu ya kukuwezesha kukamilisha hilo. Ni semina bora na ya kipekee sana kwa eneo la kutengeneza faidia kwenye biashara yako. Karibu sana ushiriki semina hii;

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji