Mpendwa rafiki yangu,
Watu wamekuwa na mioyo migumu sana, imejaa chuki, wivu na yote haya yanakuja kuzaa vitu hasi katika maisha yetu. siku zote chuki huzaa mauti na upendo huzaa upendo hivyo tunapojichagulia maisha ya kuishi kwenye vinyongo ni kama tumechagua kujimaliza sisi wenyewe.
Kuishi bila kusamehe ni mzigo mkubwa sana ambao umechagua kuubeba wewe mwenyewe. Tunapata matatizo mengi katika maisha yetu lakini kutokusamehe ni tatizo kubwa zaidi kwani wengi wanakuwa wanaishi maisha kama vile wako vifungoni.
Unatakiwa kuachilia yote, mfutie deni na ishi maisha yako, huna haja ya kuwabeba watu. Tunapokataa kusamehe maana yake tumeruhusu akili zetu kutawaliwa na wale waliotukosea. Muda mwingine hata wale waliotokosea hawana hata habari kama wametuumiza na hata kujali pia hawajali hivyo yeye anaendelea na maisha yake wewe ukipata shida, kama mwenzako analala na kukoroma wewe hupati usingizi. Hivi kuna faida gani unayoipata pale unapokaa na maumivu ya kutokusamehe?
Msamaha ni kuondoa uchungu ulioumbika ndani ya moyo, kama unataka kuondoa uchumgu ulioko ndani yako kubali kusamehe sasa, samehe ili uweze kusamehewa, samehe ili mambo yako yaende, jiondoe katika kitanzi na kuwa huru leo.
SOMA; Hii Ndio Dayari Unayopaswa Kwenda Kuichoma Moto Leo Katika Maisha Yako.
Mtu mmoja aliwahi kusema, kusamehe ni kama kumwachilia mfungwa huru na baadaye unakuja kugundua kuwa mfungwa mwenyewe ulikuwa wewe. Mwachilie mfungwa wako huru ambaye ni wewe mwenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; waachilie wafungwa wote uliowafunga ili uwe huru, wasamehe wale waliokukosea ili uwe huru kiakili, kimwili hata kiroho.
Hivyo basi, maisha yanakuwa magumu sana kama hayana msamaha kwa sababu kila siku ya maisha yetu huwa tunafanya makosa na kila siku tunatakiwa kusamehe na mtu ambaye hasamehi ni amechagua maumivu makali.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net
Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti hii hapa www.mtaalamu.net/kessydeo .
Asante sana na karibu sana !