Mpendwa rafiki yangu,

Fedha inahitaji nidhamu sana, haijalishi una kipato kikubwa au kidogo kiasi gani lakini thamani ya fedha inaonekana na mtu aliyeishika pesa hiyo kwa mfano, watu wawili wamepewa shilingi elfu 10 mmoja akaenda kula chips kuku ile elfu 10 yake na mwingine akaenda kuiwekeza ile elfu 10 yake yupi hapo atakuwa ameipandisha tathamani fedha yake? Ni yule aliyeenda kuwekeza.

Unatakiwa kujiuliza je wewe ni mtu unayeongeza thamani ya fedha zako au unashusha?

FEDHA KWA BLOG

Katika mambo ya fedha tunapaswa kuwa makini sana kupita maelezo, ni kawaida sana kwa watu wengi kuishi juu ya kipato chao, hii ni kwa sababu matumizi yanakuwa mengi kuliko kile kinachoingia. Kitu cha kuwa makini nacho pale kipato chako kinapoongezeka ni hichi; dhibiti matumizi yako, kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka.

Usipokuwa makini utakuwa huna unachokifanya, unaweza ukawa na kipato cha kawaida tu lakini pale unapoongeza kipato na matumizi yanaongezeka hivyo unatakiwa kuwa makini sana na matumizi usipokuwa makini lazima utayumba. Mbabe wa mambo yote haya katika masuala ya fedha ni nidhamu ukishakuwa na nidhamu umeshakuwa mbabe wa fedha zako hivyo siyo rahisi sana kama wewe ni mbabe wa fedha zako halafu zitumike hovyo.

SOMA; Usisingizie Fedha Tena; Njia Saba Za Kupata Mtaji Wa Kuanza Biashara Hata Kama Huna Pa Kuanzia Kabisa.

Unatakiwa kuwa mtu wa kusema hapana, kuwa na matumizi muhimu tu yaani yale ambayo ukiyakosa na maisha yako hayaendi. Achana na matumizi ambayo siyo muhimu kwako na kuwa mtu wa bejeti kali, kitu ambacho hakipo katika bajeti yako usihangaike kukinunua, jinsi unavyokuwa makini na fedha zako ndivyo na fedha zinazidi kuwa rafiki mzuri na wewe.

Hatua ya kuchukua leo; fedha huwa zinakwenda kwa mtu anayejali pesa, je wewe unazijali? Kuwa na nidhamu ya fedha, dhibiti matumizi yako na ongeza kipato chako.

Hivyo  basi, usipokuwa makini katika mchezo wa fedha lazima utashindwa. Mchezo wa fedha unahitaji nidhamu ya hali ya juu, watu watakuona siyo mtu wa kawaida lakini utafanikiwa kwa nidhamu unayoweka.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !